Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu, Dar es Salaam leo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho. Katikati ni Makamu Mwenyekiti - CCM Bara,Pius Msekwa.
Rais Dkt. Kikwete akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, Ikulu Dar es Salaam, leo.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, akimpa zawadi Makamu Mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa baada ya mazungumzo ya ujumbe wa Chama hicho na Ujumbe wa CCM katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, akiweka shada la maua kwenye eneo la Makaburi ya wataalam wa Kichina alipokwenda kuyaona, eneo la Majohe, Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho na Mwenyeji wake Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM baada ya mazungumzo ya ujumbe wake na wa CCM kuwa na mazungumzo katika ukumbi wa sekretarieti, Ofisi Ndogo yab Makao Makuu ya CCM mtaa wa Lumumba Dar es Salaam. Wengine ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape NNauye, Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama na Katibu wa NEC, Uhusiano wa Kimataifa Januari Makamba.
UJUMBE wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, ukipata maelezo ulipotembelea Kampuni ya Reli ya TAZARA.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akiwa sambamba na Ujumbe wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho katika kutoa heshima za mwisho kwenye eneo la Makaburi ya wataalam wa Kichina,eneo la Majohe, Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho (kushoto), akisoma maelezo kwenye eneo maalum la kumbukumbu lililopo kwenye eneo la Makaburi ya wataalamu wa Kichina, eneo la Majohe Gongolamboto Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na watano ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Nyerere aliwafuata hawa jamaa na ukoministi wao na ndio maana nchi yetu ikabakia maskini.


    Long Live Free Market Capitalism! Long Live Adam Smith! Long Live Milton Friedman!

    ReplyDelete
  2. Vipi Nape, mgongo haupindi?lol!

    ReplyDelete
  3. Ha, ha, ha, haaaaaa. Kaka safari nyingine pinda mgongo zaidi kama wao.

    ReplyDelete
  4. Advocate JashaNovember 12, 2011

    Hapa katibu wa NEC,itikadi na ueneziCCM Nape Mnauye umetuangusha kwa vazi lako kwanini halioani na sehemu yenyewe hasa ukizingatia nafasi yako kiuongozi.Kwa tarabu katika nchi nyingi katika matukio kama hayo uvaliwa mavazi ya rangi nyeusi

    ReplyDelete
  5. Viongozi wa TZ fanyeni mazoezi,Nape hauna tofauti na Mzee Msekwa,ukizingatia wewe ni kizazi kipya kuinama shida.

    ReplyDelete
  6. NYIE MLIO NJE MKIFIWA MNATAKA KUSAFIRISHA KWA GHARAMA, MNAONA WENZENU?

    ReplyDelete
  7. Ucjali tutaanza kusafirisha majivu.

    ReplyDelete
  8. Pinda Mugongo uchiogope

    ReplyDelete
  9. NAFASI ZA MAKABURI ZIMEJAA CHINA. KUNA WATU WENGI NA ARDHI IMEKUWA NDOGO. SISI WABONGO TUTAENDELEA KURUDISHA WATU NYUMBANI KWET TANZANIA. MAPORI MENGI.

    NDIMI BABA YENU
    NATOA DUKUDUDKU

    ReplyDelete
  10. raia wa kichina ni mfano wa kuiga kwa kila hali , huyo anonymous wa kwanza nadhani ni analipuliza bange !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...