Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Tanga, Bombo alipofanya ziara ya kuitembelea hospitali hiyo kujua matatizo yake. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi, Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Rashid Uledi na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Bombo Dkt Fred Mtatifikolo.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa Bombo Dkt Fred Mtatifikolo akisoma taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa tanga ambaye alifika kutembelea hospitali hiyo.
baadhi ya wakuu wa vitengo katika idara mbalimbali katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo wakimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Tanga, wa kwanza kulia ni Katibu wa hospitali hiyo Bw. Adam Lyatuu.
baadhi ya wafanyakazi wa bombo kutoka vitengo vya fedha.
Na Mashaka Mhando,Tanga
MKUU wa mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa, amepiga kambi ya siku tatu kuanzia jana, kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo lukuki yaliopo katika hospitali hiyo kongwe.
Akizungumza jana kwenye kikao chake na watendaji wa hospitali hiyo, Mkuu wa mkoa huyo alisema kufika na kusomewa taarifa na kisha kutembezwa kwenye vitengo vilivyopo hospitalini hapo kwa siku moja, haiwezi kumsaidia kujua kiini cha matatizo anayoyasikia, yanayozungumzwa na malalamiko ya jumla kutoka kwa wananchi.
Alisema matatizo ya hospitali hiyo ambayo ni tumaini kubwa la wananchi kutoka katika wilaya nane za mkoa huo kwa ajili ya matibabu na shida zao mbalimbali, zinahitaji umakini wa utatuzi wake hivyo atanza kukaa na viongozi kisha baadaye kukutana na watendaji katika vitengo vilivyopo katika hospitali hiyo.
“Ndugu zangu Bombo ninayoijua ni hospitali kongwe ina mambo mengi sasa kufika hapa kwa siku moja kusomewa taarifa kisha mtanitembeza kwenye maeneo yenu siwezi kupata ufumbuzi wa matatizo yaliyopo…Mimi nadhani sasa hivi nitakutana na viongozi wachache Katibu wa hospitali na wengine kisha saa nane, nitambelea vitengo kuonana nanyi tena lakini kwa sasa hivi nendeni kaendeleeni na kazi na changamoto zilizopo, tuzigeuze kuwa fulsa ili tupige hatua mbele,” alisema Gallawa.
Awali Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali hiyo ya Bombo Dkt Fred Mtatifikolo, alisema kuwa hospitali hiyo iliyopandishwa hadhi kuwa ya rufaa ya mkoa kwa tangazo la serikali namba 828 la Novemba 12 mwaka jana, ina uwezo wa vitanda 500 lakini kwa sasa vinavyotumika ni 392 tu kutokana na wodi nyingine kubadilishwa matumizi yake.
Hata hivyo, alisema kuna baadhi ya majengo yanahitaji ukarabati mkubwa na mengine yanahitaji kubomolewa ikiwemo vyumba vya upasuaji vya zamani vinafanyiwa marekebisho kuwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) kutokana na kwamba hospitali hiyo kwa sasa haina chumba cha kulaza wagonjwa hao mahututi.
“Hospitali hii katika kipindi cha mwaka jana wagonjwa waliolazwa walikuwa ni 20,320 hii ni wastani wa kupokea na kulazwa wagonjwa 56 kwa siku…wastani wa wagonjwa wa ndani ilikuwa ni 280 huku wodi za wazazi na watoto zikiongoza kufurika wagonjwa,” alisema Dkt Mtatifikolo.
Namuona makongoro kabongo "Ching"
ReplyDeletelazima tuwe reliastic tusijidanganye,matatizo hayo wanayosema sugu si sahihi ni ya kudumu kama hatutabadili mfumo wa maisha yetu kitaifa.Idadi ya watu imeongezeka na sio sambamba na huduma za jamii,hivyo imetoa mwanya wa kudai rushwa katika huduma.Serikali in takwimu kila mwaka za ongezeko la watu lakini mipangilio tulionayo ni ya kuiba kwa kuongeza allowance na marupuprupu mengine kwa viongozi na watendaji badala ya kutafuta mikakati ya kuongeza huduma.
ReplyDeleteTatizo la Bombo kwa ufupi ni kuwa Hopsitali ya Mkoa inafanywa kama hospitali ya wilaya au zahanati ,wakati ilikiwa kuwa referral hospital,tuache sanaa zijengwe hospitali za wilaya Bombo ibaki kuwa referral Hospital,serikali haiwezi kukimbia majukumu yake
ReplyDelete