Lile sakata la Madaktari na Serikali Limefikia Madaktari Kuamua Uamuzi Mgumu wa Kuamua Kugoma rasmi kuanzia Kesho tarehe 24/01/2012.
Uamuzi huu metolewa leo katika mfulilizo wa Mikutano waliyoianza toka jumatano ya wiki iliyopita (18/01/2012) katika kujaribu kutafuta suluhu ya matatizo yao na ya Sekta ya Afya kwa Ujumla,Juhudi hizo hazikuzaa matunda kutoka kwa Serikali kuanzia ngazi ya Wizara ya Afya mpaka ofisi ya Waziri Mkuu ambapo kutozaa matunda.
Madaktari/watumishi wa afya hao wana madai kadhaa ikiwemo
*Kuboresha Huduma za Afya nchini (hospitali na vitanda kwa kila mgonjwa inawezekana)
*Maslahi Duni kwa watumishi wa sekta ya afya
*Malipo kwa kazi za ziada kwani Madktari wanalipwa shilingi 10,000/= kwa kukesha na kufanya kazi masaa 36 tofauti na taratibu za serikali ambapo ilitakiwa walipwe shilingi 40,000(half pediem) kama taratibu za serikali zinavyoonesha lakini viongozi wa Wizara hasa Mama Blandina Nyoni wamekuwa wakikwamisha hili.
*Haki ya kupewa nyumba au posho ya Nyumbai kama muongozo wa utumishi wa umma wa serikali ya Tanzania unavyoelekeza ule wa mwka 1994 na wa mwaka 2009..
*Kulipwa posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi(Risk allowance)
*Lingine ni Kuondolewa kwa Katibu mkuu wa wizara ya afya Bi.Blandina Nyoni ambaye anaonekana kuwa ni kikwazo katika juhudi za msingi katika kuboresha sekta ya afya Tanzania.
*Bi Blandina Nyoni anatuhumiwa kutoa kauli ya kejeli kwa watumishi wa afya kuwa anamshukuru baba yake kwa kumkataza kusomea mambo ya afya kwani sekta ya ya afya haifai na ndio maana licha ya kufaulu masomo ya sayansi baba yake alimshauri asomee uhasibu.
Madaktari/watumishi wa afya hao wana madai kadhaa ikiwemo
*Kuboresha Huduma za Afya nchini (hospitali na vitanda kwa kila mgonjwa inawezekana)
*Maslahi Duni kwa watumishi wa sekta ya afya
*Malipo kwa kazi za ziada kwani Madktari wanalipwa shilingi 10,000/= kwa kukesha na kufanya kazi masaa 36 tofauti na taratibu za serikali ambapo ilitakiwa walipwe shilingi 40,000(half pediem) kama taratibu za serikali zinavyoonesha lakini viongozi wa Wizara hasa Mama Blandina Nyoni wamekuwa wakikwamisha hili.
*Haki ya kupewa nyumba au posho ya Nyumbai kama muongozo wa utumishi wa umma wa serikali ya Tanzania unavyoelekeza ule wa mwka 1994 na wa mwaka 2009..
*Kulipwa posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi(Risk allowance)
*Lingine ni Kuondolewa kwa Katibu mkuu wa wizara ya afya Bi.Blandina Nyoni ambaye anaonekana kuwa ni kikwazo katika juhudi za msingi katika kuboresha sekta ya afya Tanzania.
*Bi Blandina Nyoni anatuhumiwa kutoa kauli ya kejeli kwa watumishi wa afya kuwa anamshukuru baba yake kwa kumkataza kusomea mambo ya afya kwani sekta ya ya afya haifai na ndio maana licha ya kufaulu masomo ya sayansi baba yake alimshauri asomee uhasibu.
Maamuzi hayo magumu yamefikiwa katika Mkutano wa leo uliofanyika Don Bosco Upanga DSM ikiwa ni mwendelezo wa Mikutano isiyokoma iliyoanza Toka jumatano ya Wiki iliyopita.
