Home
Unlabelled
barabara ya samora avenue, Dar es salaam, enzi ya mjerumani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
i fink it was better then than it's at the moment....
ReplyDeleteenzi hizo mambo mswano - dar kulikuwa na winter na snow kama mnavyoona kwenye picha....
ReplyDeleteSpace ni muhimu sana wakati wa kujenga hata huku ughaibuni unaona miji ya miaka zaidi ya mia nafasi kati ya nyumba na nyumba wana heshimu sana siyo kijijengea hovyo kama tulivyoifanya Dar. Sehemu amabayo inatia uchungu sana ni Sinza. kuna sehemu hata gari taka au za wagonjwa haziwezi kupita. It is a shame the government has put people of Tanzania down. Upangaji wa mji na usafi wakati mwingine siyo umaskini bali ni madaraka mabovu ya watu wa ardhi na serikali kuu kufuatilia. Itakuwaje sehemu ya kuchezea watoto watu wanagawiwa viwanja kujenga? Nani anayetoa hivyo vibali?
ReplyDeleteKanisa ninaloliona mbele ni st.joseph au st. albano?
ReplyDeleteMmh yani enzi za mjerumani Dar es Salaam kulikuwa na snow! Au manjonjo ya pichaz
ReplyDelete"INDEPENDENCE AVENUE"Swafiiii kweli kweli!
ReplyDeleteNdio inafurahisha sana!
ReplyDeleteHii ndio Manhattan ya bongo, Ankal au Mdau yeyote anayefahamu je hiki ni kikapande gani kwa sasa ktk Samora Avenue?
1.Inapoanzia Clock Tower na Njia ya Stesheni?
2.Makutano ya TRA Samora Avenue na Mtaa wa Aggrey?
3.Makutano ya Morogoro Road na Samora?
4.Makutano ya Zanaki na Samora?
5.Makutano ya Mkwepu na Samora (Salamander)?
6.Mzunguko wa Aaksri na Samora/ Azikiwe ?
7.Makutano ya Ohio na Samora?
8.Makutano ya Mirambo Avenue na Samora?
Linaonekana Kanisa kubwa hili ndio lipi kwa sasa?
Ndio,,,,huu ndio Mtaa wa wajanja wa Tanzania!
ReplyDeleteKila dunia ndio hali ilivyo mfano mtaa au eneo fulani kuwa ndio kitovu cha kila kitu:
1.MAREKANI:
-Manhattan ni Mtaa na bila Manhattan na vitu kama Wallmart na NYSE hakuna New York City,na bila NYC hakuna MAREKANI!
2.UINGEREZA:
-Thames River, Greater London penye daraja na Mnara wa saa, hiyo ndio asilia na kila kitu kuhusu UINGEREZA!
3.UJERUMANI:
-Berlin (Brandenburg gate-Lango la Brandenburg) licha ya kupokwa umuhimu wake kutokana na Vita Baridi kwa kugawa kati ya Mashariki na Magharibi na kupewa hadi Frankfurt, Bonn na Cologne, hadhi na umuhimu wake Berlin ilibidi urudi baada ya Ukuta wa Berlin Kuangushwa mwaka 1989,bila Berlin inakuwa hakuna UJERUMANI!
4.TANZANIA:
-Samora Avenue, ndio moyo wa Dar Es Salaam, mipango yote yenye akili inajiri katika anga hizi kama unavyoona bila Samora hakuna Dar na bila Dar hakuna TANZANIA!
Sio kwamba maeneo mengine ktk mifano minne hapo ya nchi na miji hayana umuhimu la hasha, hapa lengo ni kutanabaisha kiini cha uendeshaji wa nchi husika!
Taswira adimu, zirushe zaidi ankal tupate kuijua bandari salama ya enzi hizo
ReplyDeletetembeatz.blogspot.com
Raha raha tupu, inafurahisha sana.
ReplyDeletekuna sanamu katikati ya barabara mmeiona wadau ?
ReplyDeleteJerumani hakuwa na mchezo kabisa katika mipango miji!
ReplyDeleteHebu angalia Mkoloni alivyo weka mitaa kwa mistari kunyooka!
Weeee wangeamrishwa wasimame mbele ya nyumba zao huyo atakaepindisha kulalekii risasi itamfyeka mwenyewe Jerumani akiachia risasi mwisho wa mstari!
Kila kitu kina uzuri wake na baya wake!
ReplyDeleteHARSH RULE/ UTAWALA WA MGANDAMIZO!
Kulingana na uzembe katika kusimamia mambo yatu mengi kama uendeshaji na mipango, Mjerumani ingewezekana tunge mwita arudi (sio kiutawala) bali katika kusimamia mambo na kufikia shabaha ya malengo.
