MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIONGOZWA NA VIONGOZI WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE WAKATI AKIELEKEA UKUMBI WA MKUTANO WA VIONGOZI NA WATAALAMU WA WANAOSHUGHULIKIA KUONDOSHA MIGOGORO BARANI AFRIKA ULIOFANYIKA HOTEL YA MELIA ILIOPO PWANI MCHANGANI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA.
 MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIFUNGUA MKUTANO WA TATU WA VIONGOZI NA WATAALAMU WANAOSHUHULIKIA KUONDOSHA MIGOGORO BARANI AFRIKA UNAO ENDELEA KATIKA HOTEL YA MELIA ILIOPO PWANI MCHANGANI ZANZIBAR.
  WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA TATU WA VIONGOZI NA WATAALAMU  WANAOSHUGHULIKIA KUONDOSHA MIGOGORO BARANI AFRIKA WAKIMSIKILIZA BALOZI SEIF ALI IDDI WAKATI AKIFUNGUA MKUTANO WAO. 
PICHA YA PAMOJA YA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA TATU WA VIONGOZI NA WA TAALAMU WANAOSHUGHULIKIA KUONDOSHA MIGOGORO BARANI AFRIKA MKUTANO HUU UMETAYARISHWA NA TAASISI YA MWALIMU NYERERE WAKISHIRIKIANA NA KITUO CHA HAKI ZA BINAADAMU CHA KIMATAIFA PAMOJA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA NORWAY.

Na Othman Khamis Ame.


Changa moto kubwa  inayolikabili Bara la Afrika Hivi sasa katika kuelekea kwenye Maendeleo zaidi ni kutumia mbinu na Marifa yaliyopelekea kupunguza migogoro ya Kijamii katika baadhi ya Mataifa ndani ya  Bara hili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Viongozi na Wataalamu wanaoshughulikia Kuondosha migogoro Barani Afrika unaofanyika huko  katika Hoteli ya Melia iliyopo Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Balozi Seif alisema Jamii ya Kimataifa imeshuhudia utatuzi wa Migogoro kadhaa Barani Afrika  hali ambayo kwa kiasi kikubwa imepunguza  Migogoro na hata Mauaji ya Raia wasio na hatia.

Aliwataka Viongozi na Wataalamu hao kutumia fursa nzuri iliyopo ya Amani iliyorejea Barani humu kwa kuweka Mipango bora  itakayoleta faraja zaidi ya ustawi wa Jamii katika miaka ijayo.

“ Tumeshuhudia utulivu wa Kisiasa ilivyorejea ndani ya Bara hili hasa katika Ukanda wa Maziwa Makuu eneo ambalo Sudan na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo { DRC } zilikuwa katika migogoro mikubwa ya Kisiasa  ”. Alikumbusha Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea  matumaini yake  kwamba Ripoti itakayotolewa na Viongozi  hao baada ya kumalizika Mkutano wao itawezesha kujenga mazingira bora ya kudumisha Amani Barani Afrika.

Balozi Seif amezipongeza Taasisi zilizoandaa  Mkutano huo ile ya Mwalimu Nyerere, Kituo cha Hali za Binaadamu cha  Kimataifa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Norway kwa uamuzi wao wa kufanya Mkutano huo Hapa Zanzibar na hasa ndani ya Jimbo lake ya Kitope.

Alisema uwamuzi wao huo haukuwa wa kubahatisha bali imekuja  kwa kuzingatia sifa ya Zanzibar ya amani iliyopelekea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa { GNU } kufuatia Mgogoro wa muda mrefu uliovihusisha Vyama vya CCM na CUF.

Balozi Seif aliwaeleza Washiriki wa Mkutano huo kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inafanya kazi zake vyema huku ikikabiliwa na changa moto kubwa ya kutekeleza matarajio ya Wananchi wote wa Zanzibar.

Akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Dr. Salim Ahmed Salim alisema yapo Maendeleo makubwa ya kupunguka kwa Migogoro Barani Afrika jambo ambalo limeleta faraja kwao akiitolea mfano nchi ya Sudan.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Haki za Binaadamu bwana David Harland ameipongeza Zanzibar kwa ukarimu wake unaopelekea kupokea Vikao na Mikutano Mzizito ya Kimataifa ndani na nje ya Bara la Afrika.