Kama malipo kidogo njooni ughaibuni mshahara utakutosha kufanya kila ulitakalo.
ReplyDeleteMgomo wa madaktari ni matokeo ya serikali isiyo sikivu kwa wananchi wake. Hongereni madaktari, ni haki yenu kugoma hadi mtakapo sikilizwa. Bravo Tools Down!
ReplyDeleteTuliwaambia wananchi ikataeni ccm mkapewa kanga na sukari wananchi wakifa hospitalini ni nyinyi wenyewe. Sisi huku poa unatibiwa kwanza kudaiana baadae. Poleni.
ReplyDeleteTuna hamu kubwa kuwatumikia wananchi wenzetu, sababu tumesomeshwa kupitia kodi zao. Isipokuwa serikali yetu inatuangusha kutumika ipasavyo.
ReplyDeletewapiganapo mafahali wawili, ni nyasi ndio ziumiazo......., nawaonea huruma wagonjwa.
ReplyDeleteMadaktari nao eti wanadai 'POSHO' kama wabunge ,kwa hili siwaungi mkono hata kidogo..walipa kodi tunataka POSHO zifutwe kabisa....! waweke tools down na warudishe kodi zetu tulizowasomeshea mara moja,tutaenda kwa Babu tukiumwa!
ReplyDeleteHii ndio faida yakweka machizi serikalini..km kweli huyu mama ametoa hii kauli hebu jiulizeni yeye haumwi?bcoz kwa kauli yake hio amewatukana sio tu madaktari wa bongo bali dunia nzima tena nafani nyengine za sayansi.
ReplyDeleteHivi mtu kama huyo anapaswa kupewa hata uenyekiti wa mtaa?
Lkn kwa namna wabongo tulivyokua vichwa maji mtaona comment hapa zenye kumtukuza huyo mama na kuwalaumu madaktari..sasa sijui hawa watu wanamatatizo gani..
Ooh..sio macho yaliyopofuka bali ni mioyoambayo iko vifuani ndio iliyopofuka!
Hii taarifa yenye madai makali yanayoelekezwa mwa mtu binafsi (Nyoni) IMETOLEWA NA NANI? Imesainiwa na nani? Michuzi usitoe taarifa zisizo na kichwa wala mguu la sivyo wewe ndio utakuwa MCHAFUA HALI YA HEWA hatari zaidi
ReplyDeleteHONGERA SANA MADAKTARI HUO UWE NI MWANZO WA KUONYESHA KAMA INAWEZEKANA, WAO WAMEKAA KUJIONGEZEA POSHO KILA SIKU NA WALALAHOI HATA KITANDA MTU AKILAZWA HAKUNA WALA CHAKULA NA HOSPITALI HATA DAWA HAWANA. WATANZANIA TUMECHOKA WASHEM
ReplyDeleteNZI WAKUBWA HAO VIONGOZI WAKIUGUA WANAPELEKWA INDIA KUTIBIWA NA NAULI YA SEREKALI, ACHA TUFE KWANZA NDIO MAENDELEO YATAKUWEPO NA HAKI ZA BINADAMU
kwani mbali na umaskini tuliyonao,eti bado kuna mtu adhubutu kusema maneno ya ovyo kuwa kuwa sekta ya afya haifai ya huyu kiumbe ,anabahati yupo tz,kama ni nchi za wenzetu wala hakuna hilo ni wa kurusha kama mfuko wa uchafu,anatakiwa aondoke sioni sababu ya kubeba watu kama hao ila wajui siku moja isiyo na jina atakumbuka huo mdomo wake mchafu
ReplyDeletekweli serikali hii duh!! watu nyeti kama madaktari bado haiwasikilizi.Madaktari ni watu wamuhimu sana katika jamii.. sasa huo mgomo wao utaendana na baadhi ya wagonjwa kufariki .. mbona hili ni janga jamani.. chondechonde kikwete fanya jambo mapema..
