Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi (kulia ) akiwa na Mchungaji, Dk. Bill Hybels ( kushoto ) wakimsikiliza Mratibu wa mkutano wa mafunzo ya Kuinua Uchumi, Ustawi wa Jamii na Uongozi Bora, mchungaji ,Peter Mitimingi uliofanyika leo kwenye hoteli ya Blue Pearl – Ubungo Plaza jijini Dares Salaam. Naibu Waziri huyo alifungua mkutno huo kwa niaba ya Makamu wa Rais,Dk Mohamed Gharib Bilal, ambapo alisisitiza kuwa suala la kuendeleza nchi linategemea juhudi za pamoja kutoka kwa watu mbalimbali na mashirika na kuongeza kuwa serikali itayafanyia kazi mapendekezo yatakayotokana na mkutano huo. Wakati huohuo Dk. Hybels alisema ili kuweza kuondoa umasikini ni lazima kila mwananchi apate kibali halisi cha kumiliki ardhi ikiwemo kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwapatia elimu . Picha na Magreth Kinabo – Maelezo.
Home
Unlabelled
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje afungua mkutano wa mafunzo ya Kuinua Uchumi,ubungo plaza leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...