Siku za hivi karibuni kumekuwepo taarifa na tahariri kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la kufukuzwa kwa wanafunzi wachache vinara wa uhalifu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

Katika taarifa hizo kumekuwa na madai kwamba kabla ya uamuzi wa Baraza la Chuo wa kuwafukuza wanafunzi hao, milango ya mazungumzo na maridhiano kati ya uongozi na wanafunzi ilikuwa imefungwa, na kwamba wanafunzi hao hawakupewa fursa ya kusikilizwa na kujitetea mbele ya vyombo husika vya Chuo. 

Sisi tunadhani madai haya yameandikwa kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kupotosha yaliyojiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi uamuzi wa kuwafukuza wanafunzi wachache vinara wa uhalifu kufikiwa na Baraza la Chuo. Taarifa hii inaweka bayana hali halisi kuhusu vitendo vya fujo na uhalifu vilivyofanywa na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Awali ya yote tungependa kuwakumbusha wadau wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwamba katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mwelekeo miongoni mwa baadhi ya wanafunzi usio wa kawaida na unaotishia ustawi na heshima ya Chuo hiki. 

Kumejitokeza utamaduni hatari wa makundi madogo ya wanafunzi kuvunja taratibu zote za kisheria na za kiuongozi pale kunapokuwa na jambo fulani linalowakera, kwa kutenda vitendo vya kihalifu wazi wazi wakishinikiza matakwa yao yatekelezwe mara moja. 

 Mara nyingi vitendo hivyo vimekuwa vya uhalifu wa jinai. Mwelekeo huu hatari umekuwa ukikua taratibu, na kadiri siku zinavyopita umeanza kuotesha mizizi na kuimarika kama kwamba ni utamaduni unaopaswa kukubalika ili mradi tu unafanyika ndani ya mipaka ya Chuo.

Dalili za kukua kwa utamaduni huu zilianza kuonekana wazi tarehe 22 mwezi Februari mwaka 2008, pale ambapo baadhi ya wanafunzi waliendesha vurugu kubwa wakati wa usiku katika mabweni na maeneo ya huduma ya chakula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. kusema ukweli huenda wanafunzi wakawa na makosa ila vile vile pale mlimani kuna ma prof ni wanyanyasaji sana na wanapenda kutukuzwa kama Miungu,waliosoma pale watakubaliana na mimi jinsi ma prof wanavyonyanyasa wanafunzi...pale hata mwalimu akiwa hajui humkosoi ukisema kitu umekwenda na maji.hii ndio hali halisi na ndio elimu ya tanzania.

    ReplyDelete
  2. tatizo kubwa mi bado nalaumu sana ni mambo ya siasa kuingilia masomo inabidi serikali iwe makini na hilo kwa nn serikali ikubali kuwe na mataiwi ya siasa vyuoni?jamani ifikie wakati sasa tuzingatie elimu yetu na kuijali ikumbukwe kuwa hao wakuu wa vyama vya siasa wenyewe tayari wana digrii zao na hawana msaada wowote watakao utoa baada ya kushawishi fujo vyuoni na wahusika kufukuzwa sisi wanafunzi tunao soma nje ya nchi ukweli tunasikia uchungu sana hasa kuona wanafunzi wenzetu wanafukuzwa kwa migomo ambayo ukiiangalia sana chanzo chake kinatokana na wanasiasa mbona huku tunakosoma katika nchi za watu hakuna vitu kama hivyo?kwa nn kwetu viwepo?naserikali kuendelea kuviachia tu viwepo? ifikie wakati sasa elimu ya ithaminiwe vijana wasome wapate taaluma zao watakapokuwa katika maisha yao waendelee na vyama vyao wakiwa mitaani na sio vyuoni chakushangaza muda mfupi tu baada ya wanafunzi kufukuzwa walijitokeza watu eti wenyewe hawakupewa taarifa kuwa wanafunzi wamefukuzwa eti sababu yeye ni mbunge wa jimbo hilo ukiwa mbunge ndio ufanye nn sasa jimbo lako linakushinda utaweza mambo ya wanafunzi?ushauri wangu tu kwa vijana wenzangu tusomeni ili tuijenge nchi yetu tusikubali kutumiwa umasikini tulionao ndani na nje ya familia zetu tunaujua wenyewe hakuna wa kutukomboa zaidi ya hiyo elimu tunayo ichezea mungu atubariki sana amen

