Baada ya usafiri wa daladala kuwa wa shida leo Ankal kaamua kupanda bodaboda ili awahi kupiga boxi
Pilot yuko makini sana ila mwendo wake ni ule wa 'sanda mkobani'
Ankal na pilot wake wanaibukia Jangwani ambako kunatandazwa bonge la mkeka la kuibukia Kigogo. Mambo ya kupita Migomigo itakuwa hadithi..
Tatizo mafuriko yamekula daraja...na wakandarasi wako katika kuweka mambo sawa pale karibu na klabu ya nanihii..
Ikabidi Ankal na pilot wake wakodishe deiwaka kuwavushia bodaboda lao, maana wadau wa Jangwani baada ya kuathirika na mafuriko imebidi wavunje nyumba zao na kuhamia kuleeeeee. hata hivyo Ankal aliwahi kupiga boxi...Shhhhhhhhhh...usimwambie mtu kuwa Ankal anatumiaga usafiri huu...noma!
ankal next time piga helmet, dereva abaki kichwa wazi, ala!.. mteja mfalme bwana, ikiwezekana hata protection jacket uvae wewe sio yeye....wanaoumia zaidi kwa ajali za boda2 ni abiria sio madereva....chunguza njomba utabaini.....
ReplyDeleteKama hali yenyewe ndo hii basi mi sirudi bongo hata kwa bunduki! Yaani kwa TZ maskini na tajiri wote wanashare same circumstance. Tajiri hata akiwa na Cadillac Limo lake ataliendeshea wapi Bongo hali hiyo? Kazi tunayo. Halafu Michuzi nakushauri next time vaa helmet aisee, style hiyo hakuna usalama kabisa hapo! Duh!!
ReplyDeleteheshima kwako ankal !
ReplyDeleteinasikitisha ankal umekosa hata kuvaa helmet wewe ni mtu mkubwa halafu ikitokea bahati mbaya utasemaje ndio ajali .
ankali wewe ni mtu mkubwa na muhimu katika jamii ya kitanzania unasomwa kila kona ya dunia kuwa makini na mambo kama haya .
mdau northampton uk
sanda mkobani tena....aloo anko eeeh!
ReplyDeletemjomba vaa helmet huo ubongo hazina. Tafadhali wewe ukivaa helmet na wajomba wetu watavaa.
ReplyDeleteAcha ujinga ww...ulitaka tajiri apite angani maskini apite ardhini,,,kaa US na ubaguzi wako hatukuhitaji wala hatuhitaji maoni yako yenye kuonesha ulivyo na upeo mdogo! US US , US KITU GANI! Ata huoni aibu kujiita Mdau US...! wabongo bana...sio kwa sababu kuna uhuru wa kutoa mawazo basi uje ututolee pumba zako hapa...halafu unampa Michuzi usahuri...una ushauri gani wa kumpa mtu wewe!?! Busara hainunuliwi dukani anony...loh!
ReplyDeleteAnkal unatutisha maana nilifikiri utaulizia hiyo kofia ya usalama kwanza upewe ili ukae kwenye hiyo bodaboda yako sasa kama wewe umeweza panda tu na kuweka picha yako humu basi sisi mbumbumbu kabisa tumekwisha maana mimi niulizwa na traffic nitamuuliza tu mbona ankal alipanda bila kofia hamkusema kitu mnatuonea sisi wanyonge tu.
ReplyDeleteKwa taarifa yenu, Ankal aliweka LIMO yake pembeni kwa kuwa sehemu hiyo lazima upande boda boda au baiskeli, safi sana kwa kuhakikisha unapata habari kwa njia yoyote!!!
ReplyDeleteAnkali pole na majukumu!
ReplyDeleteMausafiri ya namna hiyo ndio utu uzima wenyewe wa uasikari katika upiganaji!
Suala la helimeti na mambo mengine ni upande mwingine, pana hali inatokea inapobidi mfano ''Mahala pasipo na Dakitari'' je unaweza kuahirisha kuugua?
Daima mpiganaji katika vita hachagui silaha wala bunduki!
Kweli unajituma katika Libeneke na kwa vile unaenda kulingana na hali halisi tuliyonayo!
Sssssshhhhhhh usiseme sana maana Ankal hajavaa kofia ya kuzuia ajali, TIGo wakimuona watamlamba pesa ! ohooo
ReplyDeleteuncle toa mfano vaa helmet wee mtu mkubwa bwana watu wote tunakuangalia,role model kwa wengine
ReplyDeleteShija uko sawa, nilikuja huku ili nimwambie ankal hilo. Maana hapo kipindi cha (UBU) hakijakufikia kabisa Ankal. Faini 20,000/= maana najua huwezi chakachua kwa kuondoa 0.
ReplyDeleteHAHAHA UNCLE WEWE NI NOMA.. I LIKE UA LIFE STYLE UNAJICHANGANYA KOTE KOTE.
ReplyDeleteDuh Ankal unatutisha!!!!....isipokuwa rangi tu, hilo shati lako ukiwa katika boda boda kama gwandazzz vile!!!
ReplyDeleteAhh mambo ya maslahi bana, usije kuwa tayari umeshajaziwa katika akaunti ukawa umeungana na itikadi ya Kanda ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini!
Ankal umevaa kiserikali!.... Pole na majukumu
ReplyDeleteAnkal wewe bado tunakupenda ila umeonyesha hali ya hatari sana inakuaje umepanda bodaboda bili kuvaa helment kichwani????/ Next time hakikisha kwamba unavaa helmet kwani hii ni hatari sana kupanda pikipiki bila kuvaa helmet! Usirudie tena bado jamii inakuhitaji banaa alaaaa!
ReplyDeleteHahaa Ankal mimi pia ndo usafuru wangu huo lakini nikypnda Bodaboda mi ndiye nayevaa Helmet ili mwendeshaji awe makini akijua kichwa chake ki wazi.
ReplyDeleteEnhee Ankali katika usafiri huku na li shati la Umugambo,,,mara nyingi tunakuona katika mashati na tisheti za kawaida ila leo katika shati la mifuko zito...ndio safari ya Kumwitu nini?
ReplyDeleteMaana harakati, itikadi, uenezi wetu na hisia zetu zinaashiriwa na aina ya mashati tunayovaa!
Ahhh ila usije ukaingia Msituni, na tumalizane mezani na Majukwaani tafadhali!
Anonym wa US uelewa wako mdogo sana. Xcscschwiiiiiiiiiii. Elewa mkataa kwao ni Mtumwa. Falsana weye??@:@::::£$%"&!^%
ReplyDeleteAnkal salama natumai ni mzima wa afya uminisikitisha sana kukuona umepanda piki piki bila helmet wewe kama role model for our new generation to come na mtu ambaye huko kwenye macho ya watu all the time you should be setting good examples.
ReplyDeleteankal sasa unawachokoza wale walala hoi wa nchi za ng'ambo kwa hilo neno lako la KUPIGA BOX nchokoz weye njomba,
ReplyDeleteHahaha Ankal na neno la KIPIGA BOX hajakosea kwa vile sambamba na neno hilo hebu tuangalie ameva shati Kadeti Jeusi zito lenye double pocket ''shati la mifuko miwili'' ingawa wengine wamemsoma katika Msimamo wa Kisiasa ni mtazamo tu,,,ingawa yeye ametaka kuashiria yupo katika kazi nzito!
ReplyDeleteDuhh Itikadi zetu za ki Siasa zimetufikisha sasa tuna soma watu kwa kulingana na aina ya mashati waliyovaa ,,ahhh hii kubwa!
ReplyDelete