MWAKILISHI WA BARA LA AFRIKA,UMOJA WA MATAIFA,BALOZI AMINA SALUM ALI (KULIA) AKIUKARIBISHA UJUMBE WA ZANZIBAR UNAOONGOZWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, BALOZI SEIF ALI IDDI (WA PILI KULIA) ULIPO MTEMBELEA OFISINI KWAKE ILIYOPO KATIKATI YA JIJI LA WASHIGTON DC,MAREKANI.
MWAKILISHI WA BARA LA AFRIKA,UMOJA WA MATAIFA,BALOZI AMINA SALUM ALI AKIZUNGUMZA NA UJUMBE WA ZANZIBAR UNAOONGOZWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR,BALOZI SEIF ALI IDDI ULIPO MTEMBELEA OFISINI KWAKE ILIYOPO KATIKATI YA JIJI LA WASHIGTON DC.

Na Othman Khamis Ame - OMPRZ

Mwakilishi wa Bara la Afrika katika Umoja wa Mataifa Balozi Amina Salim Ali amewataka Watanzania kulitumia vyema soko la Marekani katika kukuza uchumi wa Taifa.

Balozi Amina alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Ujumbe wake ulipomtembelea Ofisini kwake Mjini Washington DC Nchini Marekani.

Amesema Marekani kupitia mashirika na makampuni kadhaa ya Nchi hiyo hivi sasa yameelekeza nguvu katika kuwekeza Vitega Uchumi kwenye Mataifa kadhaa Ulimwenguni.

“ Hakikisheni Watanzania mnachangamkia vyema fursa hizo ambazo wenzetu wa Nigeria, Ethiopia na hata Majirani zetu wa Kenya wanazitumia ”.Alisema Balozi Seif.

Balozi Amina ameziasa taasisi zinazosimamia uwekezaji kuwa makini na wawekezaji wanaoonyesha hamu ya kutaka kuwekeza.

Amesema si vyema kwa wawekezaji hao kuhangaishwa wakati wanapotaka kuwekeza vitega uchumi vyao Nchini.

Balozi Amina ameupongeza Ujumbe huo wa Zanzibar unaofanya ziara Nchini Marekani kwa hatua yake ya kuitangaza Zanzibar kwa wawekezaji wa Marekani kufungua milango ya uwekezaji Zanzibar.

Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi alimshukuru Balozi Amina kwa kuwa kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya Zanzibar na Wawekezaji wa Marekani.

Balozi Seif alisema Mwakilishi huyo wa Bara la Afrika katika Umoja wa Mataifa amechangia kuifanya ziara hiyo kuwa ya mafanikio kwa kiwango kikubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. michuzi vp bei ya madafu mbona kimya sana?
    ikiwezekana tuwekee japo kila baada ya siku 2 ili tujuwe mabadiliko ya madafu

    MAOMBI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...