Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Mkoani Kagera, Asumpta Mshama akielezea mikakati ya wenyeji wa Wilaya ya Misenyi wanayoifanya kuboresha masuala ya Elimu, Afya na Uchumi kwa ujumla wilayani humo. Alikuwa anazungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wakazi wa Dar es Salaam wenyeji wa wilaya hiyo, kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Misenyi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Mwenyekiti wa Mfuko huo,Profesa Wenceslaus Kilama.
Baadhi ya wakazi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Picolo, Msasani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Wilaya ya Misenyi,Profesa Wenceslaus Kilama akitoa maneno ya ufunguzi wa mkutano wa wana Misenyi wa kujadili maendeleo ya wilaya hiyo.
WanaMisenyi wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo
Viongozi wa Mfuko huo, wakiingia kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali mstaafu Issa Njiku, Mbunge wa Nkenge, Asumpta Mshama, Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo, Godfrey Kamukaya na Mwenyekiti wa Mfuko huo, Profesa Wenceslaus Kilama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongera sana wote kwa kusoma alama za nyakati ,Na Kwa Misenye mabadiliko yanaweza kuwepo kwa nia mlianzisha . Kwa Historia ya Bukoba ,Mabadiloko uanzia Misenye na Kiziba ,Na sasa ni mda wa mabadiliko Ahsanteni sana wote hasa Mbunge ongeza Nguvu sana upo nyuma ya mda !Ahsanteni wote !

    ReplyDelete
  2. Misenyi oyeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!, tuko pamoja kwakweli tunataka ule moto wa elimu na maendeleao urudi.Hongera mbunge wetu mama Mshama na viongozi wote wa mfuko wa maendeleo.Tuko pamoja.Umoja ni nguvu.Pamoja tunaweza

    ReplyDelete
  3. Misenyi oyeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!, tuko pamoja kwakweli tunataka ule moto wa elimu na maendeleao urudi.Hongera mbunge wetu mama Mshama na viongozi wote wa mfuko wa maendeleo.Tuko pamoja.Umoja ni nguvu.Pamoja tunaweza

    ReplyDelete
  4. Swali la kizushi....hapa naona kila kwenye meza kuna bonge la chupa la ulevi sasa ndio kuna dalili ya kujadili maendeleo hapo au kuharibu maendeleo?

    ReplyDelete
  5. Nawee watoa mmeno isenyi oyeeeee wenzioo waala zile zilizokusanywaa ajili ya maendeleo

    ReplyDelete
  6. Hongera Mh. Asumpta. Hujabadilika, uko vile vile toka enzi za Rugambwa Girls!!

    ReplyDelete
  7. Bantanuka David Hongera Haji Said Seruu Kwa vyovyote unavyo tenda hapa board Mtukula Asanteni sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...