On December 14, 2011, United States Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt swore in 41 new Peace Corps Volunteers in a brief ceremony held at the U.S. Embassy in Dar es Salaam. The new volunteers will work in Tanzania for two years in areas of health promotion and environment education and will be stationed in 38 villages and Zonal Health Resource Centers in Masasi, Newala, Mbinga, Songea Rural, Songea Urban, Ludewa, Makete, Njombe, Mufindi, Iringa Rural, Kilolo, Mbeya Rural, Morogoro Urban, Dodoma Urban, Chamwino, Kondoa, Singida Rural, Hanang, Kiteto, Same, Mwanga, Lushoto and Muheza Districts. Pictured are Ambassador Lenhardt (Centre, front row), the guest of honor, Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Agriculture, Food Security, and Cooperatives Engineer Mbogo Futakamba (third from right, front row) and the Peace Corps Country Director Elizabeth O'Malley (right, front row) with the newly sworn in volunteers.
Home
Unlabelled
Ambassador Lenhardt Swears-In 41 New Peace Corps Volunteers
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mimi bado naonya,hawa watu siyo ambassador kama wengi wanavyofikria na wao wanavyojiita.Huu ni mpango maalum wenye siri ya ndani ya kutaka kuichunguza Tanzania na kupandikiza dhana za siri za mkakati wa kuiteka Dunia unaofanywa na Marekani na nchi za Ulaya na Asia.Nashauri vijana wetu wa usalama wa Taifa na Serikali kwa ujumla hususani huko wanakokwenda kujifanyisha kazi,wawe makini na nyendo za hawa watu.
ReplyDeletewamependeza na vitenge vyao....
ReplyDeletehow does someone qualify to have there comments posted?i do enjoy reading people opinions but have no luck getting mine thru.
ReplyDeleteMdau wa kwanza uko SAHIHI kabisa.
ReplyDeleteTuwe makini, hivi ndivyo haya mataifa makubwa yanavyofanya kazi, tunafikiri eti tunasaidiwa lakini siku tutakaposhtuka itakuwa TOO LATE!
Hao ni wapelelezi na si kama tunavyoambiwa eti ni volunteers.
Pia hizi nchi zimefilisika wanatafuta raw materials kwa hali na mali.
Tukumbuke hata enzi za ukoloni walikuja wamisionari kwa malengo zaidi ya umisuionari.
Tuamke Tz.
Mbona Zanzibar hamuwaleti?
ReplyDeleteMdau wa kwanza yupo sahihi kabisa, working two years for free thats long time. lazima kuna kitu wanapata. Usually watu wanavolunteer kwa miezi 3 mpaka mwaka.
ReplyDeleteThey carry out “the intelligence cycle,” the process of collecting, analyzing, and disseminating intelligence information to top US government officials for policy making.Hii ndiyo update na secret mission ya US Intelligence Agency ndani na nje ya Marekani.Kwa mantiki hiyo nikiwa mzarendo japo nipo nje ya Tanzania,nasisitiza serikali iwe makini na hawa watu siyo wazuri hata kidogo na hawatusaidii kutoka moyoni na rohoni bali machoni na midomoni.
ReplyDeletekwani hata wakiwa wapelelezi kuna baya gani yanfanywa na uongozi..KAMA YAPO NI VIZURI NA KAMA HAYAPO WAACHENI WACHUNGUZEEEE.......SEREKALI NI SAFI AU TUNASEMAJE???
ReplyDeletejamaa wako poa sana, kwa wale ambao tulishawahi kuziona kazi zao naamini tulizipenda. wanajituma sana kuliko hata sisi wenyewe wazawa. Nakumbuka wakati nasoma nilishafundishwa nao mara mbili mara ya kwanza O leve na mara ya pili A level. kwa ujumla wako poa sana kuliko hata walimu wetu wazawa!
ReplyDeleteKWA NINI NA SISI TUSITUME VIJANA WETU 41 KWENDA MAREKANI KUFANYA KAZI BILA MALIPO, YAANI KUJITOLEA KWA MIAKA MIWILI?
ReplyDeletenashukuru umeweza kuniweka katika comment zetu ila bado sioni hao peace corps wanatumwa kutupeleza sisi kwani wapo pembe zote za dunia na maambasador pia wapo sehmu nyingi duniani kusema wote ni wapelezi ni ujinga na kama tunawasiwasi nao tunaomba seikali yetu isiwape visa kama wanatunyima visa zao.wacheni watusaidie.
ReplyDeleteWewe anony wa tisa kutoka juu, tongotongo zako nzito sana, lazima utumie alcohol ndiyo zitoke.
