Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akizungumza na waandishi wa habari, Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam leo, kuhusu ushindi wa hukumu ya rufani ya kiwanja cha Oysterbay jijini Dar kilichokuwa kikimilikiwa na Kampuni ya Kahama Gold Mining, iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa jijini . Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Patrick Rutabanzibwa.Picha na Kamanda Mwaikenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ikiwa hawa watu wameuziwa kiwanja na halmashauri yakinondoni vipi mnawadhulumu?Halmashauri ni nini?si serikali?kwakweli hii nchi dhulma tu!sasa hawa watu wakadai wapi pesa zao?serikali imejaa matapel ndio maana watu wengi wanadhulumika!mimi mwenyewe niliuziwa kiwanja na diwani na wizara ya Ardhi ilikuwa inaniletea kila mwaka malipo yakiwanja halafu baadaye wanakuja kuniambia kiwanja sio changu!kwakweli nchi itakwenda pabaya kwa dhulma!!

    ReplyDelete
  2. Anon wa kwanza, Uliuziwa kiwanja na Diwani wa wizara ya Ardhi!? Mwe! Kweli tatizo ni Watanzania wenyewe, Serikali inaonewa!!

    ReplyDelete
  3. Shida ni kuwa Watanzania tumezoea Rushwa. Huyu nampongeza. Lomesha kabisa rushwa ili wajifunze!

    ReplyDelete
  4. Naomba nieleweshwe, ni nani mwenye mamlaka ya kuuza kiwanja Bongo? (Nadhani tunaongelea viwanja vile vya mjini, sawa!?) Kusema kweli sijui nataka nifundishwe.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana wizara, ila sio ndio kiende kwa mwingine, tunafuatilia kwa umakini na ukaribu sana.

    Mpiganaji.

    ReplyDelete
  6. Matatizo mengine watu hujitakia hasa wakiwa na pesa.Hawa matajiri wakati mwingine hulazimisha kununua kiwanja hata kama hakiuzwi kwa mujibu wa sheria.Kuna matajiri wengi wameuziwa sehemu za wazi mpaka unakuta hakuna sehemu za wazi za watu kujipumzisha au watoto kucheza japo mpira.Maisha yanabadilika na watadaiwa mmoja mmoja mpaka kieleweke.

    ReplyDelete
  7. Mwenye mamlaka ya kutoa viwanja inategemea na sehemu. Mfano Dodoma kuna CDA. Kwingine wahusika wakuu ni Halmashauri na wizara ya Ardhi. Sema kunatakuwa na maslahi ya watu ndio maana kunatokea mizozo kama hii.

    Watu wengekuwa wahadilifu isingetokea kipindi kiwanja kimoja wamili 5. Tanzania ni kama mgonjwa amepelekwa hospitali hajitambui na ana maradhi mengi yana msumbua kiasi kwamba dokta anashindwa aanze lipi wakati huo huo hali inazidi kuwa mbaya. MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  8. Anon wa Tue Nov 22, 10:01:00 PM 2011, inavosemekana na nadhani kisheria , "ARDHI" ni mali ya serikali (hapa kidogo hata mie napaona pachungu kwangu" kwa hiyo kama unataka kununua ardhi ni lazima kwanza umuone huyo "ALIEMILIKISHWA" kwa muda maana alie lease, lakini kabla ya kununua inakubidi uende ardhi kwanza tafuta watu wa ardhi wakuletee kile kipimo chao nimesahau jina lake waangalie eneo hilo unalotaka kununua limeangukia katika sehemu ya mradi? au sehemu ya makazi ya watu? au eneo la biashara? au viawanda ? au sehemu ya kutumia kwa ajili ya kutumikia jamii yaani Hospital, MIskiti, makanisa na huduma zozote za jamii, then ndio unaweza kununua , lakini hata hivo NAKUSHAURI ! ni bora ununue viwanja vilivopimwa na serikali maana siku hizi serikali kila sehemu inaweka mradi! mimi yamenikuta! nilinunua eneo Zinga Bwagamoyo na hapo niliambiwa kuwa kuna makazi ya watu ! baada ya muda serikali ikasema kuna mradi wa EPZ, na katika bunge lililopita muswada umepitishwa wa ardhi, tukiuliza fedha zetu za kulipwa tunaambiwa hakuna pesa tusubiri na siku zinaenda ! cha ajabu huo mwaka tutakaokuja kulipwa hata ukitaka kununua sehemu mbadala hizo zilizopiwa na serikali thamani ya shillingi itakuwa imeshashuka kwa kuwa wametathmini kwa shillingi ya mwaka 2010 TUTAFIKA, Haya, kama hayo hayatoshi, nimenunua kigamboni nikasema nijenga kibanda changu! na inaonseha kabisa makazi ya watu ! serikali imepiga hodi kuna mradi na nadhani itakuwa umeusikia ambao umewafanya watu mpaka leo hawaendelezi maeneno yao wanasubiri tamko la serikali ambalo nadhani mpaka yesu arudi ndio tutapewa jibu! sasa kwa kukushauri ni bora kama una pesa ndugu yangu tafuta kiwanja kilichopimwa cha serikali! au sivyo utaishia KULIA KAMA MIMI HAPA! MOLA ATUSAIDIE NA NINA HAKIKA NA KUWA NA IMANI THABITI KUWA HAKI YA MTU HAIENDI BURE! na nina imani pia yeyote anaetaka kuja kutudhulumu basi ATADHULUMIWA YEYE NA MWENYE EZ MUNGU KABLA HAJATUFIKIA SISI!

