Balozi Ngemara akiwa na viongozi wa UTU.
Siku ya ujumaa ya 9.12.2011 na jumamosi 10.12.2011 Watanzania waishio Ujerumani na nchi jirani wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani,walifanikiwa kulitingisha jiji la Berlin "!
katika sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara, sherehe hizo zilizoongozwa na Balozi Bw. Ngemela na maofisa wa ubalozi akiwemo Bw. Ali Siwa zilianzia katika ukumbi wa Martim ambako kulikua na mkusanyiko wa mabalozi wa nchi mbali mbali,vingozo wa ngazi za juu wa serikali ya Ujerumani,watanzania, mashirika NGO's,na marafiki wahisani wa Tanzania walikuapo kusherekea na kuipongeza Tanzania kwa kufikia miaka 50 ya uhuru kwa amani, Tanzania pia ilipongezwa na kutajwa kuwa nchi ya Amani barani afrika ambayo wananchi wake wameshikama kwa amani na upendo.
Ngoma Africa Band aka FFU chini ya uongozi wake Ras makunja aka Kamanda wa FFU,muziki wa bendi hiyo ulifanaikiwa kuwachanganya uwanjani madipromasia na wadau walioudhuria katika sherehe hizo ijumaa na jumamosi bendi hiyo maarufu inatamba na CD mpya Shangwe 50 Uhuru anniversary.
Pia sherehe hizo ziliambata na ufunguzi wa chama cha Watanzania ujerumani (UTU) ambacho kilifunguliwa rasmi siku ya jumamosi 10.12.2011 na Balozi Mhe.Ngemera ambaye pia ndie aliyetilia mkazo kwa kuanzishwa kwa umoja huo ambao ndio mwavuli wa watanzania wote waishio Ujerumani,Umoja huo umesajaliwa na serikali ya Ujerumani kama NGO's na mwenyekitiki wake Bw.Mfundo Peter Mfundo.
Balozi Ngemera (katikati) akiwa na viongozi wa Umoja wa watanzania Ujerumani UTU.
kamanda Ras Makunja wa FFU alikuapo pia.
Ras Makunja na mzimu wake wa Ngoma Africa band.
washambuliajji wa magitaa wa FFU wakipakua vitu.
watanzania ujerumani hakubaki mtu nyumbani hadi watoto wachanga.
watanzania ujerumani wakijipendelea.


Ndugu Yangu Shaha Bennie Man najua siku hiyo lazima ulitoa show hahahahahaha.
ReplyDeleteMc Leicester Uk.
Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wetu yaliyojiri Dunani kote, yamedhihirisha kuwa tuna timu kamili kama tutashirikiana ipasavyo na kupeana nafasi za kuchangia kulisukuma gurudumu letu la maendeleo mbele!
ReplyDeleteNimefurahishwa sana na jinsi Watanzania walivyo jitoa ina maana kama pana uwezekano wapo Wasmomi ,Wadau na Wataalamu wa kila kada na sekta.
Kilicho baki hapa sasa mambo yasiishie ktk Maadhimishi ya Uhuru bali mipango thabiti iwekwe kwa watu kujipanga na kushirikiana ili tupate maendeleo nyumbani nchini Tanzania.
TAFADHALI SANA MASLAHI YA WOTE WADAU YAZINGATIWE, WAPEWE MAZINGIRA YA KUSHIRIKI KTK MASUALA MBALIMBALI KUHUSU TANZANIA.
1.Mipango kama DIASPORA idumkishwe
2.Suala la Uraia wa nchi mbili (DUAL CITIZENSHIP) lipewe kasi zaidi kutoa vikwazo.
TAFADHALI SANA ,OFISI ZETU ZOTE ZA UBALOZI ZIWAJIBIKE HUKO UGHAIBUNI.
Pamoja tutajenga NCHI!
MUNGU IBARIKI TANZANIA!