ReplyDeletewe annony wa kwanza bahati yako sana ankal amekataza, unabahati sana japo umejeruhi hisia zangu.
ReplyDeleteBinafsi naumizwa sana na uamuzi huu wa madaktari ila wanamadai ya msingi na nipo radhi kupigwa mabomu nikiandamana bega kwa bega kudai maslahi yao, tena si kwamba wanadai yaboreshwe bali wanachodai serikali itimize makubaliano yake.
Tatizo wenzetu wanatibiwa apollo ndio maana hawaoni umuhimu wa madaktari wetu, ila sisi wapiga kura ndio tunaojua madhara ya mvutano huu unaosababishwa na serikali ya kipumbavu kama hii inayokumbatia wageni na kutudharau sisi.
....Walaaniwe walioiweka madarakani serikali hii kwa maana wameshindwa kuonesha uzalendo , uadilifu,uwajibikaji, utiifu,na umakini.....
ETI KAZIYA KUJITOLEAA..WAO WANALALA KWENYE MAHEKARU..
ReplyDeleteInasikitisha....
ReplyDeleteIngekuwa huku ..(ng'ambo), mlango wa kutokea kwa Nyoni na Waziri ungeshafunguliwa na kufungwa zamani! Tutalindana mpaka lini?
Hiyo kauli ya huyo mama siyo tu ni kejeli bali ni matusi .. au kwa kuwa yeye akiugua anaenda kutibiwa Appolo India?
Duh kama kweli huyu mama alinukuliwa akisema hivyo imekula kwake
ReplyDeletesafi sana madakitari nawaunga hadi miguu, iweje mle nondo ngumu ya udakitari halafu mje mfanye kazi katika mazingira magumu kwa ajili ya wababe wachache? ilhali wengine wamekwepa umande lakini wapo huko bungeni wanapokea posho kwa siku laki mbili wakati nyie mnakesha na wagonjwa ati mnalipwa elfu 10,000. huu ni uzandiki wa hali ya juu hadi kieleweke, kila siku nchi masikini, inatia hasira sana mama mjazito kushare godoro sakafuni halafu wao wanajinunulia mishangingi na kujipendelea na hela ndeefu hii haikubaliki hata kidogo ati viongozi wa nchi ndo mnyananyapae wananchi namna hii?
ReplyDeletemnadai serikali haina hela wakati nyie maisha yenu mnaishi kama vile mko peponi? serikali tunaomba saaaaaana muwasikilize madakitari na mtekeleze maombi yao mara moja, najua leo wagonjwa watakuwa na hali ngumu, lakini imebidi njia hii itumike, kwa vile serikali ni wababe sana mnapenda kulazimisha mambo leo pelekeni ffu na magari yenu ya maji ya kuwasha, manake hiyo ndo njia yenu ya mkato badala ya kukaa mezani kutatua matatizo nyie mnatumia mabavu.
michuzi tafadahli naomba usibane hii huu ni ukweli na uwazi!
Tanzania ni nchi yetu lakini tukiri tu kwamba ni nchi ya kijinga ambayo haijawahi kutokea duniani. Tunashindwa kuwalipa madaktari wakati tuna kila aina ya madini. Kwenye dhahabu kwa mwaka wawekezaji wamepata dola bilioni 3.6 na sisi tumeambulia dola milioni 78. Ujinga gani tena zaidi ya huu? Wacha madaktari wagome. Mhasibu anapewa kuongoza wizara ya afya baada ya kuvuruga maliasili na hazina, na kila kitu kinajulikana.
ReplyDeletewewe mdau wa pili vipi waje ugaibuni ndugu zako watatibiwa na nani/ tumia akili kabla hujaongea.