    ReplyDelete
  9. Diwani nae anahusika vipi katika uuzaji wa viwanja? Anon wa kwanza naomba ufafanuzi..

    ReplyDelete
  10. Fuata taratibu sahihi siyo uuziwe kwa kujuana halafu baadae watu wanapofuata sheria useme umetapeliwa. Tena hawa wanaojiita wawekezaji ndiyo usiseme wanalobi si kitoto. Wao ndiyo waliodhulumu kwa kununua kiwanja mali ya umma na kumlipa mtu binafsi akajiendeleze yeye! Ndiyo wakome sasa kwani kuna mtu anayefuatilia sheria sasa yuko incharge.

    ReplyDelete
  11. Anonymous wa pili niliuziwa na kiwanja na Diwani alisema kiwanja nichake na kutengeneza offer fecky na offer iliandikwa na ofisa wa Ardhi aitwaye mwajabu anaefanya kazi wizara Ardhi magomeni na mkuu wake mama kesy alitia saini na nilipelekwa mpaka makao makuu kuonyesha Ramani kuu na baada ya hapo nikawa ninaletewa kila mwaka nilipie kiwanja sijui kama utanielewa lakini ukitaka kunielewa utanielewa sbb nafikiri point nikwamba serikali ndio inafanya makosa kuweka matapeli na wezi kwenye wizara zao!Nani asie juwa kama Hashim mbonde aliekuwa Diwani wa mbweni alikuwa ndio tapeli wakwanza wakuuza viwanja na halifu akaenda kuwekwa yeye ndio muamuzi wa migogoro ya viwanja?

    ReplyDelete
  12. Anonymous wa pili umeuliza swali kwa Anonymous wa kwanza lakipumbavu kabisa!!Wizara ya Ardhi iko na Diwani?Kweli mwe!!(Iringa mbali na Dar)!!

    ReplyDelete
  13. Annon 10:01:00 PM 2011, mwenye mamlaka ya kuuza viwanja mjini ni halmashauri za wilaya za miji husika mfano ukiwa Mwanza ni Halmashauri ya jiji la Mwanza na Ukiwa Kigoma ni Halmashauri ya manispaa ya kigoma hivyohivyo kwa mikoa mingine. Kwa Dar es salaam kimsingi wanaotakiwa kuuza viwanja ni halmashauri za Ilala, Kinondoni na Temeke ila kwa Dar kwa kuwa wizara ya ardhi ipo hapohapo ikajiingiza kwenye kazi hiyo japokuwa wao walitakiwa wawe wanasimamia shughuli zote zihusianazo na ardhi, kwa kuwa wamezoea kuuza viwanja kama wizara sasa kuachia halmashauri zifanye kazi inakuwa ngumu kwa watakula wapi. Tatizo hikli lipo pia Dodoma ambapo kuna CDA na Halmashauri ya manispaa ya Dodoma nazo zinagongana

    ReplyDelete
  14. Anonymous wa 10:08 nimeshatowa jibu na pia ujue mtu yeyote anaweza kuuza kiwanja akisema nichake!ndio maana yuko mtowa maoni mwenzangu hapo amesema wilaya ya ilala imejipa kazi ya uuzaji viwanja sbb ya ulaji!point nikwamba serikali haina system imewapa ulaji watu wengi kutokana system yao fecky!

    ReplyDelete
  15. Katika swala la viwanja ni wafanyakazi wa ardhi wanaongoza kwa utapeli wakishirikiana na matapeli wa dar. Sasa serikali ni nani kama siyo hao wafanyakazi wa ardhi. MAMA TIBAIJUKA UNGEFUKUZA WAFANYAKAZI WOTE WA ARDHI NA KUAJIRI WAPYA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...