![]() | ||
Wapiganaji toka vyombo mbalimbali vya habari wakisubiri nje ya ukumbi wa White House wa makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo |
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakisubiri
kuanza kwa kikao cha leo.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo katika siku ya kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma imefanya uteuzi wa makatibu 10 wa CCM wa wilaya .
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye walioteuliwa kuwa ni Makatibu wa wilaya wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo: -
1. Ndg. Zainabu Mlawa,
2. Ndg. Paulo Mwita,
3. Ndg. Magdalena Ndwete,
4. Ndg. Ramadhani Sevingi,
5. Ndg. Odilia Maholelo,
6. Ndg. Omari Zuberi Mbwana
7. Ndg. Raymond Mangwala,
8. Ndg. Yahya Saleh Issa,
9. Ndg. Ame Omar Mkadam
10. Ndg. Langael Akyoo
Pia Kamati Kuu ya CCM imetengua uteuzi wa Makatibu watatu wa wilaya na kuwapangia kazi nyingine. Makatibu hao ni:-
1. Ndg. Zubeda Mbarouk aliyekuwa Kwimba
2. Ndg. Mussa Wenema aliyekuwa Kilindi
3. Ndg. Mkongea Ally Pira aliyekuwa Wilaya ya Magharibi.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa inafanyika tarehe 21 na 22/11/2011 na kufuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika tarehe 23 na 24/11/2011. Kikao hicho na vingine vinafanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Baada ya kumalizika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa tarehe 25 hadi 27/11/2011 kutafanyika Semina ya Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi wa ngazi ya Kitaifa hadi Wilaya. Katika semina hiyo watakaoshiriki ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Sekretarieti za Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (UWT, UVCCM na WAZAZI), Makatibu wa CCM wa Mikoa na Wilaya zote nchini.
ndugu ndugu imetokea wapi tena. mimi nina jamaa yangu hapo na hapendi kuitwa ndugu so and so. hayo yaliisha bwana.
ReplyDelete