    ReplyDelete
  3. Nyiew wazazi (udsm management) je mwanao (mwanafunzi)akikunyea mkononi utakata mkono???!! Tafadhalini tafuteni suluhu na sio kukimbilia kufukuza hao vijana chuo tafuteni adhabu mbadala na sio kuwafukuza, mnazidi kulididimiza hili taifa sio kweli kwamba madai yao hayana msingi ni kwamba ni ule dhana potofu ya kitanzania kwamba mtoto hawezi kujitetea mbele ya mzazi hata kama mzazi amekosea.

    ReplyDelete
  4. ONLY IN AFRICA ndo wanazitupa dhahabu na almasi kwa kutojua thamani yake mbeleni.

    ReplyDelete
  5. jifikirie wewe ni prof, unasomesha darasani halafu vinakuja vitoto vinakumwagia maji. yaani nidhamu ya wanafunzi kwa wakuu wao zimepungua sana... sijui nao bange inawasumbua!

    ReplyDelete
  6. Nadhani hapa kuna "abuse of power" kwa upande wa uongozi, na pia kuna kuna swala la "delusion of grandeur" kwa upande wa wanafunzi. Wanafunzi wa chuo kikuu wa Tanzania wana tabia ya kujiona muhimu kuliko umuhimu wao wa kweli.

    Wameshafukuzwa, kuna wale ambao baba zao watawapeleka vyuo binafsi, na kuna wale ambao hawana nafasi hiyo. Sasa kama wewe ulikuwa ukiwafuata wale ambao baba zao watawapeleka vyuo binafsi, na umeshafukuzwa chuo kwa upumbavu wa "tuongezewe pesaaaa!!!" utajiju.

    ReplyDelete
  7. anoni wa 12:35 hakuna kitu chochote kinachohusiana nasiasa hapo hayo mambo ya UDSM wanafunzi kufukuzwa hayakuanza leo.Mambo haya ya migomo yalianza tangu late 60s early 70s wanafunzi walikataa kwenda JKT walirudishwa makwao kama wahalifu na hatimae vinara walifukuzwa hao walikuwa babu zao na bibi zao hawa walio fukuzwa leo. Je hapo palikuwa na mambo ya siasa? kwanza hata chama kilikuwa TANU chama chenye sauti kubwa kuliko CCM. Usichanganye mambo ya siasa na matatizo ya vyuo kwenye 3rdworld. Huko unakosoma wewe mwalimu akikosea unaweza kumsahihisha lakini huku kwetu ni kosa la jinai hulo kwenu mawaziri husika wa Elimu wakiona wanafunzi hawaridhiki na hali halisi ya chuo lazima wataanngalia kosa liko wapi na watalirekebisha kwani wasipoangalia wanaweza kumwaga unga lakini huku kwetu daima kosa ni la mwanafunzi yeye hana haki ya kudai haki zake kwa hiyo wale waoga ndiyo wanaitwa wenye nidhamu Warudisheni wanafunzi kwenye karne ya21 kwani wakati ukuta.

    ReplyDelete
  8. anoni wa 12:35 hakuna kitu chochote kinachohusiana nasiasa hapo hayo mambo ya UDSM wanafunzi kufukuzwa hayakuanza leo.Mambo haya ya migomo yalianza tangu late 60s early 70s wanafunzi walikataa kwenda JKT walirudishwa makwao kama wahalifu na hatimae vinara walifukuzwa hao walikuwa babu zao na bibi zao hawa walio fukuzwa leo. Je hapo palikuwa na mambo ya siasa? kwanza hata chama kilikuwa TANU chama chenye sauti kubwa kuliko CCM. Usichanganye mambo ya siasa na matatizo ya vyuo kwenye 3rdworld. Huko unakosoma wewe mwalimu akikosea unaweza kumsahihisha lakini huku kwetu ni kosa la jinai hulo kwenu mawaziri husika wa Elimu wakiona wanafunzi hawaridhiki na hali halisi ya chuo lazima wataanngalia kosa liko wapi na watalirekebisha kwani wasipoangalia wanaweza kumwaga unga lakini huku kwetu daima kosa ni la mwanafunzi yeye hana haki ya kudai haki zake kwa hiyo wale waoga ndiyo wanaitwa wenye nidhamu Warudisheni wanafunzi kwenye karne ya21 kwani wakati ukuta.

