VIONGOZI WAPYA WA KLABU YA COASTAL UNION WALIOCHAGULIWA JULAI 2 MWAKA HUU MAKAO MAKUU YA KLABU HIYO BARAARA 11 JIJINI TANGA, KUTOKA KUSHOTO NI ALBERT PETER (Mjumbe), SALIM AMIR (Mjumbe), AHMED HILAL 'AURORA' (Mwenyekiti), JAMES MWINCHANDE (Mjumbe) NA JULIUS BENJAMIN AMBAYE ALICHAGULIWA KUWA MJUMBE PIA .

Na Mashaka Mhando,Tanga
WAJUMBE wawili wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Coastal Union huenda wakaenguliwa katika nafasi zao kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kutokuhudhuriwa vikao vinavyoitishwa na klabu hiyo.
 
Akizungumza katika mkutano na wanachama wa klabu hiyo uliofanyika juzi makao makuu ya klabu hiyo barabara 11 jijini hapa,Mwenyekiti wa Klabu hiyo,Hemed Aurora alisema kuwa wajumbe hao hivi sasa wanatarajiwa kuandikiwa barua ya kujieleza  ni kwa nini hawadhurii vikao hivyo.
 
Aurora alisema kuwa licha ya kuhudhuriwa vikao hivyo wajumbe hao hawana msaada wowote katika timu hiyo hivyo wameamua bora wakaachia ngazi ili nafasi zao ziweze kuzibwa na wanachama wanye mapenzi ya kuitumikia klabu hiyo.
 
Aliwataja wajumbe hao kuwa ni Kweli Nashon na Julius Benjamini ambao tangia wachagulie hawakuwahi kuhudhuria kikao hata kimoja huku kukiwa hakuna taarifa za wao kutokuhudhuriwa vikao hivyo.
 
Aurora alisema kuwa wajumbe hao wataandikiwa barua ya kuitwa kwenye kikao ili waweze kujieleza wana mchango gani kwenye klabu na sababu zipi zinawafanya kushindwa kuhudhuriwa vikao hivyo..
 
Wakati huo huo,Klabu ya Coastal Union imepata basi jipya kutoka Saruji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...