MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda (pichani), ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, ni miongoni mwa wajumbe walioteuliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuunda kamati maalumu ya kukamilisha mchakato wa kupendekeza Vazi la Taifa.



Wengine wanaounda kamati hiyo itakayoanza kazi rasmi kesho ni Joseph Kusaga (Mwenyekiti), Angela Ngowi (Katibu) na wajumbe ni Habibu Gunze, Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali, Makwaia Kuhenga na Ndesambuka Merinyo.

“Kamati itaanza kazi rasmi Desemba 15 mwaka huu na itatakiwa kukabidhi taarifa yake Februari 28 mwakani,” alisema Dk. Nchimbi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.

Alisema hatua inayofuata sasa ni kuwashirikisha wananchi kuhusu mapendekezo yaliyopo na hatimaye kupendekeza vazi mahususi litakalotambulisha utaifa wa Watanzania.

“Mchakato wa kupata vazi la taifa umeshapiga hatua kubwa, wabunifu wazalendo wa mitindo ya mavazi wameshashirikishwa na kutoa mapendekezo yao,” alisema na kuongeza:
“Utafiti wa namna mataifa mengine yalivyoweza kuteua mavazi yao ya kitaifa ulishafanyika na madhumuni ya kuwa na vazi la taifa ni kuongeza vitambulisho vya utaifa wa Watanzania,” alisema.

Aliongeza kuwa utambulisho mwingine ni Ngao ya Taifa, Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa, Lugha ya Taifa - Kiswahili, Mlima Kilimanjaro, Twiga na Mwenge wa Uhuru.

Alisema vazi hilo litakuwa rasmi kwa wanaume na wanawake na linatarajiwa kuongeza utambulisho zaidi kwa taifa kama ilivyo kwa mataifa mengine yakiwamo ya SwazilandGhanaNigeriaSudanEthiopia na Mali.
Serikali kupitia Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilianzisha mchakato wa kupata vazi la taifa mwaka 2004.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kwasasa hivi kupata vazi la Taifa ni kitu kigumu sana, wangefanikiwa endapo wangelitafuta kipindi tulichopata Uhuru au Mkoloni angelianzisha. Ni sawa na Kenya kutafuta Lugha rasmi ya Taifa kwa kipindi hiki ambacho tayari kila kabila linataka kutambuliwa na kuheshimika zaidi ya lenzake, Tushukuru sana Viongozi waliopigania na kufanya tuwe na Lugha ya Taifa Japokuwa hawakutilia maanani Vazi la Taifa

    ReplyDelete
  2. Vazi la Taifa huwa ni Vazi la kitamaduni na si la kibiashara kusema lishonwe na watu wachache. Lazima liwe na Asili na Maana yake ambapo kila aina ya jamii itaelewa uhalisia na maudhui yake. Wanapofikilia Vitambulisho vya Taifa wasisahau kwamba mavazi ya watu wa magharibi hayana tambulisho zozote za Nchi zao japokuwa ukiyaona unatambua yanatokea ukanda upi. Vivyo hivyo kwa mavaazi ya watu wa kusini mwa Afrika (Afika kusini na Swazilanda). Tukubali kwamba dhana hii ilitupita kipindi ambacho Taifa halijakomaa.

    ReplyDelete
  3. Toka lini na ni wapi vazi la Taifa lilipatikana kwa KAMATI?. Duh

    ReplyDelete
  4. kama hatukuwa na vazi la kitaifa enzi za zamani sijui kama ina haja ya kulibuni sasa. hii itakua tu watu wakijaribu kuiga mavazi ya watu wengine especially ya west africa au kungine. nchi nyingine kama kenya zimejaribu lakini in the end wakaacha. hii iliishia kupoteza pesa na muda. jamani sio lazima tuwe na vazi la kitaifa. hatuja wahi kuwa na vazi la kitaifa na we missed nothing.

    ReplyDelete
  5. huu ni upotezaji wa muda na resources tu. Vazi la Taifa lilitakiwa lijitokeza naturally tu sio kulilazimisha kwa kamati and all. Sifikiri kama watu wa Scotland, Peru. Mexico au Japan waliunda kamati kugundua vazi lao la Taifa. Kama mpaka sasa hatuna vazi just let it go.

    ReplyDelete
  6. In the villages of my beloved country women still have to walk more than 10kms for water, affordable housing is a luxury for the middle class,Panadol is not a tablet you can get easily any place in Tanzania, chicken and eggs are considered luxury by most, milk don't even go there... Now why in the hell are we creating committee to discuss about National dress??? Who is truly a Tanzania? Which culture will you represent in this effort to waste tax payers' hard earn cash? Another 50 years more for utter nonsense. We need to channel our efforts in much more creative manner. First of all we need to ensure the basic demands of our people are met.
    Homer Simpson

    ReplyDelete
  7. Sio vibaya kuwa na vazi la taifa lakini hatuwezi kulilazimisha kuwepo, linaweza kuwepo kutokana na utamaduni, mazingira, wakati n.k.

    Tanzania tuna mambo mengi muhimu zaidi ya kushughulika nayo kuliko vazi la taifa.

    Kwa uchache tuna tatizo la umeme ambalo tumeshindwa hadi sasa kupata solution ya kudumu, maji safi na salama kwa maeneo mengi bado ni shida.

    Mwananchi wa kawaida hasa aishie kijijini sasa bei ya mafuta ya taa kwake ni mzigo unaotokana na tamaa ya wachache especially wachakachuaji.

    Vazi ni kitu ambacho hujileta chenyewe kutokana na hali ya utamaduni wa watu na mazingira yao, wakati, na mambo mengine kadhaa.

    Sioni haja ya kuunda kamati na kutumia pesa za nchi kwa ajili ya vazi la taifa wakati tunashindwa kulipa gharama za umeme n.k. Mtanzania hawezi kushindwa kuzalisha kiuchumi kwa kutokua na vazi la taifa.

    PLEASE TUWEKE PRIORITY/KIPAUMBELE KWA MAMBO YALIYO MUHIMU ZAIDI KWANZA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...