ReplyDeleteKwanza mlichelewa.hii nchi ya kina rizione sisi tumepangishwa tu! Erick
ReplyDeleteDUH YAANI KAZI KWELIKWELI .SASA MAREKANI MFAGIAJI KIMA CHA CHINI DOLLAR 8 KWA SAA . UKIFAGIA MASAA 10 UNA DOLLAR 80 KWA SIKU HUU NI MSHAHARA WA MWEZI WA MTANZANIA
ReplyDeleteDEGREE ZA TANZANIA HAZITAMBULIKI USA . ITABID MUANZE UPYA
ReplyDeletemama nyoni lako hilo.lazima ujivue gamba.dharau zimekuponza wote tungekuwa wahasibu nani angekutibu!acha kashfa.
ReplyDeleteMSHAHARA NA MARUPURUPU YA WABUNGE,,,(((JUU!))),,,(WASAFISHA VINYWA) NA WENGI WAO AMBAO HULALA VIKAONI TUNAWAONA HADI KATIKA LUNINGA!.
ReplyDeleteMASLAHI NA HALI YA KIKAZI (WORKING CONDITIONS) YA MADAKITARI,,,(((CHINI!))),,,WANAOOKOA VIFO VYA WANANCHI NA AFYA ZAO NA HUKU WAKIWAPA MSAADA HAO HAO WAHESHIMIWA WAKIZIDIWA NA VISUKARI VYAO NA MASHINIKIZO YA DAMU!.
WANASIASA NI KUNDI MOJA LINALETA MATATIZO MAKUBWA KATIKA JAMII NYINGI DUNIANI, KWA MIPANGO YAO ISIYOKUWA NA AKILI!
TATIZO ZAIDI LINAKUJA WANAPOPEWA MWANYA WA KUINGILIA MWENENDO WA UTENDAJI WA SERIKALI, ANGALIA MAANDAMANO HATA KATIKA NCHI ZILIZOENDELEA KAMA MAREKANI NA UINGEREZA HAYA YANAJIRI SIO TU HUKU KWETU MANYASINI!
HAYA NI MATOKEO YA SIASA ZAIDI KULIKO SAYANSI!
KWA MTAJI HUU TUTAFIKA?
Mbona madaktari wenyewe ni wachache! yaani serikali inashindwa kuwahudumia kweli? Tunao wabunge karibu 400 wakuchaguliwa na kuteuliwa! Nafikiri katika katiba mpya hakuna wabunge wa vitu maalum, hii inaonekana ni kupeana ulaji tu na kuifilisi serikali, bora hiyo pesa walipwe madaktari kwani wabunge hao wanalipwa mabilioni ya pesa kwa mwaka na hawana mchango wowote bungeni kwani kuna wengine hawajawahi kuuliza swali au kuchangia hoja yoyote kwa kipindi chote cha miaka 5 bungeni!
ReplyDeleteNingekuwa na mamlaka, uamuzi ambao ningefanya mara moja ni kumuondoa katibu mkuu wa wizara, nadhani baada ya hilo madaktari wangelainika na kubadili maamuzi yao. Record ya Blandina Nyoni ktk utumishi wa umma inaonesha ni ya mapambano na mivutano kila anakokwenda.
ReplyDeleteHakika madakitari mnastahili kulipwa hayo yote ambayo hamjatimiziwa. Naiheshimu sana kazi yenu. Nikazi moja ngumu sana lakini bado hamkati tamaa. Nimacho wasii ndugu zangu msigome kwani sisi masikini tusio na uweza kwenda hospitari kama za Agakani, Regency, Hindumandal,TMJ na nyikinginezo kama hizo. Kwakweli tutaendelea kupoteza maisha yetu hasa kina mama wajawazito na watoto na wazee. kama mnavyo fahamu hari kwa sasa ni ngumu sana kwa wananchi natumaini hata serikalini.Nawaombeni muwe wavumilivu mpaka hapo serikali itakapoweza kuwasaidia kwani hata serikali inazidiwa mambo ni mengi kuna ndugu zenu walimu nao wanamadai lukuki. Mungu awapeni nguvu ya kufanya kazi.
