Ankle Michuzi,
Habari za hivi punde ni kwamba kuna ajali imetokea eneo la Kitunda Relini iliyo husisha gari ndogo aina ya Toyota Rv4 na Kichwa cha Treni majira ya saa 4:25 asubuhi. Mashuhuda wa ajali hiyo walisema hakuna alie poteza maisha ila majerui ni mmoja na alikimbizwa Hospitalini.

Hatahivyo baadhi ya watu walio shuhudia ajali hiyo wametoa ushauri kwa madereva kuwa makini na alama za barabarani ili kuepukana na ajali zinazo weza kuepukika.
Pichani ni Gari lililo gonga Treni na mashuhuda wakishuhudia tukio hilo.
Gari aina ya Toyota RV4 lililo gonga Treni eneo la Kitunda Relini likiwa limeharibika vibaya.
Pichani juu na chini wasamaria wema wakilinasua gari dogo lililo sababisha ajali toka kwenye njia ya Treni.
Picha zote na Mdau Seif wa Makumbusho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kiberenge kinaweza kufunga break ya ghafla kama gari ya kawaida..
    Nina hakika huyo dereva wa kiberenge amempelekea makusudi huyo mwenye Rav4.
    Tatizo la africa ni mentality mbovu kwa kukosa ustaarabu.

    ReplyDelete
  2. Ndugu zangu, tuachane na kasumba za kupokea kila tunaloambiwa bila kulitafakari kwa maana yake na kiuhalisia wake. Najua mambo ya kisheria yanatuambia tuseme kuwa gari imegonga treni. Ila kiukweli kabisa ni bora turipoti kuwa treni imegonga gari (hali halisi), na mengine tuwaachie wanasheria.

    ReplyDelete
  3. Gari imegongwa natreni au unaweza kusema treni imeigonga gari. Kutuambia gari imeigonga treni ni kutudanganya wazi waziv gari hiyo ilikuwa haendi kiubavu ubavu na kuigonga treni.

    ReplyDelete
  4. cha kushangaza hakuna njia inayovuka hiyo reli so huyu jamaa wa rava 4 sijui alikuwa anakwenda wapi???!!!!
    au ndo dili za kulipwa na insurance

    ReplyDelete
  5. Mengi tutachangia lakini pana maswali mengi kuliko majibu!.

    Kwa kawaida mtu unayeendesha gari unapokuta njia ya Reli au alama za Punda milia ktk barabara taratibu na sheria inasema nini?

    ReplyDelete
  6. Kwa kawaida mtu unayeendesha gari unapokuta njia ya Reli taratibu na sheria inasema nini? Mwenye gari akili hana imekula kwake tena inatakiwa ashitakiwe ailipe tazara.

    ReplyDelete
  7. Ajali popote na ndio hiyo. Ila Gari kugonga treni ni sawa na mtu kugonga gari. Kiwasihi kwa bidii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...