Washiriki wa kike wakiwa tayari kupiga kasia katika mashindano ya Mitumbwi ya Balimi Extra Lager,hapa wakisubili kulia kwa filimbi na kuondoka.
Washiriki wa shindano la Mitumbwi Balimi Extra Lager wakiwa katikati ya maji wakati a shindano hilo.
Washiriki wa shindano la Mitumbwi Balimi Extra Lager wakiwa tayari kuondoka wakisubili filimbi kupulizwa.
Washiriki wa shindano la Mitumbwi Balimi Extra Lager wakiondoka baada ya filimbi kupulizwa.

Na Michael Machellah - Mwanza

NANSIO Ukerewe waibuka mabingwa na kujinyakulia jumla ya Miliioni 4,800,000, katika Fainali za mashindano ya Mitumbwi ya Balimi Extra Lager yaliyomalizika Mwaloni Jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Fainali za mashindano hayo yaliyokuwa ya Kanda ya ziwa ikishilikisha jinsia zote za kike na kiume,ambapo Ukerewe waliibuka washindi kwa jinsia zote kwa wanaume kikundi cha Martin Mwarabu kutoka Nansio Ukerewe na kujipatia zawadi ya Shilingi Milioni 2,600,000, na kilichoongoza na kwa upande wa wanawake ni Kikundi cha Teddy Totto cha Nansio Ukerewe na kuzawadiwa Shilingi milioni 2,200,000.

Matokeo hayo yalifanya mashidano kuwa na shamrashamra za kushangilia kwa aina yake kwa ngoma ndelemo na vigelegele toka kwa wana Ukerewe waishio Mwanza hivyo kukifanya Kitongoji cha Mwaloni kujaa ndelemo na vifijo.

Washindi wa pili kwa wanaume walikuwa ni kikundi cha Umoja kutoka Bukoba ambao walizawadiwa Shilingi 2,000,000, wa tatu ni kikundi cha Kisolya kutoka Musoma ambao walizawadiwa Shilingi milioni 1,600,000 na wa nne ni kikundi cha Nyalusulya kutoka Musoma pia na washiriki wa tano hadi wa kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi laki nne kila kikundi ambavyo ni Kanchakwizi kutoka Bukoba,Elisha Jacob cha Mwanza,Godfrey Ignatus cha Nansio Ukerewe,Rwekaza kutoka Bukoba,Matinika Hangaika kutoka Mwanza na cha Shija Andrew kutoka Mwanza.

Mshindi wa pili kwa wanawake walikuwa ni kikundi cha Kinesi kutoka Musoma ambacho kilipata Shilingi 1,600,000,cha tatu ni kikundi cha Mfunda Mfunda Mbogo kutoka Mwanza na cha nne ni cha Happiness Mnare kutoka Mwanza na vikundi vingine cha tano hadi kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi laki mbili kila kikundi ambavyo ni Rwagasire kutoka Moma,Tindichebwa Mganga kutoka Mwanza,Busira kutoka Bukoba,Seleka kutoka Bukona,Paskazia Shukurani kutoka Nansio Ukerewe na cha Elizabeth Charles kutoka Mwanza.

Mashindano hayo yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Evarist Ndikilo ambaye ndiye akikuwa mgeni rasmi akisindikizwa na Mkuu wa Wilaya ya Mwanza, Said Amanzi na viongozi wenyeji kutoka Kampuni ya Bia Tanzani waliokuwa ni Meneja wa Bia ya Balimi iliyodhamini mashindano, Edith Bebwa na Meneja mauzo na usambazaji wa Kanda, Malaki Staki.

Shamra shamra za mashindano hayo zilisindikizwa na Ngoma mbalimbali za makabila yanayozunguka Kanda hiyo ikiwemo ya Bugobogobo kutoka Misungwi na wakerewe kutoka Nansio pamoja na wasanii mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. safi sana hii, hio timu ya kina mama ndio imenikosha kweli. Sasa waandaaji na TBL ileteni Dar hii, Msasani Peninsula will be ideal place. You can push nduvu or Castle brand, changamkeni kabla ya SBL!!

    ReplyDelete
  2. Hivi, TBL hawakuona huo uchafu kando ya ziwa na kuusafisha kabla ya shindano au ndio mila yetu hiyo.

    ReplyDelete
  3. safi sana TBL

    ReplyDelete
  4. Ule uchefu vipi? ni jadi yenu wa TZ

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...