    ReplyDelete
  9. anoni wa 12:35 hakuna kitu chochote kinachohusiana nasiasa hapo hayo mambo ya UDSM wanafunzi kufukuzwa hayakuanza leo.Mambo haya ya migomo yalianza tangu late 60s early 70s wanafunzi walikataa kwenda JKT walirudishwa makwao kama wahalifu na hatimae vinara walifukuzwa hao walikuwa babu zao na bibi zao hawa walio fukuzwa leo. Je hapo palikuwa na mambo ya siasa? kwanza hata chama kilikuwa TANU chama chenye sauti kubwa kuliko CCM. Usichanganye mambo ya siasa na matatizo ya vyuo kwenye 3rdworld. Huko unakosoma wewe mwalimu akikosea unaweza kumsahihisha lakini huku kwetu ni kosa la jinai hulo kwenu mawaziri husika wa Elimu wakiona wanafunzi hawaridhiki na hali halisi ya chuo lazima wataanngalia kosa liko wapi na watalirekebisha kwani wasipoangalia wanaweza kumwaga unga lakini huku kwetu daima kosa ni la mwanafunzi yeye hana haki ya kudai haki zake kwa hiyo wale waoga ndiyo wanaitwa wenye nidhamu Warudisheni wanafunzi kwenye karne ya21 kwani wakati ukuta.

    ReplyDelete
  10. Pamoja na mapungufu yote ambayo yanaweza kuwepo kwa Waalimu bado utaratibu huo wa fujo haukubaliki naunga mkono wanafunzi hao kufukuzwa na ikiwezekana wafungiwe hakuna kujiunga na chuo kingine chochote nchini ili iwe fundisho.
    Lakini pia hesima ya chuo cha dar es salaam haipo tena kwa sasa si chuo cha mtu kukipa kipaumbele, kilichobaki UDSM ni politics, UDSM ilikuwa zamani kwa sasa hakuna kitu hilo lipo wazi. samahanini kama nimewakera.
    #Cheers

    ReplyDelete
  11. NI WANAHARAKATI WA AINA GANI HAO WASIO NA NGUVU YA HOJA KUUSHAWISHI UMA WA UDSM KUKUBALIANA WANACHOKIAMINI BADALA YAKE WANATUMIA HOJA YA NGUVU KWA KUWACHAPA VIBOKO WALE WASIOTAKA MIGOMO TENA KWASABABU AMBAZO WAO WANAHARAKATI HAWAZIFAHAMU? LAKINI PIA ILI UMSHAWISHI MSOMI KUGOMA LAZIMA SABABU UNAZOMPA ZIWE ZIMEJITOSHELEZA KITAARIFA NA KIMANTIKI. NI SAHIHI HAO KUFUKUZWA KABISA KWANI ELIMU HAIJASAIDIA KUBIKIRI FIKRA ZAO

    ReplyDelete
  12. Tatizo liko kwa Uongozi wa chuo na sio vingine jamani!

    Mambo ya siasa yanayosemwa ni kukimbia wajibu tu

    Mali yote ni kupuuzwa kwa haki za wanafunzi

    ReplyDelete
  13. waondolewe tu hao wakaangalie kingine cha kufanya huenda wakapata akili baadae.maana wakiachiwa hata wakapata hizo degree hazitoisaidia jamii baadae ni kupoteza muda2,inakuaje umlazimishe mwanafunzi mwenzio ambae ametulia darasani kujisomea aungane na wewe kuleta fujo??? je huo ndio ushawishi wa hoja? hao ni wavuruga amani na utulivu ambayo inatakiwa ili mwanafunzi asome kitu kiingie kichwani.nadhani walipaswa wakafungwe jela kabisa kwa muda flani ili wajirekebishe na wakitoka wapewe kazi za jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...