ReplyDeleteni mimi Raia mwema Mtanzania
nimesikitishwa sana maana wanaoumia ni wananchi wenye kipato kidogo.......mbaya zaidi kauli ya kejeli jamani.........
ReplyDeleteHIVI SERIKALI INASHINDWA NINI KUONGEA NA MADAKTARI NA KUMALIZA MATATIZO YAO??????? MSIWEKE SIASA KILA MAHALI. NGOMENI MPAKA KIELEWEKE
ReplyDeleteMhh! hii ya Blandika kali, anamshukuru baba yake kwa kumshauri kusomea uhasibu badala ya udaktari, hivi akiugua anatibiwa na nani, hata huyo baba yake nadhani kauli hii ni ya kudhalilisha fani za wengine. Kwa kweli hili amepotoka. Haya wote tukiwa wahasibu nini kitatokea? Mungu amsamehe tu. Hajui hiyo wizara anayofanyia kazi ipo hapo kwa sababu za afya na hao watoa huduma wa afya kama madaktari bila wao hata yeye asingekuwa hapo.
ReplyDeleteIngekuwa nchi za wenzetu kauli hii ingemfanya alazimike kujiuzulu.
Serikali imeshindwa kazi hii jamani, hakuna kinachoenda jamani. Umeme bei juu, maji shida, maisha magumu haina mfano, migomo kila kukicha...
ReplyDeleteSerikali mnacheza na moto.JK ingilia kati pliizi.Wewe unayewashauri waje ughaibuni hauna ndugu zako TZ au huwa hawaugui?.Hata mimi nipo ya nje ya nchi lakini nafikiria watakaoumia kwenye hii 'Saga' ni watu ambao hawana hatia.
ReplyDeleteDavid V
Kwakweli ni AIBU kwa serikali yetu hii. Elfu 10 kwa mtu anayekesha kuangalia afya yako,ya ndugu yako, ya jirani yako......?!?! Hakuna usawa kabisa,ukizingatia kuna watu wanapata posho kubwa sana kwa kitu ambacho sio significant kama utoaji wa huduma wa afya hapa nchini.
ReplyDeleteBusara isipotumika hapa matokeo yake ni maumivu kwa wananchi.Huyo katibu mkuu wa wizara ya afya,anawasemea mbovu watumishi anaotakiwa kuwacancell na kuwapa tumaini.Hivi nchi hii haina criteria za kupima efficiency ya kiongozi wa umma.Yeye Blandina efficiency yake inapimwa kwa uboreshaji wa huduma ya afya,ambayo inatakiwa ifanywe na madaktari ambao yeye ndiye anawabeza,anawadharau na kuwakatisha tamaa.Hawa ndio viongozi wetu.
ReplyDeleteNinawaunga mkono Madaktari kwani hakika wamejitahidi lakini Serikali imewaona hawafai na imewatelekeza. Ninaamini kabisa kama watagoma kwa ujumla wao serikali itawapigia magoti na kilio chao kitasikilizwa.
ReplyDeleteSekta ya afya na wahudumu wake wamesahaulika kabisa. Vipaumbele vinawekwa katika mambo yaliyo ya kisiasa badala ya kuweka katika mambo yanayowaathiri wanaanchi moja kwa moja. Mambo ya kusema Udaktari/Unesi/Ualimu ni wito yamepitwa na wakati! Ni Daktari/Nurse/mwalimu yupi ambaye haiitaji kusomesha mtoto wake katika shule nzuri, ni nani ambaye hatataka kujijengea nyumba nzuri, ni nani kati ya hao ambaye hatataka kuwa na uhakika wa maisha yake mara baada ya kustaafu ajira yake? Hii itawezekana tu kama watapata maslahi mazuri na stahiki zao za kazi. Kwahiyo inachotaka Serikali ni kuona kada hizi zikiishi maisha ya shida kwa vile kazi zao ni za wito na keli ya Taifa iliwe na wngine hususani wanasiasa na wanaowazunguka?
