Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunjo amewataka wadau wa maandalizi ya sera ya Taifa ya Miliki Ubunifu kuhakikisha sera hiyo inakidhi mahitaji ya nchi ya kwa kujenga msingi wa matumizi ya Miliki ubunifu ili kuchangia kikamilifu katika kufikia lengo la Taifa la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025

Mh Mapunjo ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati ikifungua mkutano wa Wadau katika kuandaa sera hiyo, mkutano uliofanyika katika Hotel hya Blue Pearl.

“Ubunifu ni nyenzo muhimu sana ya kuongeza ubora wa bidhaa na huduma zinazozalishwa kwa gharama nafuu. Sera ya Taifa ya Miliki Ubunifu itasaidia kufikiwa kwa malengo ya 2025 ikiwemo kupunguza umasikini nchini. Kufanikishwa kwa lengo hili la kitaifa kutapelekea ukuaji wa uchumi wetu kwa kiwango kati ya 8% hadi 10% katika sekta ya kilimo sambamba na sekta ya viwanda inayotegemewa na karibu 70% ya Watanzania.

Hii itawezekana tu iwapo kutakuwa na maendeleo ya kibiashara na uhamasishaji wa matumizi ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu vya ndani katika masoko ya maeneo EAC na SADC pamoja na masoko mengine ya kimataifa ambako kuna ushindani mkubwa.” Amesema Mapunjo.

Bi Mapunjo ameongeza kuwa, Tanzania imepiga hatua kubwa ya ubunifu katika maeneo nyeti ya kiuchumi kama vile kilimo, kwa hiyo ipo haja ya kuhakikisha uvumbuzi huo unalindwa ipasavyo. Ni muhimu pia kulinda mali asili zetu kama vile utamaduni, na maeneo ya kijiografia. Maeneo mengine yanayohitaji kulindwa ni pamoja na muziki, na sanaa.

Tanzania ni mjumbe wa WTO katika kundi la nchi masikini (LDCs) ambapo inayo fursa ya kufaidika na makubaliano mbalimbali ya kimataifa ambayo hupatikana tu pale ambapo nchi husika itazingatia utekelezaji makini na wa kimkakati wa Sera ya Taifa ya Miliki Ubunifu.
washiriki wa mkutano huo wakiwa katika awamu mbali mbali za mjadala wa pamoja .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. DOKEZO DOGO:
    Maandalizi ya Sera ni vema yaambatane na ususi mzuri wa Kisheria itakayo ilinda sera za miliki bunifu.

    2.Mtego upo kwenye uwezeshaji na ukomavu wa majadiliano, upatanishi na usuluhishi wa kimataifa kwa wanasheria na mawakili wetu wa miliki bunifu.

    3. Utafiti unaonyesha wazi kuwa uanachama ktk WTO sio fanaka dhidi ya migogoro tele ya miliki bunifu kwa sababu nchi zenye mitaji mikubwa zimekua zinapora rasilimali asilia toka zile zinazoendelea bila hata Ahsante achilia mbali kukiri chanzo cha asili ya miliki/ugunduzi wa rasilimali husika. WTO inajua tatizo hili vizuri lakini haiwezi katu kusaidia nchi masikini kwa uwazi sababu ya nguvu nyingi za upenyezo na uwakili wa kufunika mashauri hayo pale yanapo wakilishwa(tena kwa udhaifu)

    3.Nchi tajiri zimejijengea kanda za maslahi na utetezi wa kisheria wa miliki bunifu mf Ulaya magharibi;ulaya ya meditrenian; jumuiya ya dola za kimataifa(ulaya tiifu kwa Urusi); marekani;chache za marekani kusini na mataifa ya uchumi unaoendelea. Sheria na Sera zetu ni vema zitumie changamoto ya ufahamu huu ili kusuka wigo imara utakao leta faida na kulinda maslahi yetu dhidi ya mataifa mabeberu (ambayo hata mwili wa marehemu ni mtaji kwao).

    MAINA Ang'iela OWINO.
    owinoz@yahoo.co.uk

    :Consultant -International Trade and Commercial Law.
    :Excutive Chairman- FEDHA GROUP

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...