Bro Michuzi naomba uniwekee hii kwenye blogu ya Jamii
Mini kwanza nampongeza Rais kwa kukubali kukutana na Chadema, huu ni ukomavu mkubwa wa kisiasa. Kwa yale yanayoendelea sasa katika madaliano yanayohusu katiba, ni wazi kila mtu anafikiri kuwa ni mbio za Chadema na CCM.
Nashukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametegua mtego huu. Hii itatusaidia sisi wananchi kufuta dhana hii ambayo imekuwa ikikuwa kwa kasi. Katika namna hiyo hiyo Chadema wameonyesha ukomavu mkubwa, mtu yeyote ambaye anafahamu mtindo ambao umekuwa ukitumika na Chadema kudai kusikilizwa, angefikiri kuwa maandamano yangekuwa namna ya pekee kwa chama hicho kudai kusikilizwa. Lakini Chadema walikaachini na kuamua kukutana na Rais.
Hata kama hawatakubaliana kwenye mambo mengi, lakini hakuna jambo zuri kama kusikiliza. Katika utumishi wa uma Rais lazima atakuwa na jopo la wataalamu na Chadema wameandaa timu ambayo ina wataalamu wengi wa sheria. Hivyo natarajia mambo makubwa yatakuja kutoka kwenye mkutano huu.
Baada ya kutoa pongezi kwa wanasiasa wetu, naomba nizungumzie kauli ya CCM iliyotolewa kupitia katibu muenezi Nape Mnauye. Hapa mimi nadhani chama kimekosa uelewa wa mambo mawili. Kwanza ni kwamba kuna tofauti kati ya uenyekiti wa chama na uRais.
Chadema wameomba kukutana na Rais na si Mwenyekiti wa CCM. Bila shaka Rais aliamua kukubali kukutana na Chadema bila ya kuomba ridhaa ya chama. Suala la pili ni kwamba Chadema wana jambo linawakereketa kweli kuhusu mchakato mzima wa kuelekea kupata katiba ambao wameona ni bora wakamualeza Rais kabla ya kufika mbali katika mchakato wa kupata katiba mpya.
Chadema wamejaribu kupenyeza wanachoamini ni sahihi bungeni lakini ikashindikana. Nafasi iliyobaki ni kukutana na Rais ambaye kwa sasa ana hatma ya mswada husika. Vyama vingine ambayo vina wawakilishi bungeni vilikaa kimya bungeni kuonyesha kwamba wameridhia utaratibu kama ulivyo, kwa maana hiyo hawana hoja wanayotaka kuwasilisha kwa Rais kwa sasa. Ndio maana wakaa kimya. Kwa hiyo kwa nini CCM inavilazimisha vyama vingine kukutana na Rais.
CCM, badala ya kutoa tamko, wangeweza kumshauri Rais ambaye pia ni mwenyekiti wake kuwa ingawa umekubali kukutana na Chadema, tunaona ni jambo jema pia kukutana na wawakilishi makundi mengine ambayo, kupitia majukwaa mbalimbali, yameonyesha kuwa yana hoja wanataka kuwasilisha.
Hii ingeweza kufanyika katika ngazi ya chama na wananchi tungepata taarifa kuwa Rais amekubali ushauri wa chama chake wa kukutana na makundi mengine.
Chondechonde jamani hata siasa zinahitaji weledi.
Mdau
we mdau bwana usipoteze muda wako utapata presha bure. haya mambo yanaingiliwa na udini, ushabiki wa kutotaka kuona mbali. watu si kwamba ukweli hawajui, wanajua lakini HAWATAKI. time will tell kila lenye mwanzo lina mwisho. we muda huu mwaka jana ulitegemea gadafi asingekuwepo?
ReplyDeleteAnonymous hapo juu mbona unatoa ushauri bila point. Mara udini, ushabiki nk, bila mifano halisi inayoingiliana na mada iliyopo.
ReplyDeleteMimi binafsi nimshukuru sana aliyetundika "Criticism" juu ya namna ambavyo rais angeweza kushauriwa kwa busara na chama chake, na kwamba hakutani na Chadema kama yeye mwenyekiti wa CCM, bali kwa kofia ya urais/ukuu wa nchi. Hapo lazima tuwe makini kutenganisha viwili, japo kuna wakati anazivaa kofia 2, lakini kwa hilo havai kofia 2 akikutana na Chadema.
