Msanii wa Muziki wa Dansi nchini,Charles Gabriel a.k.a Charles Baba akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumzia nia yake wa kujitoa rasmi katika Bendi yake ya awali ya African Stars (Twanga Pepeta) kwenye mgahawa wa Hadee's uliopo katikati ya Jiji.Charles Baba pamoja na kutangaza nia yake hiyo,pia amemtangaza Meneja wake Mpya,Bw. Bernard Msekwa ambaye atasimamia shughuli zake zote za Kimuziki ikiwa ni pamoja na kuingia mikatana na Bendi yeyote itakayomuhitaji.
Meneja Mpya wa Msanii wa Muziki wa Dansi nchini,Charles Baba ,Bw. Bernard Msekwa akisisitiza Jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na msanii wake huyo leo kwenye mgahawa wa Hadd's uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Waandishi wa habari waliofika kumsikiliza Msanii huyo pamoja na Meneja wake wakisikiliza kwa makini.
Yaani bongo ukitaka upaishwe hewani kwa ghafla, tafuta msanii yoyote na utangaze wewe ni meneja wake.. Tambararee..!!
ReplyDeleteCharles Gabriel aka Baba ni mwanamuziki mzuri sana hadhi ya kina Choki na anastahili kuwa na bendi yake mwenyewe. Kaza buti dogo onyesha kipaji chako we will support you ila usipige fleva itakulostisha. Kama utaweza mchukue Barnaba kwenye bendi yako, yule dogo anaimba ila anaharibu sauti yake kuimba nyimbo ama muziki usioendana na sauti yake. Shughulikia hili suala.
ReplyDeleteCharles utajuta kilicho kutoa Twanga huyo sio!!!
ReplyDeleteSijui Twanga Pepeta kuna nini, mtu akiondo huwa anarudigi mwenyewe tu..kuna wakati choki aliondoka akarudi hata sasa hasikiki, Kocha wa dunia naye alihangaikaa baadae karudi.
ReplyDeleteTWANGA!!!!! KUNANI KULEEEE!!!MBONA KILA MSANII ANATIMKA!!!!!!!
ReplyDeleteUmejimaliza mwenyewe, unatoka Twanga!!!Waulize wenzio mapacha watatu wako wapi sasa?
ReplyDeleteaende huko hana lolote, meneja bongo!
ReplyDeleteCharles hongera kwa uamuzi wako,usitishwe na mashabiki uchwara,ukiwa mwoga ktk kutafuta maisha utakufa maskini,Ona wenzio akina Chokky,Mapacha watatu nk.wanaenedelea vizuri,wewe haukuzaliwa Twanga,pia kwa wasanii wengine inabidi mtafute mabadiliko na maendeleo ya maisha yenu na siyo sifa,Big up Charles.
ReplyDeleteChaz umetisha ila huyo manager chaka ni mzee wa mjini ila big up kaka
ReplyDeletenenda kaongee na rafiki zako kina jose mara na chokoraa, na kalala kama mlivyopanga hapo awali iwe mapacha original mtatishaaaa balaaa!!! NI wakati wa kuondoatofauti na kufanya kazi na kuleta burudani holla..!!
ReplyDeleteHongera dogo ni maamuzi mazuri, katika kila penye maendeleo watu walithubutu ndio wakafanikiwa, naamini wewe umeamua kuthubutu basi utafanikiwa usiziogope changamoto zozote wadau na washabiki wanazokupa ww zichukulie hizo zote ni changamoto kwako za maendeleo yako. KAPINGAZ Blog.
ReplyDeleteTwanga inaonekana ni Chuo cha kuwatengeneza wanamuziki mpaka wakaweza kuwika na kuuzika. Huyu Chalz Baba inasemekana kajiunga na Bendi ya Mashujaa inayomilikiwa na Sakina Trans na mumewe Maisha ambao ni marafiki wa karibu wa Asha Baraka kwa kitita cha Shs milioni 15 na marupurupu mengine. Sasa hapa sijui kama kutokana na mikataba ilivyo kama Twanga pepeta kama bendi wamelipwa chochote.
ReplyDeleteHUYO ANAENDA MASHUJAA BAND WANATUZUGA TU LAKINI POA HONGERENI MASHUJAA KWA KUONYESHA THAMANI YA WANAMUZIKI
ReplyDelete