Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Sam Elangallor akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa wawakilishi kutoka katika makampuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel nakuhudhuria na wadau mbalimbali na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa semina ya Airtel money inayotolewa kwa makapuni mbalimbali leo kwa muda wa siku mbili, uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na wadau wengi na waandishi wa habari.
Mmoja wa wakilishi kutoka katika makampuni yaliyohudhuria semina ya huduma za Airtel money akichangia hoja wakati wa semina hiyo iliyozinduliwa rasmi leo na kuendesha na Mkurugenzi wa Airtel Sam Ellangallor na Mkurugenzi wa fedha Kalpesh Meltha katika ofisi za makao makuu ya Airtel.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...