Inasikitisha kuona Serikali inawatisha watoto wake (Madaktari walio ktk mafunzo ya vitendo)kwa kudai pesa zao za kujikimu! Hii inasikitisha mno tena mno na haikubaliki.
Kwa hakika ninawaunga mkono Madaktari kwani ninaamini bila ya mgomo hahuna kitakachobadilika. Igeni mfano wa wenzenu wa Kenya... Pamoja.
Mi nlikuwa nashangaa mnasubiri nini muda wote huo.
ReplyDeleteTuko pamoja na tunathamini michango yenu madaktari. Hizo kauli za kejeli za huyo mama ni zake, sisi watanzania (wa kawaida) tunatambua umuhimu na mchango wenu.
Pamoja sana
nyinyi mkigoma nasisi tukigoma hivyo vibajaj vyenu mtapark majumbani mwenu au mtalala kwa usalama??? Taifa litajengwa na wenye moyo bana tupigeni kazi tusubiri uchaguzi then tutoe hukumu vilivyo
ReplyDeleteWewe anony Tue Jan 24, 11:58:00 AM 2012 wewe ras Makunja nini?
ReplyDeleteHakuna cha 2015,gomeni na nyie.ngedere wee
Huyu mama anayekejeli taaluma ya tiba analindwa na nani? Tanzania ina wasomi wengi tu kwa nini asondoklewe na akawekwa mtu anayefuata taratibu. Kama waraka wa serikali unasema madaktari wanastahili kulipwa posho ya kufanya kazi katika mazingita hatarishi yeye anagoma ni nani? Aondolewe kwa sababu yeye atapelekwa India kwa hiyo wengine wacha wafe tu.
ReplyDeleteSikutegemea kama huyu mama angewatukana mpaka mabosi wake (Mwawaziri ambao ni wataalamu wa afya). Kwa hili mbali na kuonyesha kiburi amemtukanisha baba yake na kuwafanya wahasibu waonekane hamnazo kiasi hiki. Kwa hiyo dili kama zile za mhasibu wa Bodi ya Mikopo za kupiga millioni 90 kwake ndo shule na taaluma yenye heshima. Uwi kaaazi kweli kweli.
ReplyDeleteUjanja ni kusomea Stahili rahisi na za kufikia Malengo kwa njia ya mkato na kuingia katika Siasa!
ReplyDeleteBlandina Nyoni ni Kizazi cha Wanasiasa Dhalimu ambao sifa yao kubwa ni kejeli kwa FANI ZINGINE!
Tatizo viongozi wetu wa afrika, sana bongo, wanaujasiri wa kuropoka lakini busara hawana. Ukianza na huyu mama, atasamaje maneno kama hayo?(kama kweli amesema)
ReplyDeleteHapo Ndina ni mhasibu lakini roho mbaya na bora alikuwa mhasibu maana angekuwa daktari angechoma watu sindano za sumu kwa roho yake mbayaaaaaaaaaaa!
ReplyDeleteFUNDISHO KWA MADAKTARI: Bwana Yesu atakuwa daktari badala yao, acha wasuse, hijapokuwa bado alikuwa daktari lakini kwa sasa anashuka na nguvu ya pekee, kwani wagonjwa wote watapokea uponyaji na hapatakuwa na magonjwa tena duniani kote, watakula jeuri yao.
ReplyDeleteYaani mimi nilikuwa nawashangaa sana madaktari. Mpaka mliniudhi kwa kuchelewesha mgomo. Huu mgomo ilitakiwa muutangaze toka Jumatano iliyopita. Chelewa chelewa huumiza matumbo! Time will tell, anyway! This is the right time for You to strike hadi serikali itambuwe umuhimu wenu.
ReplyDeleteIngawa wananchi tutakufa sana katika kipindi hiki but we hope the outcome of our deaths will be betterment of your salaries, allowances and health services!
