MATOKEO ya uchaguzi wa udiwani wa kata ya Kijitonyama, Kinondoni jijini Dar es Salaam yaliyomtangaza mgombea Uloleulole Athumani wa CHADEMA kuwa ni mshindi, yamebatilishwa na Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu.
Uamuzi huo umetolea leo Mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Genvitus Dudu katika kesi ya kupinga matokeo hayo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo.
Dudu katika uamuzi wake alisema amesikiliza mashahidi wa pande zote mbili, mahakama imeona mdaiwa katika fomu ya
kugombea nafasi hiyo, aliandika jina la Uloleulole Juma Athumani wakati kwenye hati ya kisheria lipo jina la Juma Uloleulole Athumani.
Alisema mahakama hiyo imeona kwamba hao ni watu wawili, inakubaliana na Bulembo (mdai) kuwa kungekuwa na hati ya kiapo inayoonyesha mdaiwa alibadilisha jina lake.
Alisema kutokana na kukosekana na hati hiyo, inatosha kumvua mdaiwa nafasi aliyokuwa nayo na pia katika hati ya kisheria anayotakiwa kutia saini mbele ya hakimu, mdaiwa imeweza kuleta mashaka kwa kuwa ina tarehe mbili tofauti.
Alisema hati hiyo inaonesha mdaiwa alitia saini Agosti 14, mwaka 2010 na ya pili inaonesha hakimu alitia saini Agosti 18, mwaka 2010 mahakama inashindwa kuelewa kama kweli mdaiwa alitia saini mbele ya hakimu au la.
Aidha Hakimu huyo alisema wananchi wananyimwa haki yao kutokana na kutotimiza matakwa ya kisheria hawakuweza kujua vigezo vya mgombea kutokana na kwenda kinyume cha Sheria ya Uchaguzi mahakama hiyo inaona uchaguzi wa udiwani wa kata ni batili.
Kutokana na hayo, alisema maombi ya mdai yamefanikiwa kwamba matokeo ya uchaguzi yaliyomtangaza mdaiwa ni mshindi ni batili.
Hata hivyo alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kumtangaza Bulembo kuwa ni mshindi na kusema uchaguzi urudiwe kwani mamlaka hayo yapo kwenye mamlaka nyingine.
Bulembo alifungua kesi hiyo, akidai kutoridhishwa na matokeo hayo ya uchaguzi huku akiwa amewasilisha sababu sita. Katika sababu hizo aliiomba mahakama itamke matokeo batili, atangazwe yeye ndiyo diwani au kufanyike kwa uchaguzi wa
wazi na huru.
Hata hivyo mahakama ilisema pande zote mbili kama kuna ambaye hajaridhika na uamuzi huo anayo haki ya kukata rufani.
Kesi ya kumwondoa mpinzani imekwenda haraka haraka, kweli tunazo mahakama huru?
ReplyDeleteSikumaliza kusoma lakini hakimu Anachekesha sbb majina kinyume mbele lakini yote niyakwakwe na jambo hili Afrika nikawaida!lakini sishangai jamaa ni CHADEMA na mlalamikaji ni CCM mimi sina chama chchote lakini naona hakuna Demokrasi na haki bado tanzania!
ReplyDeleteHii ni kali. Basi wale tuliosoma chuo kikuu cha Dar es Salaam kipindi kile, sijui kama mpaka sasa utaratibu ni uleule, digrii zetu zitakuwa ni batili. Maana walikuwa wanaanza na Surname, tofauti na sekondari waliokuwa wakianza na Jina la kwanza.
ReplyDeleteMfano Ali Juma (akiwa sekondari), aliitwa JUMA Ali (akiwa chuo kikuu)
Bulembo hafai kabisa huyo ubabaishaji wake umeanzia mbali sana tokea huko musoma,fat na alipotaka uwenyekiti wazazi taifa akiwa nyuma ya mafisadi.Nguvu ya umma itaamua.
ReplyDeletembona hii imechelewa kuliko ile iliyomuangusha madabida wa ccm katika jimbo la kilwa dhidi ya mheshimiwa 'bwege' mbunge kwa tiketi ya cuf, acha ushabiki usio na maana... hatuubiri siasa hapa kama unataka yaho nenda kwenu jf
ReplyDeleteWewe Anon (nov 11, 04:38). Ulitaka iende polepole? Ili? Hebu acha hizo. Huo ni mwanzo tu. Tunasubiri Arusha Lema atakavyonyanganywa ubunge. Pambafu kabisa yule
ReplyDeletepole kwa wote waliopata usumbufu juu ya hukumu hiyo,ila naimba tume iitishe uchaguzi haraka kama hakuna rufani juu ya kesi hiyo ili amani isipotee
ReplyDelete