Hapo ni Azikiwe kuangalia Picha ya askari (Azikiwe na Samora) . Lile kanisa kule ni Azania Front na mbele ni bahari ndio maana kunaonekana hakuna kitu kule mbele. Ukiangalia kwa makini utaona katikati ya roundabout kulikuwa na sanamu kama ile ya askari ila kama ya mtu kashika kiuno, siui ilikuwa sanamu ya nani? Wanaojua historia watupashe maana kama kawaida yetu waafrika documentation ni tatizo mpaka tuandikiwe na wazungu.
ReplyDeleteHii picha imepigwa toka ilikokuwa idara ya habari-maelezo ya zamani.
Mzozaji
kwetu kuzuri ndiomaana wakoloni wakaja
ReplyDeleteeheee bongo oooyeyeeeeeeeeee kumbe tuna snow.
ReplyDeleteGerman RULE/ UTAWALA wa Jeremani haukuwa na masihara!
ReplyDeleteAngalia:
-hadi barabara zimenyooka!
-hadi miti katika mistari ya barabara imenyooka!
-nyumba zimepangwa kwa mistari iliyonyooka!
-nafasi ya kutosha katikati kwa ajili ya barabara!
-kila kitu kwa utaratibu hakuna mchezo mchezo na kujuana!
Kwa mtaji huu wa usimamizi makini kama huu utategemea UFISADI kujitokeza hapo?...thubutu atakayefanaya Ufisadi ni risasi!
Acheni fix kanisa ni la St. Joseph pia shule ya forodhani ambayo tumafahamu imejengwa enzi ya njerumani inaonekana. Kuna sanamu sio ya Askari
ReplyDeleteMwelekeo sijaupata!!!
ReplyDeleteWadau mfano nimesimama upande huu wa chini wa picha kulia kuna maandishi 183A na kushoto kuna maandishi mistari miwili juu na chini.
Natazama kule kwenye Sanamu sasa huku nilikosimama kwa siku hizi ndio upande wa wapi?
Na kule mbele ndio upande gani?
Pia je ile Sanamu ya Bismin inaashiria Historia ya vita gani vita ya Mjerumani au ya Mwingereza?
Naomba mnifahamishe!!!
Tafadhali, naipenda sana Historia!
Kama hili ni Azania Front mbona kuna jengo jeupe ng'ambo ambapo hapo ni Bustani (Park) kwa sasa?
ReplyDeleteili hilo kanisa liwe ni Azania basi hii picha ilichukuliwa maeneo ya Tancot House(opposite na Life House). Kwa hiyo lile jengo jeupe linakuwa ni NEw AFrica Hotel.
KWa kifupi anayejua atuambie. Manake picha hii ni nzuri sana. Halafu inasikitisha kuona historia ya Tanganyika imefutwa kabisa. Hakuna mambo ya kuvutia yanayoandikwa kiasi kwamba hata jina Tanganyika eti halijulikana lilitoka wapi?!!!!
Tunamshukuru sana aliyeleta picha hii. Na kama zipo zingine tunaomba atuletee
Kwa maoni yangu mimi picha hii inaoyesha makutano ya Azikiwe Str na Samora Avenue hususan kwenye keep left ya Sanamu ya Bismini (Askari monument). Kanisa tunaloliona ni lile la Kilutheri (Lutheran Church) na Jengo linaloonekana kama kuungana na Kanisa hilo ni ile Hoteli ya Kaiserhof au Africa Hotel kama ilvyokuja julikana baadaye (sasa ni New Africa Hotel). Hiyo barabara yenye miti mingi kila upande inayoambaa na Hoteli na Kanisa ni Azikiwe Str. Barabara ya Samora ni hiyo inayokutana nayo. Hiyo sanamu inayoonekana hapo katikati ya makutano ya Barabara hizo mbili ni ya aliyekuwa Mtawala wa Kijerumani Otto von Bismarck (Waswahili walimwita Bismini). Waingereza walipoingia nchini waliibomoa hiyo sanamu na badala yake waliweka ile ya sasa ya Askari ikiashiria mapambano ya Vita vikuu vya I vya Dunia vya kumng'oa Mjerumani. Weupe wa barabara si wa snow ila ni mchanga kwani hakukuwa na lami wakati huo.
ReplyDeleteMWANA MZIZIMA kweli wewe ndio mwenye Mji na mletaji kwetu wa Historia nzuri kabisa, Ahsante sana kwa maelezo yako muhimu saaana, pia Mdau wa 14 hapo juu MZOZAJI ahsante kwa taarifa yako ambayo inafanana na ya MWANA MZIZIMA!
ReplyDeleteMAONI YENU NDIO MAELEZO SAHIHI KABISA KUHUSIANA NA PICHA HII.
Wakati wa mjerumani hapakuwa na samora avenue!
ReplyDelete