Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo (kushoto) akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi uliofanyika nchini mwezi Septemba 2011 leo jijini Dar es Salaam. Katika matokeo hayo wanafunzi 567,567 kati ya 983,545 wamefaulu mtihani huo, wavulana wakiwa ni 62.49% na wasichana wakiwa 54.48% ufaulu ukiongezeka katika masomo ya kiingereza, Kiswahili, Maarifa ya Jamii, Sayansi na Hisabati huku wanafunzi 9736 wakiwa wamefutiwa matokeo yao mkoa wa Manyara ukiongoza.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. wewe mlugo wanafunzi hao unatangaza wanakwenda wapi kwani tumeona tayari walimu wanagoma na walimu wapya hutaki kuajili umekaa unadanganya mara mwezi wa tisa watakuwa kazini mara trh 15 november na siku unajibu swali bungeni ukasema haitafika december walimu wapya hawaja fika vituo vyao vya kazi sasa sijui hao watoto utafundisha wewe na hao wabunge wanaoongezewa posho

    ReplyDelete
  2. Hii elimu yetu ni kiboko, mpaka watoto wa shule za msingi wanafutiwa matokeo

    ReplyDelete
  3. hivi kweli hao viongozi wa elimu wana akili. inatia hasira sana kusikia eti wanafunzi wa shule za msingi wana futiwa mitihani. hii ni aibu tupu.

    ReplyDelete
  4. MHESHIMIWA NAIBU WAZIRI NAOMBA NITOFAUTIANE NA WEWE KUHUSU KUFELI AU KUFAULU. NAFIKIRI TUNGEKUWA SAHIHI KUTUMIA MANENO "WALIOCHAGULIWA NA WASIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE ZA SERIKALI KULINGANA NA NAFASI CHACHE ZILIZOPO".NASEMA HIVYO KWA SABABU UKIENDA SHULE ZA SEMINARY AU INTERNATIONAL, UTAKUTA KUNA MCHANGANYIKO WA WATOTO WANAOITWA WALIOFELI PAMOJA NA WALE WALIOFAULU LAKINI WAKAPUUZIA KUJIUNGA NA SHULE ZA SERIKALI WALIZOPANGIWA. SASA UKIANGALIA MATOKEO YAO WANAPOFIKA KIDATO CHA NNE, UTAONA WANAOONGOZA KATIKA KUFANYA VIZURI NI WALE WA SEMINARY NA INTERNATIONALS. SASA TUJIULIZE WALE WALIOFAULU DARASA LA LASA NINI KIMEWAATHIRI MARA TU WALIPOINGIA SHULE ZA SERIKALI? JE, NINI KIMEFANYIKA KUWASAIDIA WALE AMBAO HAWAKUFAULU DARASA LA SABA WAKAJIUNGA NA SEMINARY AU INTERNATIONAL NA WAKAWA NI TISHIO KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KWA KUFANYA VIZURI? KWA NINI SHULE ZA SERIKALI ZISIIGE MFANO WA SEMINARY AU INTERNATIONA SHOOLS? KWA MAONI YANGU NAFIKIRI NI BORA TUTUMIE "WALIOCHAGULIWA NA WASIOCHAGULIWA KATIKA MTIHANI WA DARASA LA SABA KUJIUMGA NA SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI KULINGANA NA NAFASI ZILIZOPO. MWANAFUNZI MWENYE KIWANGO CHOCHOTE CHA IQ AKIPATA MWALIMU MZURI ANAWEZA KUFANYA MAAJABU, NA MWALIMU MENYE SIFA HIZO, PAMOJA NA MAMBO MENGINE, NI YULE ANAYELIPWA VIZURI NA KWA WAKATI MUAFAKA. MWALIMU ANAYEFIKIRIA MATATIZO KILA WAKATI NI RAHISI KUMPANDIKIZIA MWANAFUNZI YALE ANAYOYAFIKIRIA NA BADALA YA KUMSAIDIA, ANAZIDI KUMFANYA ACHANGANYIKIWE.MWANAFUNZI ANAYECHANGANYIKIWA LEO NDIYO KIONGOZI WA KESHO. ANAPOSAISHWA MIKATABA MIBOVU TUSIMLALAMIKIE MAANA ELIMU ALIYOIPATA HAIKUMSAIDIA,BALI IMEMCHANGANYA. LAKINI TUKUMBUKE KUWA ALIPOMALIZA DARASA LA SABA ALIFANYIWA PATI KUBWA ETI AMEFAULU.

    ReplyDelete
  5. Annym.. wa kwanza hadi inakatisha tamaa nadhani wanakomoa wazazi tu, wala hakuna tatizo,au labda ubabe tu wa viongozi

    ReplyDelete
  6. Haina ukiboko wala nn! ni ujinga tuu wa viongozi wetu ambao wamekalia falsafa za Nyerere ambazo wasomi wanatakiwa kuwa wachache!......wakati hawajui kwamba nchi ndio wanairudisha nyuma!.......

    ReplyDelete
  7. Hamuwalipi walimu mnategemea nini? ufaulu wa wanafunzi utoke wapi? Serikali ni ya kulaumiwa kabisa.

    ReplyDelete
  8. Naiomba serikali ifikirie kwa undani namna ya kuboresha mfumo wetu wa elimu. Kimsingi hali ya sasa ni mbaya mno. Inatia hofu kuona viongozi wetu wakiendelea tu kula kuku utadhani mambo yenda mswano wakati sekta ya elimu inateketea. Hivi huyo Mulugo haoni aibu kuwa naibu waziri katika sekta ambayo ipo hovyo kiasi hicho halafu hakuna mkakati wowote waliouleta kwa wananchi kuboresha hali hiyo? Hivi serikali yetu ipo kwa ajili ya nini hasa, kupanda mashangingi au kufanya kazi ili kuboresha hali ya Mtanzania? DISGUSTING!!

    ReplyDelete
  9. Hivi unapomfutia matokeo mwanafunzi wa Darasa la Saba, aende wapi. Darasa la saba halina kurudia. Hivyo huyo mtoto mdogo wa miaka 12,13 akae mtaani kweli. Me nashindwa kuelewa!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...