Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania, nchini Burundi, Dkt. James Mwasi, baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, kwenye Ukumbi wa Golf, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza (katikati) na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Jan Ping, wakisimama kwa heshima wakati ukipigwa wimbo maalum wa Afrikam baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga rasmi Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliliana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Jan Ping, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akiwa katika Ukumbi wa Golf, wakati akimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifunga rasmi Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni maziwa makuu au afrika mashariki. Bendera' nembo ni za east afrika-

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza hapo juu kwa mtazamo wangu, Maziwa Makuu Africa ni Victoria, Tanganyika na Nyasa...kitu ambacho tukiita East Africa nchi kama Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hazimo ila zipo ktk maziwa makuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...