Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli akiongea kwa msisitizo wakati alipoongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya Wizara hiyo kuhusu upanuzi wa barabara ya Kilwa Road yenye kilomita 5.1 kwa kiwanga cha lami itakayojengwa kwa marudio na mkandarasi Kajima Corporation. Barabara hiyo inarudiwa kujengwa kwa mara ya pili baada ya kampuni hiyo kuboronga katika ujenzi wa awali, Waziri Magufuli ameongeza kwamba Mkandarasi ataondoa tabaka la lami katika urefu wa Kilomita 5.1 na tabaka jipya la lami lenye unene wa sentimeta 7 akitumia lami yenye kiwango cha ugumu cha 40/50 na kokoto za ukubwa wa milimita 20. Yaani zege la lami (Asphalt Concrete) lenye kokoto za ukubwa wa milimita 20 (AC20), lami iliyoimarishwa zaidi itafikiriwa kutumika sehemu za barabara zenye kubeba mzigo mkubwa zaidi, katika picha kulia ni Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mh. Masaki Okada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Tanzania Bila Magufuli, Haitaenda Popote! Huyu Jamaa yuko Makini na Kazi yake na anachokisisitiza, Watanzania Mlioenda shule Mlindeni huyu Bwana Kwani ni Zawadi Kwa Taifa.

    ReplyDelete
  2. wakati wote wanajenga nyie mlikuwa wapi?usitoe macho ukajiona wa maana sasa kwa mtindo huu ndiyo maana ni vigumu kwa mataifa tajiri kuwekeza nchini kwa sababu hatuko makini na mambo yetu.haya ni sawa kwa watu wanaoishi mabondeni kuwaacha mpaka maafa yatokee.Ningependekeza tujikague kila kuanzia siku ya kwanza tusisubiri mpaka kazi imeisha.wanaoishi mabondeni kama wangetolewa siku walipoanza kuchimba msingi serikali isingeingia gharama ya kutafuta viwanja leo kwa ajili yao.mambo mengi yanafanyika Tanzania kienyeji kama vile hakuna serikali.Viongozi wetu wanaota dili zaidi kuliko kuwajibika.

    ReplyDelete
  3. kweli watanzania tukiamua tunaweza, wamezoea sana hao wanadhani tz shamba la bibi. safi sana Magufuli kwa kazi nzuri, songa mbele baba.

    ReplyDelete
  4. Piga kazi babaake, acha wanakutumia kuuza sura waendelee na biashara yao!

    ReplyDelete
  5. Magufuli, hongera kwa kujali viwango, muda na ufanisi kwa faida ya Watanzania. Lakini, inakuwaje hadi ujenzi unakamilika ndio mnaliona hili? Ni nani alipaswa kukagua na kukupa taarifa? Na ukaguzi hufanyika kwa kila kilometa ngapi zilizotengenezwa au kila baada ya muda gani? Kaza buti, lakini zuia kufikia hatua hii ikiwezekana.

    ReplyDelete
  6. Yaani nimeipenda sana hii.... We need five more like you... Thats progress...!!

    ReplyDelete
  7. Alikuwa wapi mpaka barabara inakamilika ndio aseme irudiwe.? Hii ilitakiwa ionekane tangia mwanzo wa ujenzi.pia wakandarasi wa serikali waliosimamia ujenzi huu hapo awali wamewajibishwa"?

    ReplyDelete
  8. Magufuli for Prime minister 2015.!! we need more leaders like him to move in the right direction..Keep up the good work.

    ReplyDelete
  9. KAKA onyesha wewe ni mfano kama wangekuwepo kumi wengine kama wewe,basi tanzania ingenyoka, acha wale lakini na sisi angalau tufaidike kidogo,washike hao mashati hata wakileta kung FU mbele kwa mbele.

    Kaza buti mkuu utapeli umezidi huko

    mdau belgium

    ReplyDelete
  10. mchangiaji wa pili kichwa cha mbuzi mtupu!!

    ReplyDelete
  11. makufuli mimi na wewe tuko juuuuu.

    ReplyDelete
  12. Hongera sana Mr.Data (Bw. Magufuli)!!!. Pongezi zangu pia kwa mpango thabiti wa kuanzisha usafiri wa majini kwenda Bagamoyo. Haya nyie Wabunge mliopiga kelele, semeni la kusema kwa data alizowapa. Nanyi mnaosema mpaka barabara inafikia hapo mlikuwa wapi? Hebu jiulizeni, wakati wa ujenzi mkataba wao unawaruhusu wa TZ kukagua? sio mnatoa lawama tu.

