Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa pole baadhi ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es salaam kwenye shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa wakati alipowatembelea leo Desemba 31, 2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea Dar es salaam ambao wameweka kambi katika shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa leo Desemba 31, 2011.
Vijana wakipika ugali kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya Dar es salaam walioweka kambi kwenye shule ya sekondari ya Benjamin jijini Dar es salaam wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowatembelea leo Desemba 31, 2011.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Imagine hayo majasho yanoingia ndani ya ugali huo, yani ina maana wameshindwa kabisa kufunika vichwa vyao???

    ReplyDelete
  2. wafunike vichwa? Sawa. je na hizo kofia zikiingia kwenye ugali itakuwaje???

    ReplyDelete
  3. hata mie niliwaza hivyo kabla sijasoma maoni ni kweli ndugu yangu nakuunga mkono

    ReplyDelete
  4. Inanikumbusha jeshini (JKT) enzi hizo jinsi ugali na mboga ulivyokuwa unapikwa kama hivi, wakati huo masufuria yalikuwa mapipa (drums) yaliyokuwa yanakatwa, pipa moja linakatwa katikati na kupata masufuria mawili. Wakati huo vijana wa kiume ndio walioweza kupika ugali wa JKT dada zetu walikuwa wanakuja kula kilichopikwa na kaka zao maana upishi kama huu unahitaji misuli hasa, vijana wengi wapishi walikuwa wale volunteers maana walipata mafunzo wakiwa jandoni, sisi compulsory tulikuwa tunapata ujuzi toka kwao.

    ReplyDelete
  5. hebu wacheni kuropoka ropoka hovyo jasho jasho jasho non sense, hawa ni watu wenyewe wamejitolea kwa hiyo watu wasile sababu ya jasho, hamjui shida nyie????

    ReplyDelete
  6. nani kasema ugali unasongwa na wanawake?

    ReplyDelete
  7. wakifunika vichwa jasho halitawatoka? mifuniko ya vichwa inazuia kutokwa na jasho? think man! think man!!!

    ReplyDelete
  8. jua, moto, mvuke, na kazi ya kusokota ugali usitokwe na jasho umekuwa nani? na kazi yenyewe ni ya kujitolea hulipwi. mnatakiwa kupongeza na si kukashifu.

    ReplyDelete
  9. acheni kutoa comment za kukashifu hao vijana wewe mbona hujajitolea hata kwenda kupika chai?vitu vyengine uwe unafikiria kwanza kabla ya kusema!hata kama majasho wewe yanakuhusu nini? wewe ndiye unakula huo ugali? wenyewe mbona hawakuwakataa wasipike?mijitu mingine ikiona picha hapa kazi kulopoka tu!habari ndiyo hiyo hata ukichukia messagge sent!

    ReplyDelete
  10. NIMEJISIKIA FAHARI SANA KWA HAWA KAKA ZANGU KWA MOYO WAO WA KUJITUMA KUPIKA NGUNGA/SIMA/SAZA/KUON/UGALI/GARI/SEMBE/ HILI KWA AKILI NA NGUVU ZAO ZOTE.

    YAWEZEKANA WALIHAKIKISHA WATOTO, MAMA NA WAZEE WAKASHIBA KWANZA NDIPO WAO WAKALA AU WAKAKOSA KABISA.

    HUU NDIYO MOYO WA KUJENGA TAIFA.

    HAYA NDIYO MAPINDUZI NA MAADILI TULIYOYATAKA KWA VIONGOZI WETU BORA.

    2.(UTANI) KAKA HAWA NAONA WATANI WA JADI (KWA SARE ZAO).

    MAINA OWINO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...