Daniel Ngowi na Aloyce Joseph wakiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro walipoipandisha bendera ya Taifa ikiwa ni kilele cha Kampeni ya Kilimanjaro Jivunie uTanzania iliyokuwa ikiendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kusherekea miaka 50 ya Uhuru.
Aloyce Joseph (kushoto) na Daniel Ngowi wakiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro walipoipandisha bendera ya Taifa ikiwa ni kilele cha Kampeni ya Kilimanjaro Jivunie uTanzania iliyokuwa ikiendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kusherehekea miaka 50 ya Uhuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. hayo matambara machafumachafu ni ya nini huko juu?

    ReplyDelete
  2. kwa kufafanua zaidi ni katika picha ya pili ambapo matambara ninayoyazungumzia yanaonekana hovyo hovyo

    ReplyDelete
  3. sisi tuliopanda mlima huu na mengine huwa tunaacha kitu chako mlimani kuonesha kwamba ulikuwa hapo, hivyo vitambaa ni vya wale waliopanda kabla

    ReplyDelete
  4. Hongera TBL na zaidi hongera kwa timu iliyoweza kupanda mpaka kileleni.

    Tembeatz.blogspot.com

    ReplyDelete
  5. duh.. hayo mavazi na baridi lake huko!!

    ReplyDelete
  6. Duh Dani unatisha Kk, yaani hapo i'm sure ni below -5C lakini umetulia na T-shirt, next time i get friend want to climb Kili nitakutumia, good job!!!

    ReplyDelete
  7. Mnaonaje mkajenga bendera yakudumu huku kiboni na kila atakae panda akaona kumbukumbu.

    ReplyDelete
  8. hivi kwanini wasiweke bango zuri lenye kupendeza wanaacha hivo vibao vilivyochoka na nguzo za miti

    ReplyDelete
  9. HONGERENI. LAKINI TBL MNGEENDA HATUA MOJA MBELE YA KUTENGENEZA BANGO LENYE HADHI KUONYESHA KILELENI MAANA BANGO LIKIWA ZURI NI KIVUTIO HATA KWA WANAOPIGA PICHA HUKO, NA HATA INAONYESHA KWAMBA TUNAUTHAMINI MLIMA KILIMANJARO.

    ReplyDelete
  10. Sisi wahifadhi kila kitu kinatakiwa atleast kuwa nachuro so halihitajiki bango la kisasa huko.. na Marketing ya Mlima si lazma kuweka bango la kisasa ila matangazo via njia mbalimbali... Mabango ya Kisasa ni Getini wakati wa kuingia mbugani.

    ReplyDelete
  11. Hayo sio matambala machafu bali ni Tibetian prayer mtu kaacha hapo kileleni..hawa jamaa watakuwa wako fit kupanda hadi kileleni kwa haraka kiasi hicho?..

    ReplyDelete
  12. Thamani waliona kuupigia kura ili uingizwe katika maajabu saba ya dunia. Yaani wenyewe hatubuni mpaka aseme au aanze mzungu.

    Mimi nilibahatika kutembelea baadhi ya nchi sa huku ughaibuni. Yaani miongoni mwa sehenu ambayo sisahau ni pale tulipotembelea mapango ya chini ya mlima. Mle ndani wameingia mpaka umeme. sehemu au maeneo mapana wameweka viti meza nk. Yaani wanathamini sehemu za utalii.

    Kama wenzangu walivyosema, naunga mkono; tuwekeni vibao angalau vinvyovutia. Yaani miaka 50 ya Uhuru, bado mabango yaliyochoka!!!

    Usipokipenda chako mwenyewe, utawashawishi vipi watu wapige kura ili kuwekwa katika hayo maajabu?

    Wakati umefika, tujitathmini wenyewe.

    ReplyDelete
  13. kama siku hizi lileleni kilimanjaro unavaa tisheti then barafu kwisha kazi

    ReplyDelete
  14. Sasa haki imetendeka kweli?...inaonekana Yanga ndio imefanikisha bendera ya Tanzania kufika kileleni mlima Kilimanjaro,,,angalia jezi tu!...TBL hii imekaa sawa?

    Yanga walilalamika ktk nembo ya ngao ya Hisani ya Vodacom kuwa na rangi za Simba.

    ReplyDelete
  15. JAMANI NIMESIKIA MAONI YENU ILA TUNANGOJA MWEKEZAJI AJE AWEKEZE KWENYE UJENZI WA BANGOOOO

    ReplyDelete
  16. Tulivyopanda mlima Kili in 1987 usingepozi na T-shirt like that,ilikuwa ni full Makoti ya winter,kofia za soksi zinazofunika hadi pua,these guys look so casual,au ndio mambo ya Global Warming? where is the SNOW?

    ReplyDelete
  17. \lol... ama kweli mabadiliko ya tabia ya nchi 'climate change' inajidhihirisha mlimani.. maana theluji imepungua sana ..... jamani tuwahi kupanda kileleni kabla haijaisha kabisa ambao hatujapanda ...

    ReplyDelete
  18. Unapopiga picha huku umeshika bendera unahakikisha watakaoiona picha wanaona bendera kama vile kuna mlingoti upande wa kushoto ama sivyo bendera inaonekana imegeuzwa. TBL you should have done your homework!!!!!!

    ReplyDelete
  19. kweli barafu imepungua sana ... 98 nilipanda kilimanjaro haki ya nani hilo winter siajwahiona barafu ilikuwa nyingi sana nakumbuka saa sita usiku wakati tunaanza safari ya kuanza kupanda mlima snow likuwa inanguka... naona siku hizi baridi imepunua .. uhuru peak na tshirt duh!

    ReplyDelete
  20. kumbe baridi hakuna tena kileleni ndio maana hatukuweza kushinda maajabu mapya ya dunia tukabakia kulalamika bure ,picha inaonyesha wazi !

    ReplyDelete
  21. teh teh teh global warming - alafu mnataka kushinda tuzo la maajabu saba ya dunia.

    Yanga hoyeeeeeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  22. Hivi huo mlima unatoa bia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...