Habari za mchana Uncle Michuzi.

Nataka kuwataarifu wanablog ya jamii wenzangu wote kuwa kuna gari linatumika na wezi wa vitu kwenye magari katika sehemu nyingi hapa mjini Dar na jana usiku mida ya saa mbili nilikoswa koswa nikiwa maeneo ya Savei madukani karibu na chuo kikuu. 

Hawa jamaa wanatumia gari aina ya Toyota Mark II (GX100) nyeupe lina namba za usajili T431AWU. Walikuwa tayari wanataka kuvunja kioo kidogo cha mlango wa nyuma ili washughulike. Tafadhali mtu yeyote anayeweza kutoa msaada asaidie ili kukomesha tabia hii mbaya.

Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Kama unayo number ya gari kwanini usiripoti Polisi ili kama watafanya tukio lolote itakuwa ni rahisi kuwakamata.

    ReplyDelete
  2. nathani TRA wanaweza retrieve hii namba kwenye system zao nakuangalia imesajiriwa kwa nani na kama ina match na description za hiyo gari nakumaliza huu utata wanakera sana

    ReplyDelete
  3. Ulitoa taarifa kituo cha polisi?

    ReplyDelete
  4. Polisi wanashikiriana na wezi na mahambazi kwenye uhalifu. Hata ukitoa taarifa ni kazi bure. Ndio maana wananchi wakati mwingine wanajichukulia sheria mkononi.

    Inasikitisha sana!

    ReplyDelete
  5. Wakati mwingi watu wanshindwa kutoa taarifa Polisi kwa sabau ya usumbufu walionao polisi wetu.Unajua polisi wetu wengi ni form four failure,walikuwa hawatilii manani elimu shuleni wakati walijua umhimu wa elimu.Tabia hiyo pia iko vituo karibia vyote ya Polisi,ukienda kuripoti tatizo na wewe wanakuchukulia kama mharifu vile.Ndiyo maana mtu akishaseerve kuibiwa anauchuna na mwingine hata akishaibiwa na wezi kutokomea pia anauchuna tu.Mungu atusaidie-kul;iko kwenda polisi bora ukapigia simu rafiki zako au kuanza kuliwinda gari hilo kwa namna unazojua na kutoa kipigo cha mwaka kwa wezi,ukiwezekana uaa kabisa-Wananchi wenye hasira hawafungwi wala kushitakiwa na hasa kama kosa liko wazi.

    ReplyDelete
  6. Hao jamaa wenye hiyo gari T431 AWU inabidi washughulikiwe haraka, huu sio muda wa mzaha tena.

    Kutokana na Police Post zilivyo na rushwa ukiripoti suala hili halitiliwi uzito kwa kuwa pale wanataka matukio ambayo ni direct yenye mdai na mdaiwa ili wale kote kote ndio zao.

    Mimi nimeshatuma e-mail polisi kutoa taarifa ya uhalifu kwa kuwa sasa Idara ya Polisi inafikika ki teknolojia ina tovuti www.policeforce.go.tz

    ReplyDelete
  7. Kuna gari nyingine corolla nyeupe number T746ABT inafanya uhalifu maeneo ya Oysterbay na Mikocheni.Report iko Polisi lakini hakuna kinachofanyika.

    ReplyDelete
  8. Jamani Tanzania sio msitu wa wahalifu kwa haraka hizi gari mbili T431 AWU na T746 ABT zishughulikiwe ili iwe mfano...wenzao Mbeya wanajituma kwa Umachinga lakini wanatumiwa Polisi na wanapigwa sasa kwa nini hawa ni wezi wahalifu wasishughulikiwe???

    ReplyDelete
  9. TATIZA POLISI WANAWAJUA VIZURI HAWA JAMAA NA WANAFAHAMU HATA GARI IKIVYNJWA ENEO GANAI WAMUONE NANI LAKINI UTEKELZAJI HAKUNA RUSHWA IMEOTA MIZIZI NA POLISI WAMO KTK HILO KUNDI WANSHIRIKIANA NA WEZI

    ReplyDelete
  10. Kwa kuwa MALARIA HAIKUBALIKI, BASI UHALIFU NDIO KABISAA HAUKUBALIKI! tutakula nao hao jamaa sahani moja na lazima wafikishwe mbele ya sheria!

    Wenzao machinga Mbeya ndio ni kweli, wanayo haki ya kudai wafanye biashara ila njia haliyotumia ya kisiasa siyo kabisa na wameshughulikiwa itakuwa hawa WEZI , ebo!

    ReplyDelete
  11. Nawapongeza wadau mlioandika izo namba na wengine wenye nazo waziandike ili jamii iwajue awa jamaa maana ni washenzi sana

    ReplyDelete
  12. mimi ni mhanga wa wizi huo jana wamevunja kioo kidogo na kuiba walivyoweza kuiba, na walihisiwa walikuwa na gari salon walikurupushwa mara ya kwanza wakadai wanamsubiri mtu katika parking hizo baada ya muda wakaondoka, nadhani walirudi baadae na kufanikiwa kufanya uhalifu huo. Nimejionea usumbufu wa kuripoti maana adha itakayonipata ya toa maelezooo kisha subiri tukisikia tutakutaarifu nimeona bora nirudishie kioo changu basi mchezo kwisha. Siku tukiwatia mikononi basi watakuwa halali yetu live.

    ReplyDelete
  13. Ni Kwamba kuna siku nilishwahi kuripoti Polisi na baada ya kuona hakuna mafanikio nikaelekea pale mnadani kutafuta replacement. Nilishangaa wale jamaa wakiniambia kabisa description ya gari langu na kisha wakaniambia kuwa kuna polisi mmoja wa pale msimbazi ndiye aliyekuwa ametoa order ya hivyo vifaa. Ilinisikitisha mmo!!

    ReplyDelete
  14. ZA MWIZI NI 40...WADAU nina waarifu ya kuwa taarifa za Wezi T 431 AWU na T746 ABT zimeshafika Idara ya Polisi Makao Makuu sio Police Post na sasa masuala yote mawili yapo ngazi za juu kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...