Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe akiwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenda kwa Mtukufu Sultan Qaboos wa Oman kwa Mhe. Yousef Alawi Bin Abdallah Waziri Anayeshughulikia Mambo ya Nje wa Oman mjini Muscat leo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe akiwa katika mazungumzo na Waziri Anayeshughulikia Mambo ya Nje wa Oman,Mhe. Yousef Alawi Bin Abdallah mjini Muscat leo.Picha na Assah Mwambene

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Mtukufu?Astaghfirullah..

    ReplyDelete
  2. Huyu michuzi ni muislamu kisha anajifanya hayawani kumwita binaadamu mtukufu

    ReplyDelete
  3. JK nakuaminia baba, najua huo ni mzinga tu wala usibishe.
    Uzuri wa huyo Sultan Qaboos misaada yake huwa anaituma kwa majina ya watu na sio kupitia wizara hivyo usifanye makosa baba.

    Thamim, safarini Magomeni Makuti nikitokea Chalinze

    ReplyDelete
  4. Tunapokwenda ni mbali tuache masihara na sifa ni kufuru kubwa mbele ya Mola binaadamu anayekwenda haja tunamwita mtukufu kwa lipi? na kwanini? iweje? kuna kufa na tukishakufa ndio tutakutana na MTUKUFU wa kweli tuache ukauzu binaadamu tusiitane watukufu.

    ReplyDelete
  5. Muogopeni Mwenyezi mungu jamani, kwanini aitwe Mtukufu? Huyu ni mwanadamu kama nyinyi jamani?

    ReplyDelete
  6. haya mambo mengine duh,tuwaachie wenyewe

    ReplyDelete
  7. Dah! "mtukufu sultan....." Kah! yaleyale ya mtukufu Rais.....This is too much.

    ReplyDelete
  8. mtukufu manake nn?,mtukufu ni mungu peke yake,huo ni upuuzi wa hali ya juu wa kibinaadamu,labda utukufu wa hapa duniani lol,nawakilisha

    ReplyDelete
  9. JAMANI HUYO GABUS NI MTU TU KAMA SISI HAWEZI KUA MTUKUFU NI KING TU LKN SIO MTUKUFU MTUKUFU NI MWENYEZI MUNGU PEKE YAKE HAKUZAA WALA HAKUZALIWA WALA HANA ANAEFANANA NAE HATA MMOJA

    ReplyDelete
  10. umasikini ndo unatufanya tukubali utukufu wake au?

    ama kweli umasikini ni mbaya kuliko jehanamu.

    ReplyDelete
  11. Nadhani yeye mwenyewe Qabus akisikia kama watu wanamwita mtukufu hatofurahika kwakuwa uisilamu unamtukuza mwenyezi mungu na sio binaadamu.

    ReplyDelete
  12. hahaha haya ndo matokeo ya kuipenda sanaa dunia.. mpaka watu kama sisi wanaitwa " watukufu". uncle MUOGOPE ALLAH IPO SIKU TUTASIMAMA MBELE YAKE KUJIBU HAYA YOTEEE¬

    ReplyDelete
  13. Kwa kweli hata mimi naona huo ni mzinga kenda pigwa huyo Sultani.Mhe Membe ungeenda na Twiga...maradhi yote ugua lakini usiombee kuchacha...

    ReplyDelete
  14. mambo ya kumwita binadamu mwenzako mtukufu yalikataliwa na raisi wa awamu ya pili

    raisi mstaafu ali hassan mwinyi ndio raisi aliewahi kukataa kuitwa mtukufu na kusema kuwa aitwe mheshimiwa raisi inatosha na sio mtukufu kwa maana yeye hakuwa mtukufu.

    ReplyDelete
  15. Kwani hamujui kwamba hata yale Mapinduzi ya Januari 12, 1964 kule Zanzibar huitwa Mapinduzi Matukufu.

    ReplyDelete
  16. MTUKUFU NI MUNGU TUU!! wee michu una tabia ya kubebabeba watu sana sijui una tatizo gani... mara dakta bla blaaa kwani si umtaje mtu kwa ubiniwake mpaka uweke naskshi nakshi utadhani umekuja mjini juzi, grow up!!!

    ReplyDelete
  17. UPEO NI KITU MUHIMU SANA NA ELIMU WALA SISHANGAI KWA WATANZANIA HATA NYERERE NI MTAKATIFU PIA NI CHA AJABU.?

    ReplyDelete
  18. acheni upuuzi, mnadiscuss utukufu wa nn? Mmejaa madhambi kibao..! Wao huko wanajiita watukufu na ndio maana wanawataja kwa vyeo vyao huko sio kwamba membe anajitajia tu. Mahopeless nyie

    ReplyDelete
  19. Haya wadau chagueni. Mnataka daraja pale kigamboni, sio? Mtoni kwa mama na kwa Kichaka watatusaidia tukikubali masharti ya kutoa makal**. Mtukufu atatusaidia kwa kumuita Mtukufu tu. Chagueni, hatutaki basi tuendelee kuogelea. Michuzi munamuhukumu bure, ni mjumbe tu, hana makosa.

    W. Mwisho

    ReplyDelete
  20. Njaa mbaya...haya sasa msaada wa Mwingereza kupitia Donald Cameron makubwa tumeyaona ,na huu msaada wa Mwarabu ndio haya...lakini gharama yake ni kubwa, hiyo ni lugha ya bora mkono uende kinywani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...