Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera , akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa CHF, Athuman Rehani akitoa mada kuhusu mkakati wa CHF kwa wote.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa CHF, Athuman Rehani wakati wa kongamano hilo.
Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Khamis Mdee akifafanunua mambo wakati wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba (kulia), akiwaeleza waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), umuhimu wa kuuboresha mfuko huo kwa faida kizazi cha sasa na kijacho, wakati wa kongamano la kwanza la waratibu wa mfuko huo nchini, lililofanyika kwenye Hoteli ya Kisasa ya Nashera, mjini Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kushoto), akiagwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emmanuel Humba baada ya kufungua kongamano la kwanza la Waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) nchini, mjini Morogoro jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa CHF, Athuman Rehani.
Moja ya makundi ya Waratibu wa CHF, wakijadiliana jinsi ya kuweka mikakati ya uboreshaji wa mfuko huo.
Baadhi ya Waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) nchini, wakishiriki katika kongamano la kwanza la kujadili na kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za mfuko huo, lililofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, mjini Morogoro jana.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kati kati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dk Emanuel Humba ( watatu kutoka kushoto) na ( watatu kutoka kulia ) ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mgeni Baruani, baada ya Mkuu wa Mkoa kufungua kongamano la kwanza la waratibu wa mfuko wa afya ya jamii ( CHF) jana mjini hapa.(Picha na Richard Mwaikenda na John Nditi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...