Mhe. John Cheyo Mwenyekiti wa Kamati ya hesabu za Umma, na Mbunge wa Bariadi Mashariki akisisitiza jambo wakati alipokuwa akichangia majadiliano kuhusu uwazi, uwajibikaji na udhibiti wa fedha za umma.mada iliyojadiliwa katika siku ya pili na ya mwisho ya mkutano wa siku mbili uliowakutanisha wawakilishi wa mabunge kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. kulia kwake ni Mhe. Betty Machangu Mbunge wa Viti Maalum CCM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Tutajipangaje kuimarisha mapato wakati pesa zikipatikana mnazipeleka kwenye mifuko yenu?

    ReplyDelete
  2. SAFI SANA CHEYO,UMELIONA HILO MAPEMA..NI WAKATI WA AFRICA KUAMKA,NI KWELI WAZUNGU WAMECHACHA ILE MBAYA SASA HIVI.

    ReplyDelete
  3. Hata kama tutaimarisha uchumi wa ndani bado watakaonufaika ni akina Mapesa na wenzake tu. Angalia sasa hivi wamejipandishia posho hadi 200,000 kwa siku. Mkulima yeye posho yake iko wapi?

    ReplyDelete
  4. Mtajipangaje wakati ndo kwanza mmeongezeana posho????? Au una maana wakujipanga ni kina sie walala hoi???

    ReplyDelete
  5. Mzungu anakusaidia wakati anataka kitu kwako, kama madini ameshachukua au ameshaweka mkataba na wewe kwa miaka 50, kwa kukubembeleza na vimisaada hapo mwanzo.. aendelee kukusaidia kwa lipi tena?! Ngoja wagundue tuna kitu kingine kama mafuta uone watakavyomwaga misaada siku za mwanzo. Mzungu hajaishiwa Ndugu zanguni.

    ReplyDelete
  6. Asante Mh. Cheyo. Hili umeliona mapema kama mdau alivyosema hapo juu. Harafu wewe huwa kuwakopeshi, unawapa papo kwa papo. Lakini tatizo la viongozi wa Africa hamna umoja wala maelewano, sijui sisi watu weusi vichwa vyetu vina matatizo gani. Lini tutaamuka? Ni kweli mizuka inaona mbali sana yenyewe sasa hivi inaona mambo ya miaka hamsini au mia ijayo kwa hiyo haiwezi kutoa misaada ya kumwaga kwa kuwa uchumi wao nao umekuwa kile sisi nyumbani tunaita MASHI GA MBITI.
    Cheki ukweli wa anony wa Wed. Nov. 30, 03:08:00PM 2011. Asante anony.

    Kichaka alipochukuwa madaraka tu, katamka mwenyewe "Africa is not our priority" Sasa hivi anazungukia kama pia!!! Ni wale wale, athibitiwe.

    Mdau Mwenye nchi.

    ReplyDelete
  7. Nani ka kwambia mzungu kaishiwa, wanyama, madini tumeshawapa bado sasa wanafukuzia uranium wakishapata tu teke la nguvu. JK cheka nao tu sasa wakishapata chao utasoma namba ushangae.

    ReplyDelete
  8. Kujipanga kunataka tuwajibishane, wale MAFISADI walioiba na ushahidi upo wafilisiwe, warudishe na walipe fidia, sio watu walipishwe kodi kali na TRA halafu hakuna kuhoji, makusanyo yaende mifukoni mwa watu wachache!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...