Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue akizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika wakati Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa lilipopitisha kwa kauli moja, azimio la ujenzi wa Mnara wa kudumu wa kumbukumbu ya Utumwa na Biashara ya Utumwa, Mnara huo utajengwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kama sehemu ya kuwakumbuka wahanga wa biashara ya utumwa lakini pia mnara huo utatumika kama sehemu ya elimu kwa umma kuhusu madhara na mateso waliyotendewa mamilioni ya waafrika weusi kupitia biashara ya utumwa. katika hotuba yake, Balozi Sefue alisema waafrika ni waungwana ambao wako tayari kusamehe maovu waliyotendewa lakini kamwe hawatasahau.
Na Mwandishi Maalum
New York
Nchi za Afrika zimesema, zinao uungwana wa kutosha kusamehe udhalimu na ukatili wa kutisha ambao waafrika weusi,walifanyiwa kupitia utumwa na biashara ya utumwa.Lakini kamwe hazitaweza kusahau tukio hilo baya kuliko yote katika historia ya mwafrika.
Msimamo huo wa Afrika umetolewa na Mhe. Ombeni Sefue. Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, alipozungumza kwa niaba ya nchi hizo,wakati Baraza Kuu la 66 Umoja wa Mataifai lilipopitisha kwa kauli moja Azimio la Ujenzi wa Mnara wa kudumu wa kumbukumbu ya wahanga wa utumwa na Biashara ya utumwa.
Mnara huo unaotarajiwa kukamilika mwaka 2012 na kugharimu dola za kimarekani milioni 4.5 utajengwa katika eneo maalum hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Tayari mfuko wa ujenzi wa mnara huo umekwisha kuchangiwa zaidi ya dola za kimarekani Milioni Moja na Zabuni kutangazwa.
“Tunapokumbuka na kuadhimisha kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa ni lazima pia na kubwa zaidi kutambua na kuheshimu, nguvu, ustahimilivu na moyo wa ushujaa walioonyesha wahanga hao. Walihimili na kuvumilia ukatili wa kila aina, unyanyasaji, uonevu, ubaguzi, mateso, kukandamizwa, kudhalilishwa. Walihamishwa kwa mamilioni katika makazi yao ya asili na kufungwa minyororo na kupelekwa Amerika. Tu waungwana wa kutosha kusamehe lakini kamwe hatutasahu” akasema Balozi Ombeni Sefue.
Akaongeza kwamba, vitendo walivyotendewa watumwa wa asili ya afrika, vitendo vya ubaguzi wa rangi na udhalilishaji, na madhila mengine, bado ni mambo yanayoendelea hadi sasa dhidi ya mwafrika mweusi.
Akasema Afrika inaungana na nchi za visiwa vya Karibian katika kuhakikisha kwamba ujenzi wa mnara wa kudumu wa kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa unajengwa na kukamilika kwa kile allichosema mnara huo siyo tu utakuwa ni kuwaenzi watumwa, bali pia utakuwa somo tosha kwa vizazi vya sasa na vijavyo kuhusu historia ya utumwa.
Mwakilishi huyo wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akaongeza pia kwamba, ni jambo la kusikitisha kuona historia ya mtu mweusi na mchango wake katika maendeleo ya ustawi wa mataifa waliokopelekwa haujathaminiwa vya kutosha wala kuwekwa katika machapisho na kumbukumbu nyingineza. Jambo alilozema si sawa na halimtendei haki mwafrika mweuzi.
Na kwa sababu hiyo akahimiza umuhimu na ulazimu wa kuandaliwa kwa machapisho yatakayoonyesha kwa kina nafasi na mchango wa watumwa kutoka Afrika katika maendeleo ya Amerika na nchi nyingine duniani.
Baadhi ya wazungumzaji waliopata nafasi ya kuzungumza wakati wa upitishaji wa azimi hilo, licha ya kutoa michango yao na kuahidi kuendelea kuchangia, walitoa wito kwa nchi ambazo maedeleo yake yametokana na kazi kubwa iliyofanywa na watumwa kujitokeza na kuchangia kwa hali na mali ujenzi wa mnara huo wa kumbukumbu.
Aidha wazungumzaji wengine waliyataka mataifa hayo kuutambua mchango wa watumwa kwa kutoona haya kuomba radhi kwa ukatili mkubwa waliowafanyia binadamu wenzao.
Azimio hilo liliopitishwa pamoja na kuazimia ujenzi wa mnara wa kumbukumbu lakini pia linahimiza kuendeleza kazi ya kuielimisha jamii kuhusu adhari za utumwa na biashara ya utumwa, kuanda machapisho na kuendeleza maadhimisho ya siku ya kimataifa ya utumwa na biashara ya utumwa, maadhisho ambayo hufanyika kila mwaka hapa Umoja wa Mataifa.
ni kwel bila waafrica nnchi za ulaya zisingeendelea richa ya kuwatumikisha tuu pia wameiba mali asili zetu . ni haki kwa waafrica kutosahau.
ReplyDeleteSasa mbona wanarudi kiulaini na wanapewa ardhi zetu,tena tunafukuzwa tuwapishe na wanakuja kwa jina tofauti wanajiita wawekezaji??????????Na kingine wanatupiganisha waafrika wenyewe kwa wenyewe.
ReplyDeleteSorry kama wewe ni mkristo kusamehe kunaambatana na kusahau. Kama hujasahau basi hujasamehe, full stop. hakuna cha zaidi, au kama vipi wachukueni wazungu waje kuwa watumwa wenu basi walipie fidia ya babu zetu.
ReplyDeleteLakini ni mpaka lini tutaendelea kuishi kwa historia? Kwani hawa wazungu waliondoka na mikono yetu na akili zetu? Mbona tuna kila kitu cha kutufanya tuendelee na hata kuwapita? Mbona Wachina wameweza?
ReplyDeleteLabda tubadilike kimawazo ndo tutaweza. Kila siku wanatudanganya tu na sasa hivi wanarudi kutuchukulia kila kitu ambacho kingetuwezesha kushindana nao na tunawakaribisha kwa shangwe kwamba ni wawekezaji. Wanasiasa kweli wameshindwa kazi yao ni kulalamika tu na hii ni kutokana na kusaliti ushauri wa kitaalamu kutokakwa wataalamu wetu pamoja na mafundisho ya Mwalimu Nyerere.
Je, Mtu akija akakuibia mali zako zote ukabaki huna kitu huku amekuachia ofisi/shamba, uhai pamoja na watu wako wote utakaa tu uendelee kumlaumu na kumuomba akusaidie kwa kukupa sehemu ya alichokuibia au utafanya bidii kurudi pale ulipokuwa?
Please let's change na tusiilaumu historia huku tukirudia makosa yale yale waliyofanya babu zetu. We can do this and move on. Lets change jamani.........duh!
Mdau wa Mwanza