Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Msishangae wajameni, baada ya tambuu kupigwa marufuku sasa ugoro umechukua nafasi hasa maeneo ya kariakoo ndo chiboko

    ReplyDelete
  2. Hapo ni kuhalalisha biashara nyingine zisizo halali hakuna lolote.

    ReplyDelete
  3. umetimiza ndoto yangu, kwa muda mrefu nimekuwa natafuta kupiga picha hili tangazo, but ukiwa ndani ya daladala huwa ni shida kidogo kuipata vizuri, kila gari ya mwenge chuo kikuu ikipiga kona hapo huwa nafurahi kusoma hilo tangazo. lakini, 2 weeks ago, hilo eneo lilikuwa na maji machafu ya chooni yanatiririka, natumaidi mdau utatoa picha hiyo pia kama bado yapo.

    ReplyDelete
  4. Who knows inawezekana maneno "ugolo mkali sana" unaamisha kitu fulani miongoni mwa wahusika wa biashara ya "ugolo"

    ReplyDelete
  5. Uchafuzi wa mazingira kwa kuandika maandishi ktk ukuta wa watu.

    Pengine anauza kete za unga huyu.

    ReplyDelete
  6. Mi nilidhani ugoro ni kwa wazee tu

    ReplyDelete
  7. Ugoro walewale ni MIHADARATI TOSHA!

    PANA JAMAA MSOMALI ALIJITAHIDI KUACHA KUVUTA SIGARA LAKINI AKAZAMA KTK KUBWIA UGORO!

    BAADA YA MSOMALI KONA YA MTAA WA SWAHILI NA TANDAMTI DUKANI KARIAKOO KUUBWIA UGORO NILISHUHUDIA AKIPIGA CHAFYA HADI AKATOA UPEPO PYUUUU!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. nauza vipodozi,hereni na bangiiiiiili na bangiiiiiiiiiiiiiiili

    ReplyDelete
  9. Huu 'ugoro mkali sana' ni huu huu tunaoujua au ni kitu kingine? Anyway, biashara ni matangazo. Kuna tangazo nililoliona Dar miaka kadhaa nyuma ambalo lilinifurahisha kidogo. Lilikuwa linasomeka: ASALI SAFI YA NYUKI WADOGO WAKALI NA WANAOUMA.

    ReplyDelete
  10. Kama sikosei hapo ni Mwenge. Unapotoka kituo cha basi lazima utaliona tangazo hili.

    ReplyDelete
  11. Duh! Hivi ugoro hasa ni tumbaku au bangi?

    ReplyDelete
  12. HEJ WABONGO ACHENI MANENO YENU MIMI NI MKAZI WA STOCKHOLM SWEDEN, MATUMIZI YA UGORO NI MAKUBWA NA MATANGAZO YA UGORO NI MAKUBWA WAZUNGU WANAVUTA UGORO KAMA WAMECHANGANYIKIWA. , KWA HIO KWA NINI WASIUZE HATA KAMA NI WAUZA VIKETE SAWA SAWA TU BIASHARA BILA MATANGAZO ITAKUWAJE.? NINACHOSEMA MIMI UGORO NI ULEVI AMBAO HATA GEORG BUSH ANATUMIA SANA NA HAKOSI VIKETE VYA UGORO NENDA www.americantobaccouser.com utapata watumizi mastar wa kimarekani wanaotumia ugoro

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahaha mdau stokoloko.

      Delete
  13. UTUMWA NA UTEGEMEZI WA ULEVI:

    Hili limekuwa ni tatizo sana kwa jamii ya Dunia nzima wacha hapa Tanzania!

    Ugoro ilikuwa ni tasnia ya Wazee kwa Miongo mingi hapo nyuma, ila sasa Vijana ndio wanaongoza!

    Mbaya zaidi Ugoro huo huweka ktk vituo vya Mauzo, huku huduma za bidhaa zingine za ''Kilevi'' zikiendelea chini ya Mkeka bila watu kujua kabisaaa!

    ReplyDelete
  14. Bangiiiiiiiiiiiiii na bangiliii

    ReplyDelete
  15. Zama za ulevi kwa Kizazi Kipya, imefikia sasa Vijana zaidi ya kuubwia huo Ugoro wanavuta Sigara kali chapa ya Nyota na Safari ,zisizokuwa na vichungi!

