Unapotaja orodha ya Ma Dj vijana wa kitanzania ughaibuni jina la Dj Rama,mwenye maskani yake mjini München, Ujerumani, ni maarufu kwa kurusha mavituzzz katika sherehe mbali mbali. Dj Rama amefanikiwa mara nyingi kuwadatisha akili wadau wa muziki kwa kurusha na kuchanganya muziki wa Tanzania na mingineyo katika sherehe mbali mbali ni juzi tu alikua mmojawapo wa walio tingisha katika sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania,mjini Berlin.
Home
Unlabelled
Introducing DJ RAMA, Germany
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hahahaaaa! Sasa hapa hii habari ili iweje?? Kuna mambo yanayoendeleaga humu huwa siyaelewi kabisa!
ReplyDeleteJamaa anaonekana age imesonga kimtindo, but hana pete kidoleni.
ReplyDeleteSasa tutegemee nini kwa madada zetu huko kwenye ma night club anapofanya hizo DJ's zake
keep it up Dj Rama,na kwa wale wa bongo wasiomfahamu ni mtoto wa pili wa msanii KING MAJUTO.
ReplyDeleteImekuwa ni vizuri kupata habari na picha hii, kama mdau wa kwanza hapo juu unaouliza kutaka kujua ni kwa nini itoke?
ReplyDeleteTumekubali kuwa ulifunika katika kuwapa watu burudani ya muziki kama mchezeshaji muziki!
Sawasawa, Shitaka lako Dj Rama ni moja tu, unatuhumiwa kwa kupindisha utamaduni wetu, wewe unatajwa kuwa ni Mtanzania lakini muonekano wako unakuwa kama mtu wa Marekani!
Hiyo kofia NY ni New York mji uliopo Marekani, ni bora kwa sherehe za miaka 50 ya Uhuru wetu ungeenzi miji yetu kama Arusha ,Mwanza au Tabora ingefaa zaidi!
i see, nilikuwa namsikia wakati nipo Germany lkn sikuwahi kumwona. Kumbe ni mtoto wa bwana Majuto!! wamefanana maskini
ReplyDeleteNafikiri Dj. Rama inabidi ajifunze kujuwa kwao ni wapi? na wajibu wake kama mtu mwenye kwao huko ughaibuni?
ReplyDeletewewe uliesema kuwa dj rama hana pete kidoleni una maanisha nini?
ReplyDeleteusifikiri watu wote wenye wake au wachumba ni lazima wavae pete
mimi mwenyewe nina mke na sivai pete we ndiga nini au ndio wale makaka poa shain zako wacha kuingiza utamaduni wako au wa watu fulani kwa kila mtu
safi sana kukufahamu dj rama big up achana na wapigwa na vumbi chuki binafsi
NY hata Prof J haule hapo juu amevaa na ni mbongo iweje leo Mkaazi wa Ujeru. Acheni kulonga sana.
ReplyDeleteDj chapa kazi kaka.
keep it up. Nimefurahi we mtoto wa King Majuto star wangu bongo...
ReplyDeleteMtoa maoni Mdau wa 8 hapo juu ...NY hata Prof J haule hapo juu amevaa na ni mbongo iweje leo Mkaazi wa Ujeru.
ReplyDeleteMaadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania haikustahili kuwa sehemu ya kuitangaza Marekani na Miji yake!
Prof. J haule yeye ni Mbongo wa Bongo lakini ni walewale kama alivyo Dj. Rama wa huko Ujeru !
Inaonekana kuwa wewe huna ufahamu kuwa wasioelewa wapo Ndani na Nje ya Tanzania!