Wakulima wa zao la Karafuu Kisiwani Pemba wametakiwa kuhakikisha kuwa Karafuu zao ambazo wanazipeleka kwa Mauzo katika vituo vya Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) ziwe zimekauka vizuri ili kuondoa migongano isio na lazima  katika vituo vya ununuzi wa Karafuu.
 
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kituo cha Ununuzi wa Karafuu katika kituo cha Finya kiliopo Mkoa wa Kaskazini Pemba   Mussa Omar wakati alipokuwa  akiwaelezea wajumbe wa kamati ya Kitaifa ya kusimamia zao la Karafuu Zanzibar w walipokitembelea kituo hicho .
 
Amesema kuwa kipindi hichi ni cha Mvua ambayo inaonekana ni kubwa hivyo ni lazima  kwa Wakulima wa zao hilo kuhakikisha kuwa Karafuu zao wana zimekauka vizuri ili kuondoa kadhia ya wao  kuombwa kuzianika tena ili ziwe zimekauka vizuri. 
 
Aidha Mussa amewaomba Wakulima kuzisafisha vizuri Karafuu zao na baadhi yao kuacha tabia yakuchanganya Karafuu na Makonyo na vitu vyegine ambavyo havipaswi kuwamo katika magunia yao ya Karafuu kwakudhania kuwa watapata faida kubwa.
 
Akizungumzia juu ya masuala ya Upatikani wa Karafuu hivi sasa amesema kuwa wao wananunuwa Karafuu lakini si katika kiwango cha awali ,hii inatokana na Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa na kusababisha kwa baadhi ya sehemu kutochumwa  Karafuu hizo na pia  kutowezekana kuanikwa Karafuu hizo kwa kuwa jua linakuwa halipo.
 
Mussa ambae ni msimamizi wa Kituo hicho cha Karafuu cha Finya amesema kuwa yeye anaamini sana kuwa mara mvua zitakapomalizika  najua kutoka Karafuu nyingi zitaweza kuuzwa katika vituo kwani hivi sasa sehemu kubwa Karafuu hizo zinaanza kuchomoza na nyengine kupeya.
 
Mkuu wa kituo hicho ametowa wito kwa Wakulima wa Zao la Karafuu ambao hupeka kuuzwa katika Vituo vya ZSTC kuwasaidia Wachukuzi na wa Krafuu kuwapa haki yao ya fedha mara tu wanapouza Karafuu zao kwani Wachukuzi hao hawalipwi na Shirika la ZSTC  kwa hivyo ni wajibu wao kuwalipa na kuacha tabia ya kutowalipa.
 
Wajumbwa wa kamati hito yakitaifa ya Kusimamia zao la Karafuu Zanzibar iliokuwa ikiongzwa na Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Ali Abdulla Malimusi walitembelea Vituo vya ununuzi wa Karafuu vya Junguni, Finya na Kinyikani.
 
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
19/11/2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...