NAMUUNGA MKONO MDAU MCHANGIAJI WA KWANZA KWAMBA INAWEZEKANA SANA UDINI UNATUMIKA SANA KUIBURUZA SIASA YA TZ YA SASA.
ReplyDeleteNDIO UKASIKIA MAPADRE WAKAINGILIA SANA MGOGORO WA UDIWANI ARUSHA.
NDIO UKASIKIA BAADHI YA WAUMINI WAKATENGWA NA KANISA KWA KISINGIZIO ETI WAMEMPIGIA KURA MGOMBEA ALIYELITUKANA KANISA.
NA HAYA MAMBO YAMEIBUKA ZAIDI BAADA YA UCHAGUZI WA MWISHO.
NCHI YETU INAKOKWENDA MUNGU NDIYE AJUAYE, LAKINI HATUTAACHA KUMWOMBA AWADHIBITI WANAOTUMIA ITIKADI ZA DINI KUTAKA KUPITISHA MAAZIMIO YAO.
TATIZO KUBWA HUKO NYUMBANI NI KUWA MENTALITY ZA BAADHI YA WATU, KWA SABABU HII AU ILE, HAZIJAPEA KIASI CHA KUWEZA KUCHAMBUA MBIVU NA MBICHI. HAPA UK NA HATA KWENGINEKO HUKU DUNIA YA KWANZA WATU WAKIONA SIASA ZAKO ZINA MWELEKEO MBOVU, KUTOKANA NA MENTALITY ZAO KUPEVUKA, MARA MOJA WANAACHANA NAWE. THAMANI YA MAISHA NA USALAMA WA WATU NI MUHIMU. SIASA ZAKO ZA NJAA NA KULAZIMISHA WATU WANAKUACHIA MWENYEWE.
HUU UJINGA WA BAADHI YA VYAMA UNAPOTEZA MALENGO YA NCHI. SISI TUMEACHA WAZEE NA NDUGU ZETU HUKO NYUMBANI, DHAMANA ZA USALAMA WAO ZIKO MIKONONI MWA VIONGOZI WA NCHI. KWA BAHATI MBAYA SERIKALI IMEKUWA SO LENIENT KIASI KWAMBA WAKOROFI WENGI, SPECIFICALLY KUTOKA CHAMA KIKUU CHA UPINZANI, WANA TAKE ADVANTAGE NA KUCHOCHEA KUVURUGA AMANI.
MPAKA LINI?
KAMA BUNGE LINA ZAIDI YA CHAMA KIMOJA, NA KAMA VYAMA VIWILI TU KATI YA VYOTE VIMEKUBALIANA NA TARATIBU ZA KUPATA KATIBA MPYA, SASA IWEJE TENA RAIS AKUBALIANE KUKUTANA NA HIKI KIMOJA TU? NDIO DEMOKRASI YA MTINDO GANI HIYO?
KWA NINI SERIKALI NZIMA, YENYE DOLA NYUMA YAKE, IKUBALI MASHINIKIZO?
KWANZA HICHO CHAMA CHENYEWE SI NDICHO KILICHOSEMA HAKIMTAMBUI RAIS? SASA KINATAKAJE TENA KIKAO NA MTU KILICHOKATAA KUMTAMBUA? NA KAMA UONGOZI MKUU WA NCHI UTAKOSA MSIMAMO KWA NAMNA KAMA HII, JAMAA HAO WATAPATA NGUVU NA WATAENDELEZA VURUGU ZAO. KILA KUKICHA MAANDAMANO. KILA KUKICHJA UVUNJAJI SHERIA.
IKIWA KINA MEMBE WAMEWEZA KUTOA KAULI KALI KALI DHIDI YA SHINIKIZO LA DAVID CAMERON ALIPOTAKA KULETA SIASA ZAKE ZA USHOGA, KWA NINI RAIS WA NCHI ASIWEZE KUTOA MSIMAMO DHIDIO YA CHAMA HIKI KOROFI NAMBA MOJA KWAMBA MCHAKATO WA KATIBA MPYA UTAFATA TARATIBU ZILIZOWEKWA?
MTU ASIYEKUHESHIMU VIPI ASTAHILI HESHIMA YAKO.
Mdau, Ukerewe
Umuhimu wa suala la katiba ni Raisi kukutana na vyama vyote na sio kimoja ili tathimini itoke kwa pamoja.
ReplyDeleteNapongeza Raisi kuwa na busara kuridhia kutaka kukutana na ''vyama vyote vya siasa''!
