JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUSITISHA BIASHARA YA WANYAMAPORI HAI
Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa taarifa kuwa kutokana na Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 435 la tarehe 09 Desemba 2011 wafanyabiashara wenye vibali halali vya kumiliki na kusafirisha wanyamapori ambavyo hadi tarehe 18 Agosti, 2011 vilikuwa havijamaliza muda wake kisheria wanatakiwa kusafirisha wanyama hao ndani ya kipindi cha miezi mitatu (siku 90) tangu tarehe 9 Desemba 2011.
Tangazo hili la Serikali limetolewa kwa kutambua kuwa wakati amri ya kusitisha biashara ya wanyamapori hai ilipotolewa tarehe 18 Julai 2011, kuna baadhi ya kampuni ambazo tayari zilikuwa na wanyamapori katika mazizi yao waliokuwa wamekamatwa kwa mujibu wa sheria.
Muda uliotolewa kwa wafanyabiashara ni kwa mujibu wa Kanuni za Ukamataji wa Wanyamapori za mwaka 2010 zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Na. 244 la tarehe 02 Julai, 2010. Kanuni ya 12(4) na (5) ya Kanuni hizo inaelekeza kuwa wanyamapori waliokamatwa kwa ajili ya usafirishaji nje ya nchi kibiashara wanatakiwa wawe wamesafirishwa kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu tangu kukamatwa.
Vilevile, kutokana na Tangazo hilo (Na. 435 la tarehe 09 Desemba 2011) Wizara imezuia Ukamataji, Uingizaji na Usafirishaji wa Wanyamapori hai isipokuwa wadudu tu (Class 21). Hii inatokana pia na Amri ya kuzuia ukamataji ijulikanayo kama The Wildlife Conservation (Capture of Animals) (Prohibition) Order, 2011.
Mwisho, Wizara inapenda kuufahamisha Umma kuwa matumizi mengine ya wanyamapori hai pamoja na mazao yake kwa shughuli zisizo za kibiashara na zenye manufaa kwa Taifa, kama vile utafiti, yanaruhusiwa.
George Matiko
MSEMAJI WA WIZARA
14 Desemba 2011
Uamuzi huu wa kusitisha biashara ya Wanyamapori hai ni wa busara sana ukizingatia haki kwa viumbe hai wote,,,zaidi ya biashara pia mauwaji yao yaangaliwe au yasitishwe pia,,,hawa viumbe hai pia ni wakazi halali wa nchi ya Tanzania na Duniani kama sisi binaadam!
ReplyDeleteKUMFIKIRIA MNYAMA PORI PIA NI UBINAADAM!
Ni aibu kwa taifa kuona wageni ndio wanajua utamu wa nyama ya pori na wanasafirisha wanyanama hai,na cha ajabu nchi kama saouth africa hawana utaratibu huo wala kenya.je sisi ananufaika nani na hujuma hizi??Kwa nini wasije kujenga kama ni vituo vya utafiti hapa kwetu?
ReplyDeleteTAARIFA KWA UMMA HIYO NI NJIA YA KUJIKOSHA TU. WANYAMA WANAIBIWA TUNATAKA MAJIBU KINA NANI WAMEFUNGWA NA IMEKUWAJE? SIYO KUTULETEA HABARI AMBAZO HAZINA KICHWA WALA MIGUU. HIYO QUOTATIONS YA VIFUNGU VYA SHERIA VINAMSAIDIA NANI? WANANCHI TUNAPASWA TUELEZWE MAMBO MEPESI SIYO KUTUJAZIA VIFUNGU AMBAVYO HATUVIELEWI. JE LEO NDIYO MMEGUNDUA HIVYO VIFUNGU BAADA YA KUPITIA MAFAILI?
ReplyDeleteWewe mtoa maoni wa kwanza haukuzungumzia pia wanyama tuanowafuga kama bata kuku mbuzi kondoo nk. Maana hao pia wanachinjwa na wanasafirishwa nje.Naona una double standard kuhusu wanyama.
ReplyDeleteWe mdau wa pili pia wewe kama mtanzania unayo haki ya kula wanyama pori maradi ununue leseni na ukamwinde. Kuhusu wageni pia hawapewi bure hao wanyama wanawanunua kwa fedha za kigeni kwa gharama mara kumi kwa bei unayolipa wewe mtanzania.
ReplyDeleteKuuza wanyama hai nje ni sawa na kuuza mbegu, watazalisha wanyama wao halafu waache kuja kwetu kutalii sababu watakuwa nao wanao. tuweni makini.
ReplyDeleteHII NI BIASHARA HALALI NA IPO MIAKA NA MIAKA TANGU UKOLONI INAFANYIKA ACHA WANYAMA HATA NDEGE HAI WANAUZWA SIONI SABABU YA KUIFUNGIA,ILI MRADI TARATIBU ZINAFUATWA,ANAYESEMA SOUTH AFRICA HAWAFANYI NI MWONGO TENA HAO NDIYO EXPORTERS WAKUBWA SANA.BIASHARA HII INAAJIRI ZAIDI YA WATU LAKI MOJA YAANI TANGU WAKAMATAJI MPAKA EXPORTER MBONI HATUONGELEI WAWINDAJI WAKITALII????
ReplyDelete