ReplyDeletenchi yeyote ya ng'ambo inapotaka kusababisha vulugu ktk nchi fulani jambo kubwa na la muhimu ni kutafuta uimara au mapenzi ya watu kwa nchi yao. Kutafiti ni kiasi gani raia wanampenda kiongozi wao mkuu na nchi kwa ujumla. Ili mpango huu ufanikiwe ni lazima wageni hao wafanye mbinu kuu za kukubaliwa na raia kwanza, na ndiyo maana unaona wanavaa viotenge. Ni hawa walipuuza, vitu vyetu kama: ngoma, majina lugha, vyakula, madawa, elimu, uongozi, demokrasio yetu ya kijadi mahakama zetu za kijadi nk. leo wanajigubika khanga! Wanamdanganya nani?
ReplyDeleteZanzibar wapo wanne mmoja Taasisi ya mama Shadya mwingine wizara ya afya ni nesi na walimu wawili pemba
ReplyDeleteHAWA MI NAONA WANAKUJA KUCHUNGULIA SEBULENI KWETU SASA WATAINGIA CHUMBANI SERIKALI INATAKIWA ICHUKLUE JUKUMU LA HARAKA LA KUWADHIBITI NA KAMA VIPI WATUACHE NA SHIDA ZETU.
ReplyDeleteMDAU FROM MO TOWN MJI WA WAGUMU WAISHIO WAGUMU
Kila siku tunalalamika kuwa viongozi wetu wanahujumu nchi kwa ufisadi, kwamba wanaruhusu rasilimali za nchi yetu ziporwe, na kadhalika.
ReplyDeleteSasa naona anonymous wa kwanza hapa juu anawaomba viongozi hao wawe makini na suala hili la Peace Corps. Yaani ghafla viongozi hao hao tunaowalalamikia wameshakuwa wazalendo wakubwa!
Hapa naona kama anonymous anawakingia kifua na kujaribu kuwasafisha mafisadi.
Halafu, inakuwaje hao wanaoitwa vijana wa usalama wa Taifa hawakuwashika waliofanya hujuma ya EPA au rada? Yaani tunaacha kushughulikia hujuma za wazi kama hizi, tuwe tunatumia nguvu zetu kuwachunga Peace Corps ambao tumekuwa nao tangu siku za mwanzo za Uhuru?
Naamini kuwa mashirika kama Peace Corps yanaisaidia Marekani kuzifahamu nchi zingine, lakini lengo lao vile vile ni kutoa fursa kwa nchi zingine kuwafahamu waMarekani. Kitendo cha waMarekani hao kukaa nchini mwetu kwa mufa wote wanaokaa ni fursa ya sisi kuwaelewa wao. Tunayo hiyo fursa ya wazi.
Lakini sio kweli kwamba lengo pekee au lengo kuu la wa-Marekani ni kuzihujumu nchi zingine. Marekani, sawa na nchi zingine, inahitaji marafiki, washiriki wa biashara, sehemu za kuwekeza na kadhalika. Sio kweli kwamba wa-Marekani wakishatufahamu, kitakachofuata ni wao kutuangamiza.
Sisi wenyewe tuna waTanzania wenzetu wengi huko Marekani na nchi zingine. Hao ni kama macho na masikio yetu ya kuweza kujua kinachoendelea Marekani na huko kwingineko. Lakini nchi yetu imelala.
Kwa mfano, hapakuwa na sababu ya Tanzania kusaini mkataba na kampuni hewa ya Richmond, wakati wa-Tanzania wanaoishi Marekani wangeweza kufanya uchunguzi na kugundua kuwa hii ilikuwa kampuni hewa. Nchi yetu badala ya kuwatumia watu wake wanaoishi nje, iliingia kichwa kichwa kwenye mkataba huo. Na bado haijajifunza.
Tuwe makini. Tutumie fursa zilizopo na pia tutengeneze fursa na kuzitumia. Katika dunia ya leo ya utandawazi wa leo, ni lazima tuwe wepesi wa kufikiri na kuangalia mambo kwa namna inayoendana na ubadilikaji wa haraka wa hali ya ulimwengu.
Kama waMarekani ni wabaya kama inavyosemwa, na kama nchi yao ni hatari kwetu kama inavyosemwa, inakuwaje kuna maelfu ya waTanzania huko Marekani ambao wanapigania uraia wa nchi mbili? Kwa nini wapiganie kukaa katika nchi adui? Nahisi ukweli ni kwamba wanatambua kuwa hii si nchi adui bali tunaweza kushirikiana nayo.
Kwa hilo hata serikali yetu inaunga mkono. Inahimiza mipango ya DICOTA, na nilimsikia JK alivyokuwa anawahimiza wa-Marekani hapa Minnesota kuwekeza Tanzania. Ubalozi wetu hapa Marekani umepewa jukumu la kujenga mahusiano mema na waMarekani na kuhimiza uwekezaji nyumbani kwetu.
Iweje akina anonymous mnang'ang'ania kuwashambulia tu hao Peace Corps? Nina mengi ya kusema, kwani nina uzoefu wa karibu na hao Peace Corps kwa miaka mingi, na ninafahamu kuwa wanatumika katika nchi nyingi, sio Afrika tu bali kwingineko, na wametoa na wanaendelea kutoa mchango mkubwa kwa nchi hizo.