CCM upupu mtupu
ReplyDeleteNYIE CHADEMA NENDENI ZENU...ENDELEENI KUSUSA NA KUANDAMANA...UDINI UMEWAPONZA..NYINYI NI CHAMA CHA KANISA..MTAKE MSITAKE NDIVYO ILIVYO...HAMNA JIPYA.
ReplyDeletewewe mdau wa ukerewem hujui unalolisema unakurupuka tu,hujui nini maana ya kuvunja sheria, na hujui nchi yako kama kweli ni mtanzania ilikotoka na inakoelekea ndio maana unaongea tu bila kutafakari na kujia jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu kutokana na kutokuwa na serikari yetu kutokuwa makini na kuchukulia kila kitu ni siasa tu wakati watanzania hali zetu zinazidi kuwa ngumu.Mbona unashindwa kuongea utumiaji wa kodi zetu kimza mzaa mfano mzuri wa hivi karibuni wizari ya nishati na madini ( katibu mkuu wake) na boss wake kutaka kumsafisha unadhani katibu mkuu kiongozi aliamua mwenyewe kumsafiri katibu mkuu wa wizari hii, tafakari sio unaongea ongea tu, mambo mangapi yameibuliwa na wapinzani yenye masilahi kwa taifa. wewe mheshimiwa suara la katiba si kitu cha kuburuzwa watanzania wa leo sio wa zamani. KAMA NA WEWE UNATUMIWA NA UNAFAIDIKA NA MATUMIZI MABAYA YA KODI ZA WANANCHI SIKU ZAKO ZINAESABIKA!!! UTAKUMBUKA STATEMENT HII SIKU MOJA.
ReplyDeleteNyote. Rais ni kiongozi wa serikali ya ccm. Mengine yote ni semantics. Kama ccm imemshauri rais kuwa na vyama vingine kama vinattaka nao pia awasikilize shida iko wapi. Tatizo la chdm kukurupuka kiuanaharakati bila strategy. Sasa wamejiingiza wenyewe kwenye 18 ya ccm. Na bado. Wangemuuliza bwana wao cameron wafanyeje.
ReplyDeletewe mdau uliotoka kuchangia mada huna akili tena hujui unachosema. usione waarabu wanapingana na mawe huku wakijui wampigae anachombo cha moto (bunduki, bomo n.k)lakini hwajali kufa kwa ajili ya kutetea kile wanachotaka kwenye nchi yao hizo ni poropoganda zako na hao wenzako nnaojidanganya iko siku yatatimia tu watu wamechoka kuburuzwa buruzwa na hii serikali ilikuwa madarakani, mfano mdogo tu ni wamachinga au wafanyabiashara wa Mwanza na Mbeya walikuwa wako tayari kufa lakini kutetea maslahi yao wakaaamua kuutoa uhai wao kumbambana na askari kwa hali yoyote ile na namna yoyote ile iwe kwa fimbo, mawe, rungu kuchoma tairi hali hali wakijua wanaopambana nao wana silaha za moto. uwamuzi wa kuunda katiba ya haki ni wa wananchi sio CCM wala serikali, CHADEMA piganieni haki ya wananchi wenu vipi serikali inawafunga wananchi vitapambaa vyeusi machoni ili wasioni mbele wanakokwenda watapapasa tu mpaka watafika pale wanakotaka
ReplyDeleteMdau wa kwanza na wa tatu hamna point. Hamuoni mbali.
ReplyDeleteMdau wa ukerewe unaelekea kuhubiri Amani ila amani uitakayo wewe ni ya kujegwa na mtu mmoja tena kwa kauli ambayo mwishowe huishia vitendo amabavyo huelekea kuvunja hiyo amani.Amani huletwa kwa maelewano.
ReplyDeleteJamani mimi nimesema muda. Muda ukufika hakuna ujanja. Sasa hivi tubishaneeeeeeee. Viongozi wenye kupindisha mambo na wapindishe. Kiongozi yeyote mwenye akili ataona yatokeayo kaskazini mwa bara letu na hata mashariki ya kati. SIYO MIMI, ILA NI WAKATI HUO. Kufunga macho na masikio sio busara hata kidogo. Tusilete ushabiki kwenye haki za watu, wala ushabiki serikalini (ushabiki wa simba na Yanga) tulishaona hata wanaoleta ushabiki michezoni hatimae huingia matatani. Ushauri wangu kwa chama tawala- Acheni dhalau na tafutani haki na busara zaidi.
ReplyDelete