Mapema leo, wanafunzi niliowaleta Tanzania mwaka huu wameondoka nchini, baada ya kumaliza masomo ya miezi kadhaa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Wanafunzi hao nami tunaonekana katika picha hapa kushoto, tuliyopiga kwenye hoteli yaWilolesi, mjini Iringa, tarehe 10 Agosti.

Kama nilivyoelezea mara kadhaa katika blogu zangu, tulizunguka sehemu mbali mbali, kama vileKalengaMatema BeachLyulilo naBagamoyo. Baada ya mizunguko hiyo niliwafikisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nami nikarejea Marekani kwani muhula wa masomo ulikuwa unaanza.
HABARI KAMILI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hehe Profesa wasomesha wazungu!!

    ReplyDelete
  2. Kwa maProf.km huyu mbona kazi ipo nikujikweza kwakwenda mbele..hahahah

    ReplyDelete
  3. Mdau anonymous, shukrani kwa ujumbe wako. Nilianza kufundisha mwaka 1976, hapa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 1991, kutokana na sababu mbali mbali, nilifika kwenye chuo nilipo huku Marekani, kufundisha katika idara ya ki-Ingereza.

    Nataka vijana wetu wa Tanzania wasikie hivyo, ili wajijengee moyo wa kuzingatia masomo kwa dhati kama nilivyofanya tangu nilipokuwa kijana mdogo. Kwa kufanya hivyo, nao wataweza kufika mbali. Wasome na kujielimisha kwa bidii sana na kwa dhamiri moja. Hakuna njia za mkato katika masuala haya.

    ReplyDelete
  4. U dont get it, kazi kweli.

    ReplyDelete
  5. Na wewe anonymous wa pili hapo juu, una matatizo. Kazi niliyosomea na ninayofanya ni ualimu, si uchawi.

    Ni wajibu wa mwalimu kuelezea yale anayoyafahamu, anayotafiti na anayofanya katika taaluma na mengine yahusikayo.

    Kwa profesa, wajibu huo ni pamoja na kuandika makala na vitabu, ambavyo vinachangia taaluma, na papo hapo vinamtangaza yeye.

    Hiyo mipango ya ushirikiano baina ya vyuo, ambayo nimeielezea nayo ni suala la kuelezwa mbele ya walimwengu. Kutokana na kuelezea huko watu makini wanaotaka kuanzisha programu za aina hiyo, wakiwemo wa-Tanzania, wananitafuta ili niwape ushauri. Vile vile wanafunzi wanaotafuta program za kujiunga nazo wanatafuta ushauri wangu.

    Kutokana na kuandika vitabu na makala, ambayo nayo ni namna ya kutangaza taaluma na kujitangaza mimi mwenyewe kama mwanataaluma, wengi, wakiwemo wa-Tanzania, wananitafuta ili niwape miongozo na ushauri. Nami sijawahi kuwapuuzia, bali nafanya kila niwezalo kuwamegea ninachojua.

    Hao ni watu makini, tofauti na wewe ambaye akili zako zimelala. Una mawazo ya wachawi, ambao wanajificha wasijulikane. Kauli yako imenikumbusha kitu kimoja. Nimepita sehemu kadhaa za Tanzania ambako watu wanaogopa hata kujenga nyumba bora, kwa sababu wataonekana wanajikweza, na sehemu zingine wanakuambia kabisa wanaogopa kulogwa. Naona huu ndio utaratibu unaoutaka wewe, ila usitegemee kama nitayumbishwa na watu kama wewe.

    ReplyDelete
  6. Prof. Mbele, Hongera kwa kazi yako,Pole kwa kueleweka vibaya kwa baadhi ya watu na pia endelea na kazi yako.

    Baadhi ya watu sio waelewa kwa vile wanachukulia Social media kama hii blogu ni sehemu ya kujikwezea kumbe sio hivyo.

    Kwa maelezo yako ya maoni ya tano 5 hapo juu yamejitosheleza kwa sababu kazi yako ni Muhadhiri na muelimishaji na kuwa unahitaji kuwafikia wengi kadri iwezekanavyo ili mawazo yako yafike na pia uweze kubadilishana mawazo na wengine.

    Mfano ktk blogu hii ili kuthibitisha hilo tumeona baadhi ya watoa Maoni wakiendesha Experiments (Majarobio ya kisayansi ) na kuwezesha mawazo yao kuwafikia wengi huku ikiwa ni maoni yao tu kulingana na mtazamo wao!.

    Hii blogu ni sahihi kama ulivyofanya Prof. Mbele kutumika kama njia ya kuelemishana ,kutoa kile ulicho nacho mfano elimu na shughuli zako ili tushirikiane kwa faida ya wote!

    ReplyDelete
  7. Mdau mtoa maoni wa pili, tafadhali elewa kuwa kwa mtu al;iefikia kitwa 'Prof. Mbele' huku akiwa anafundisha ktk nchi za wanaofahamu kama Marekani tayari amekwisha kuwa maarufu hivyo hana anachotafuta ktk blogu hii zaidi ya kuifikisha fikra zake na kazi ya mikono yake na kushirikiana na wengi kwa nia ya wote kunufaika!.

    Dunia imekuwa kijiji kwa uwepo wa teknolojia za kisasa za mawasiliano.

    Hakuna njia ya muujiza kwa watu kufikiana isipokuwa vitu kama hii blogu ''social media'' huku Ankali akituwezesha!

    ReplyDelete
  8. Mdau mfano wa matumizi mazuri na endelevu ya ''social media'' kama anavyofanya Mdau Prof.Mbele kuwafikia wanafunzi wake kielimu kwa njia ya blogu, ni zile experiments (majaribio ya kisayansi) zilizofanywa ktk maoni ya wadau kama ile posting ya UZURI WA TAUSI DUME, inafurahisha watu wakilumbana kwa hoja na mifano hai kupitia Blogu ya jamii!!

    Blogu ya jamii ifahamike kuwa sio ''exposure'' bali ni uwezeshwaji wa watu waliokuwa sehemu tofauti kijiografia kuwa pamoja kifikra!

    ReplyDelete
  9. Profu. Acha kubishana na hawa watoto wa tandamti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...