Keep it up guys!
HEEEEEEE MBONA TOPIC HII TAMU JAMAN KWA KWELI HII NCHI IMEOZAAAA JAMAN DAKTARI ANATAKIWA KULIPWA HELA NZURI SANAAAAAA MAANA BILA WAO TUNGEKUFA TUISHE WOTE,NYIE VIONGOZI MBONA MNAPIGANIA MUONGEZWE POSHO?????? MADAKTARI MNAWADHARAU ACHENI KABISA GOMENI NAMI NIPO TAYARI KUANDAMANA NAO MMEZIDI SERIKALI KAZI KULA KODI ZETU,MKIUMWA MNAENDA NJE YA NCHI MNA AKILI KWELI NYIE, CCM HAIFAI WATU MNADANGANYWA NA KANGA,TSHIRT NA PESA KISA MCHAGUE CCM IMEKULA KWENU NYIE ENDELEENI KUWAPA KURA TUU,MADAKTARI GOMENIIIIIIIII WAWAPE HAKI YENU WAALIMU WENYEWE MMEWARUSHA,JUZI NIMESIKIA KUWA KUNA WAALIMU WALIOKUFAGA MAJINA YAO HAYAJAFUTWA CHA AJABU KUNA WATU HUMO SERIKALINI WANAKULAJE MISHAHARA YA WAALIMU WALIOKUFA WANASEMA WAPO HAI KUMBE HELA ZINAINGIA KATIKA AKAUNTI ZAO MAKUBWA HAYA TZ PUUUUU, HII NCHI ICHOMWE TUHAME
ReplyDeleteAcheni kelele nyinyi madaktari wa kibongo. Kama kweli ni madaktari wagonjwa wasingekuwa wakipelekwa India kutibiwa. Kuna yule daktari mkuu wa Ocean Road pale, anadanganya wangonjwa wende hospitali yake iliyoko Mwenge watapona kumbe anawaibia kwa kujua kuwa hawezi kuwatibu. Kama wewe ni daktari omba visa uje UK hapa kutibu uone.
ReplyDeleteKatibu mkuu anasubiri nini kujiuzulu au mpaka apigwe mawe pamoja na wenzake; W. Ngeleja, Dk. Mponda, D. Mtasiwa na Lucy Nkya?
ReplyDeleteMboooooooooooniiiiiiiiiii
ReplyDeletemadaktari wakigoma tusikubali hadi B Nyoni aachie ngazi. Dawa ni kuandamana mpaka kieleweke.
ReplyDeleteGomeni tu kwani watakaoadhirika na mgomo wenu si ndugu na jamaa zenu ambao walijitoa mhanga kuwasomesha kwa shida na sasa mmeamua kuwalipa fadhila zenu kwa kuwagomea!
ReplyDeleteHii ni vita ya ukombozi katika fani ya afya. Pull up ur socks Drs! Saa ya ukombozi ni sasa.
ReplyDeleteHii ni nchi gani lakini? Viongozi wana ufinyu wa fikra sana kiasi cha kutuogofya wengine kama kweli tutafika mahali tujikomboe kiuchumi. Yaani ni nchi gani uchaguzi ukiisha badala ya kuwahudumia wananchi wanaanza maandalizi ya uchaguzi wa miaka mitano ijayo? Na bila aibu haya malumbano yao yanarushwa kwenye vipindi vinavyoonekana kimataifa! Crazzzzzzz.........
