Kaka ISSa,
Naomba uiweke hii mada kwenye blog wadau watoe maoni yao,kumekuwepo na wananchi kulazimishwa kulipa malipo bila kuhusishwa katika mambo yanayotuhusu sisi wenyewe,tumepewa barua toka halmashauri ya manispaa ya ilala kuwa ada ya kukusanya taka imepanda toka shs elfu 30,000 kwa mwezi hadi 100,000.00(laki moja)kwa mwezi kwa maofisi.Hii ni kwa upanga mashariki,upanga magharibi ni elfu 3000 kwa kaya na shs elfu 5,000.00 kwa ofisi,tofauti hii ni kwa eneo la upanga,je ni kigezo gani kimetumika kuwekewa ongezeko la zaidi ya percent mia mbili?-nawasilisha mdau -adam
Ninakushauri kaka usifumbie macho upumbavu huu sbb kama niserikali haina wasomi wala haina huruma kwa raia wake!Ninakuomba tafuta kitabu tafuta saport za watanzania wenzako kwa kuandika majina na kutia sain halafu shirikianeni na hao mnaolipishwa nao kuwaburuza mahakamani wanaohusika sbb hapo wazi mnafanyiwa mabaya na watu fulani ama serikali yenyewe hiyo sio sahihi kabisa ukiangalia!
ReplyDeleteJamani hii kulipia taka sijui sungusungu,,mbona sasa imekuwa ni kero,,taka zenyewe zinakaa wewe mpaka zinawaozea,na sidhani kama serikali inayo habari ya pesa hizi tunazozichanga,,kila siku wanapandisha bei,,yaani wameishaona kama sisi watu wa Upanga ndo wa kuchunwa kila siku!!!!Kwani mikuta ya wakazi wa Upnaga imeisha?Jaribu kupeleka hilo shtaka mkutanoni,tatizo lingine matatizo ya raiya huwa yanaishia hapo hapo mtaani watu hawachukulii manani kufuatilia,,niko na wasi wasi isije tukachoka ikawa kama Tunisia au Egypt,maana ukimuona kobe kainama ujuwe anatunga sheria,ukimpa mtu shavu la kulia akuzabe kibao,la kushoto ukimnyaka mkono amekwisha!!!Yaani mimi nimeuchukia Tanzania,,,,,mpaka basi,,Ufisadi rushwa,ubaguzi,wizi,,na mambo mengi tu mabaya,,,,nimzaliwa wa Tanzania rangi yangu ni mweusi lakini huwa najihisi kama labda,,sisi wazalendo tusokuwa na vyeo serikalini tuna rangi za kijani,,kwa jina lingine au ni mimea wao tu watuvuneee wee mpaka tukauke,,ukipata shida huna hata kwa kushitaki,,,maana kesi ya mwizi wa chini unampelekea mwizi wa juu,,ukisema ngoja hapa nifanye kila kitu halali ndo wao wanakunyanyasa wee mpaka ushindwe kwa kwenda,,hivi hii ni nini?ni kuanzia NHC mpaka sungusungu,,Eee Mola tukinge na watu hawa!!!!Ahlam!!!!
ReplyDelete