    ReplyDelete
  13. wakati barabara hii inajengwa magufuri RAISI alimwondoa na kumtupa kwenye wizara ya kitoweo,hakuwepo kabisaa kwenye barabara hii.Aliyekuwepo alikuwa ni Mramba,na waliifungua kwa mbwembwe pamoja na raisi kupanda miti ambayo haikutunzwa imejifia yenyewe. Magufuli hana hatia katika ubovu wa hii barabara ,alikuwa anafukuzana na wezi wa samaki

    ReplyDelete
  14. Hivi huyu jamaa apewe wizara gani imshinde? I wish, next time aletwe wizara ya elimu ama afya kwa kweli. Maana serikali inamizigo mingi isiyo bebeka. Magufuli oyeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  15. Jamani hizi kazi za ujenzi wa barabara zinafanywa kwa mfumo wa "Turn Key Projects", yaani unaruhusiwa kukagua na kukabidhiwa kazi ikishakamilika, na sio wakati kazi inaendelea, thats why hao Wajep wamakubali kuirudia baada ya Magufuli kukataa kuipokea wakati wa makabidhiano.

    ReplyDelete
  16. BILA YEYE KITU GANI BWANA DAWA NI KUWATOA TU MADARAKANI WOTE HAO WANAPANDISHA NAULI YA KIVUKO OVYO HAWA NI CHAMA KINGINE TU KITAWALA WANAANCH TUWE NA MAAMUZI SAHIHI TUNAVYOWACHAGUA VIONGOZI

    ReplyDelete
  17. TUSIISHIE KURUDIA UJENZI WA BARABARA YA KILWA NA KUWAGHARIMU WAHISANI WETU JAPANI BURE!.

    ANGALIA SASA MADHARA YA UFISADI UTAYAONA HAPA CHINI KAMA UNATUMIA AKILI:::::

    MADHARA YA UFISADI::::
    (HIYO GHARAMA YA UJENZI WA PILI INGEELEKEZWA KTK MAENEO MENGINE YA USTAWI WA JAMII KAMA ELIMU, NA AFYA NA MENGINEYO MUHIMU MATOKEO YAKE GHARAMA INARUDIWA MARA YA PILI KWA KUBORONGA MRADI MARA YA KWANZA)

    HIVI WANDUGU KWA MTAJI HUO HAPO JUU KUNA SABABU YA KUUBEBA UFISADI?

    HAPA INATAKIWA HAO WALIOSHIRIKI UFISADI NA WIZI (KAJIMA NA HAO WEZI WALIOSHIRIKIANA NAO KWA KUWAPA WAHINDI MRADI) KWA KUJENGA BARABARA CHINI YA KIWANGO WAKAMATWE MARA MOJA NA WAFIKISHWE KTK SHERIA!

    ReplyDelete
  18. Mbona inazungumzwa 5.1km wakati barabara ni around 12km na kote ni kubovu?

    ReplyDelete
  19. kwani pesa walizokula mwanzoni hazikuwatosha hivyo wameamua kuanza kula mara ya pili kwenye barabara hiyo hiyo

    ReplyDelete
  20. Magufuli mimi binafsi namkubali, tatizo ni chama tuuuuu!! Yaani mtu kama huyu walitaka kumpoteza kwa kumuingilia hadi akaamua ajiulu, mzee wa Magogoni (whitehouse) akaona ilishakuwa noma. Sasa acha watu wazoee kuishi ktk eneo la barabara siku ya upanuzi wa barabara watalia tena. Sasa kipi bora kujenga ukuta ama kuziba ufa? Ni kweli nakumbuka wakati jamaa anadili na samaki, kuku, ng'ombe n.k. ndiyo barabara ilikuwa inajengwa.

    ReplyDelete
  21. wakichukia WAPIGE MBIZI

    ReplyDelete
  22. MIRADI INAYOFANYWA CHINI YA KIWANGO:

    Pana umuhimu wa kutoa Semina za Uwezeshaji wa Kibiashara ktk Idara zote zilizo oza kwa Ufisadi badala ya Wafanyakazi hao kutumia wizi ili kupata Utajiri!

    ReplyDelete
  23. MHE.JOHN MAGUFULI,TUNAKUAMINIA BABA !! KAZA KAMBA ANGALAU UIKOE NCHI HATA KWA MAENDELEO YA MIUNDO MBINU, NAAMINI TANGU ULIPOTEULIWA MARA YA KWANZA KUWA WAZIRI WA WIZARA HIYO WASINGEKUHAMISHA WIZARA NAAMINI SASA HIVI NCHI YETU INGEKUWA MBALI SANA KWA NAKSHI ZA BARABARA NA MADARAJA, SISI WADAU WA UGAIBUNI TUKO NA WEWE KAKA! NA LAZIMA KUNA SIKU UTAINGOZA NCHI YETU!BIG UP DR JOHN MAGUFULI KOMBE NA MUNGU AKUBARIKI SANA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...