Frank Mtao
Kwenu DAVID WAKATI na MR EBBO!

Kazi ya mwisho kufanya nawe, MZEE DAVID WAKATI, ilikuwa ni ya uchunguzi juu ya uelewa wa wananchi kuhusu katiba, ambapo tulizunguka karibu nchi nzima vijijini na mijini, hii yapata takribani miaka 8 iliyopita hivi!


Lakini kumbukumbu ya yale tuliyoyaona na kusikia hakika haitonitoka kamwe.


Leo hii tunapozungumzia katiba, ningetamani sana uwepo na tukumbushane safari yetu hiyo iliyokuwa na mengi ya kuelimisha, kufurahisha na kuhuzunisha!


Hakika nilifurahi na kujifunza mengi toka kwako mkubwa wangu na rafiki yangu mpendwa MZEE DAVID WAKATI!


Hata wiki haijaisha pigo lingine la kuondokewa nawe Mr Ebbo limeniacha na mshangao! 



Ebbo tulipenda kutaniana sana, hasa pale nilipokuwa nikikutania "njaa inakufanya uwe mbunifu"!

Ulitoka kwa aina yako ya kipekee ktk muziki wa bongo na hata baada ya kufungua studio yako, nilikupongeza na kuzidi kukutania zaidi na zaidi! 



Ntacheka vipi utani huo rafiki yangu 
Ebbo ukiwa hauko hapa tukacheka pamoja?

Ingawaje niko mbali huku Australia, ila naungana na ndugu, jamaa na marafiki ktk kipindi hiki kigumu cha kuondokewa nanyi tuliowapenda ila Mwenyezi kawapenda zaidi.


Ewe Mola, uwalaze mahali pema peponi rafiki zangu

 Mr EBBO na DAVID WAKATI
Amina!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. REST IN PEACE, GREAT GUY!
    You gave us a lot of joy and motivation during your times!
    You were the best in Broadcasting, lifted us when we were down, pushed us when we were stuck and carried us through the dire struggles of this Great Nation!
    SIMPLY THE BEST!
    I SALUTE YOU SIR!

    ReplyDelete
  2. Nimestuka sana kwa kifo cha Mr Ebbo,na nilikuwa sijajuwa kama David Wakati nae katangulia mbele ya haki!Mwenyezi Mungu awarehemu wote waliotangulia,,,Rafiki yangu Frank!Kumbe ulijichimbia huko Australia,,,,hukuaga rafiki yangu?,,,Nimekuona nikakumbuka pale mjini C!!wewe na akina Anwary,hivi yupo Dar nae?!!unakumbuka enzi za Nani ni nani na
    2eyes production,...Hiyo picha imekutoa chicha!
    Nimewakumbuka sana Lady Hanny...UK

    ReplyDelete
  3. Hivi wewe ninaekuona kwenye picha mzee Wakati anaweza kuwa rafiki yako au mzee wako? Sijui labda umeniwekea picha ya zamani!

    ReplyDelete
  4. Wabongo tulivyowapuuzi huwa hatumthamini mtu hadi afe.David Wakati angafundisha utangazaji na matamshi mazuri ya lugha hasa kiswahili, ingenogaa. Naye Motika japo kwa lafudhi ya kimasai amefundisha mengi ili tuondokane na fikra potovu na duni hat kufikia kuzomea timu ya taifa letu kwetu. Tumepoteza utaifa kwa utandawazi na ujinga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...