ReplyDeleteNdo maana wanasahau kufanya mema kwa wananchi KWANI KWA ULIMBUKENI WA WAPIGA KURA WENGI HAWAHITAJI HATA HUDUMA NZURI BALI WANAHITAJI VIHELA VYA RUSHWA ZA UCHAGUZI. Hivyo hawa watu wanavyofanya ni kuhakikisha wanapata mtaji wa kutosha kushinda uchaguzi ujao kwani mtaji wao si matendo mazuri bali rushwa. Kwa hiyo haya yanayotokea na taabu zote tutakazopata kutokana na migomo ya watendaji wetu tumeyatengeneza wenyewe na tunastahili hizi tabu zote. Cha msingi wanaowapa kura hawa jamaa kwa kudanganywa na Khanga, pilau ni vielfu kumi ni hao hao wa tabaka la chini ambao hutegemea hizo hospitali kuliko wale waelewa wanaotaka mabadiliko. Ni wakati mzuri wa wao kuacha kulalamika kwani walishauza haki zao kwa wanasiasa.
Madaktari nawaunga mkono na nafikiri si muda mrefu makundi mengine yatafuata kwenye migomo na hii ni kutokana na kiburi cha wanasiasa HASA WABUNGE ukizingatia ubinafsi wao jinsi walivyojiongezea poasho kama wao wanaishi kwenye kisiwa ambapo hali ya maisha ni ngumu tofauti na watu wengine!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
kwa kweli ni muda muhimu kuwasikiza madakatari na matatizo wanayo yazungumzia na kuwa na muafaka kwani kweli nchi iko pabaya kipesa ila hawa hawajasema hawayakubali bali wahahitaji kusikizwa; pili swala la kuiuka mikataba yao ya kazi eti kwasababu ni waajiriwa wa serikalini walio na wito kwenye fani sio sahihi; mwisho hawa ni binaadamu wenye mahitaji ya kimsingi kutowalipa pesa zao kila mwezi zilizokubalika kimsingi ni kuwadhalilisha. Kwa nini muwanyanyase sio tu madaktari watendaji wote wa serikali huku kunamatatizo mengi ambayo yamewekwa bayana kuhusu matumizi yasio stahili au rasmi serikalini? kuna shutma nyingi za ubadirifu na hii ya kupeleka wagonjwa india kwa vibendera kwa watendaji ndio kuu tuboreshe huduma kila mtua apate kilichopo kwa usawa sio ilivyo sasa (tunamkumbuka babu nyerere sana kwa hili). Tutafika kama tukibadilika! wengi bado tuna imani
ReplyDeleteAnony Tue Jan 24, 11:58:00 AM 2012, kavunje masaki mwisho kwenye uzio wa walio navyo; usitishe wenzio hapa
ReplyDeleteMon Jan 23, 10:34:00 PM 2012: daktari hufanya kazi zaidi ya masaa ya kwaida; kufanya kazi zaidi ya masaa hayo hulipiwa overtime. Issue ni kiwango sio wanachosema hapa. Tuliza boli!
ReplyDeleteGomeni kabisa madaktari! huku ulaya huduma ya afya inapewa kipau mbele kwani hata hao mahasibu kama hafya zao mbaya hayo mahesabu watayafanyaje! mna haki zote za kupewa mshahala mkubwa. Maisha ya madaktari wetu ni duni wakati ulaya ni moja ya career inayopeta. GOMENI!
ReplyDeletemadaktari big-up, nawaunga mkono, duh zamu ya kukaa hospitali na wagonjwa 36hrs unalipwa 10,000?-!!!! tofauti na serikali yenyewe ilivyoji-commit... haitoshi hata msosi kwa masaa hayo ya kukaa hosp...huu ni ufisadi kwa afya za wa-tz
ReplyDeleteNimependa mmejipanga kwamba huduma za dharura uzazi, emergency operation zinaendelea
Moderator hamna updates za hii habari?
ReplyDeleteKatika Dunia nzima ni Tanzania pekee nchi inayotweza TAALUMA na kuinyanyua SIASA bila hoja ya maana!
ReplyDeleteAh majitu ya Siasa Tanzania hakuna yanacho fanya lakini mgao wa fedha wanajipangia mkubwa sana!
Ni akili gani na mahesabu ya Kabila gani kumlipa Mbunge Shs. 200,000/= kwa siku na kumlipa Daktari Shs. 10,000/= kwa siku?