Wakati wa Mchana akiwa Mkoani Dodoma Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alikutana wa Uongozi wa Kampuni ya uwekezaji vitega uchumi inayojishughulisha na Mradi wa umeme unaotumia upepo na jua kutoka Nchini India.

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni hiyo ya Indomount bwana sudhakar amesema Taasisi yake imepanga kutumia  Jumla ya Dola za Kimarekani Bilioni Moja kati ya Bilioni saba zilizotengwa na waziri mkuu wa Nchi hiyo kusaidia Serikali na Taasisi Binafsi Barani Afrika.

Naye Balozi Seif ameuomba Uongozi wa Kampuni hiyo kuangali Meneo ambalo wanaweza kusaidia kati ya yale yaliyoainishwa na kupendekezwa na Zanzibar katika mipango yake ya Maendeleo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Bona naona wzungu wengi kuliko waaafrica au hawawezi tatuaa. Ndio mna maan msiamrushwe kweli kwa hali hii

    ReplyDelete
  2. Hehe...mbona mkutano wenyewe umejaa "wadhungu" hivyo...Matatizo ya afrika yatatatuliwa na waafrika wenyewe...au mambo ya utalii?

    David V

    ReplyDelete
  3. Kwani hamkujua kwamba tunaposhindwa kuishi kwa amani sisi wenyewe tunatoa fursa kwa miradi ya watu wengine? Ulizia gharama za warsha hiyo na uone vipi fedha hizo zingepelekwa kwenye maendeleo tija kiasi gani tunaikosa!! Wajinga ndo waliwao! Endeleeni kumwaga damu wengine wafaidi!

    ReplyDelete
  4. Watu wamewachoka na hawa wazungu lakini sijui kwa nini viongozi wameweka maslahi yao mbele kiliko amani,hamna hata kesi moja waafrika wataaamua na ikubalike na wazungu ila kama ina maslahi yao,hapo zaidi watazungumzia ubaguzi tu nani bora nani hafai na wapo hapo kwa ajili ya kuangalia nani anatoa points za kiuhakika na yupi si mbaguzi ambayo kwao wao wamuwekee vikao vya close doors na kumjadili vipi wamtengeneze, mambo mengine si ya kuwashirikisha kabisa hawa jamaa, mambo mangapi ya maana na yanayohusu Afrika wao wanayafanya bila kutushirikisha, na hata wakitushirikisha wanayazibia nta masikio maoni yetu mengi.WE HAVE TO WAKE UP AND TAKE OUR OWN DECISION AND RESPONSIBILITY,OTHERWISE KEEP ON DESTROYING AND FIGHTS EACH OTHER.

    ReplyDelete
  5. It's true Wajinga ndiyo waliwao kama alivyosema mdau. The continent of the dead leaders. Nchi za nje zinapotaka kuingilia mambo ya Africa zinapendakeza washa au kamkutano furani ka-kijinga. Kwa uchovu wa kutotaka kufikiri na tamaa ya sisi watu weusi basi tunakubali bila kufikiri kwa kuwa tunapenda vya bure, kama: kusafiri, posho na ikiwa kama njia moja wapo ya kupumzika nk. Tatizo ni la bara la Afrika lakini utaona weupe ni wengi na wameshika madaftari wanaandika kila mweusi atakalolisema hapo, wakirudi makwao wanakwenda kutafari, nani kasema nini. Mwenye kuonyesha msimamo watamfanya rafiki yao wa ulongo, maana wao kwa hulka yao hawana rafiki. Ukiwa rafiki yao leo kesho lazima wakumalize! Hilo lazima wote tulifahamu. Tukirudi kwenye mkutano huo weusi wote ni wasikilizaji hata wakipendekeza jambo ni bule tu maana hawakuchangia senti yeyote kwenye garama ya kikao hicho. Weupe welevu kama nyoka, yamkini wanajuwa wameshamtoa roho aliyekuwa mchangiaji mkuu wa vikao vya kiafrika, na waliobaki wote ni ombaomba au Yes Sir. Kwa hiyo wanafanya vituvyao.
    Lakini siku itafika, maana hawatatutoa roho wote.
    AFRIKA NI MOJA NA WAAFRIKA WOTE NI NDUGU ZANGU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...