    Mbaya zaidi wanavuta kwa staili ya Kizee ya kinyume nyume ya kuuingiza moto ndani ya mdomo!

    ReplyDelete
  16. Siyo Ugoro Tupu, pana kitu hapo.

    Angalia: "Ugoro Mkali sana"

    Ni kweli biashara matangazo, na ndiyo maana kuna maneno ya mkazo ambayo yanaashiria biashara mchanganyiko.

    Mkifanya uchunguzi kwa makini mtapata jawabu. Na msishangae akahama sehemu hiyo.

    ReplyDelete
  17. Huyu jamaa wa swenden kanichefua, kwa kuwa wazungu wanakula ugoro basi ni halali??. muone huyu na u** wake.

    ReplyDelete
  18. HAAHAHAHAH,

    Mnanicheksha na mnanikumbusha mbali sana!

    Mwaka 1988 nikiwa nasoma Sekondari nilianza kujifunza kuvuta sigara wakati kaka yangu ninaemfuata (Yeye mkubwa) alikuwa ni mvutaji mzuri hadi ''Sigara Kubwa''.

    Sasa tulikuwa na utaratibu wa kuvuta sigara SPOTI usiku tukiwa tunaanza kulala vitandani, kabla tulikuwa na utaratibu wa kuandaa Paketi ya sigara kadhaa pembeni ya Kabati za vitanda vyetu.

    Sasa uvutaji ulianza kunikera nikaancha isipokuwa kaka yangu alikuwa anaendelea, nilijaribu kumkataza lakini akawa mgumu, NIKATUMIA MBINU YA KUANDAA PAKETI YA SIGARA ZA SPOTI LAKINI NDANI NIKAWEKA ''SAFARI'' SIGARA KALI!

    NILIJIFANYA NIMELALA FOFOFO, KAKA ALIPORUDI USIKU ALIRUKIA PAKETI AKATOA SIGARA MOJA AKAPIGA KIBERITI KUWASHA ,,DUHHH ALIKOHOWA HADI AKAANGUKA CHINI,NIKASHINDWA KUSTAHIMILI NIKACHEKA SANA LAKINI ILISAIDIA NAYE AKAACHA SIGARA!

    ReplyDelete
  19. Hili ni balaa kubwa kabisa,,,Vijana wa umri mdogo kabisa kutumia ulevi!

    Ndio maana watoto wadogo kabisa wanazeeka haraka kwa ajili ya ulevi, unakuta kijana wa miaka 19 anakuwa na uso na mwili mkavu kama Mzee wa miaka 91 hivi!

    Haieleweki wanapoteza mawazo gani?,,,wamechanganyikiwa na nini?

    Hivi ni kweli kuwa Dawa ya Matatizo ni kulewa badala ya kutatua Matatizo yenyewe?

    Imefikia kipindi sasa Vijana WAVULANA kwa WASICHANA ndio watumiaji wakubwa wa Vilevi kuliko watu wa Umri Mkubwa na Wazee!

    ReplyDelete
  20. Huu ni ugoro kweli?

    ReplyDelete
  21. Ni jambo lisilopendeza kabisa Vijana wadogo kabisa kutumia starehe ya Wazee!

    Hata hivyo ni wazi kuwa hii kitu Ugoro ina madhara makubwa kiafya hata kwa Wazee ingawa wamekula chumvi nyingi na muda wao wa maisha upo ukingoni,,,na kuwakataza Wazee wetu inakuwa ni ngumu, ni vile huwezi kirahisi kumkosoa Mkubwa!

    ReplyDelete
  22. Binadamu bwana sasa mnashangaa nini ugoro au? Huyo kaandika hapo kwa maana yake nasi ugoro mnaoujuwa nyei huwo ni ugoro wa kunyongwa kiganjani. Au mnataka aseme kuwa bagi ili muuletee difenda.

    ReplyDelete
  23. Wewe...Binadamu bwana sasa mnashangaa nini ugoro au?

    Hiyo Ugoro wa kweli kweli, Hiyo ya kunyonga Kiganjani zote ni Walewale tu NI VITU HAVIFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU BASI TU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...