As populations expand and food prices hit record highs, international investors are hoping to strike it rich in an unlikely place, Africa. We investigate one controversial deal, that some are calling a land grab, and the surprising cast of players involved - including one of America's oldest land grant universities. Dan Rather Reports airs Tuesdays at 8pm ET on HDNet.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwanza fadhila ya punda mateke! Huyu mkimbizi anayedai kwamba Serikali yetu imewaingiza katika mtego si arudi kwao ambapo sasa kuna serikali tena ya wahutu wanaotawala! Sijaona mkimbizi yeyote aliyekaa Tanzania ambaye anashukuru fadhila za nchi yetu na watu wake.

    Pili, swala la kuwahamisha si la ajabu. Hata wanaopata kupelekwa nchi za nje kwa mfano Marekani hawachagui wapi pa kwenda; aidha hawapelekwi wote kumoja! Iweje kwetu inakua tabu?

    Tatu, ilikuwa kosa kuwapatia hiyo haki ya urai kamili. Ni nchi yetu tu ina hiyo sera na bado tunatukanwa! Hawa jamaa wengi wanataka kwenda Ulaya hivyo kutoa kila kisingizio cha kutorudi kwao hata kama hali ya siasa sasa ni bora.

    Nne,hicho kimama kinadai si haki kutoa watu katika eneo wanaloishi! Ebo! Sasa limeshakuwa eneo lao!

    Tano, swala la kuanzisha mashamba ya biashara ni mtizamo ambao watu wengi tunaweza tukatofautiana. Hata Marekani rais wao anasutwa kutoridhia ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Canada. Sisi tumeamua kufanya eneo hili mashamba tupate chakula. Uamuzi ni wetu sio wa hawa wajanja wenye ajenda za miradi ya haki za binadamu!

    Sita, iwapo n i kweli hiyo bei tunayolipwa kwa ekari ni yakutizamwa. Shilingi karibu mia saba kwa ekari! Hapo Mhe Masha anatulalia?

    Mwisho, kumbe Mhe Masha kuwapa uraia kusije eleweka ilikuwa ni mpango vile vile wa kutwaa eneo kwa maslahi ya marafiki zake? Hapa pasije pakawa kuna mgongano wa maslahi!! Imekaa je hiyo?

    ReplyDelete
  2. Huu ni wizi ekari kwa $ 0.25 . Bado haija niingia akili kweli mpaka sasa karne hii tunaitaji muekezaji wa kutoka nje kwa ajili ya kutulisha hii aingii akili ni saw una nyumba yako na familia yako na wewe wanakutegemea halafu unakwenda kutafuta mtu mwingine aje awe bread winner wa nyumbani kwako kwa kukubali kuimiza familia yako aibu tu Tanzania.
    Maendeleo ya nchi yataletwa na watanzania wenyewe sio watu kutoka nje. Umewahi kuona wapi maendeleo ya familia yakaletwa na watu kutoka familia nyingine kama tu labda kuna interest fulani ndio inaweza tokea lakini zaidi ya hapo hakuna kitu.
    Mfumo wa soko huria ni mfumo mbaya hata wazungu wenyewe hawaupendi wana ulaini na sas wanafikiria mfumo mbadala.
    Watu kutoka nje hawatakuletea maendeleo zaidi ya kukutumia na kukuacha maskini. Serikali lazima ifikirie kuwa empower wana nchi wake kwanza sio kukaribisha watu kutoka nje na kuwapa ardhi kwa bei ya kutupa na hao watu wanje kunufaika na kila kitu . Wawekezaji kutoka nje wanataka kugeuza Africa shamba lao kwasababu population yao inaongezeka na chakula kwao hakitoshi tuwe makini na hilo sula nisisi wananchi tupewe nafasi tulime tuwauzie na sio wao waje walime halafu wachukue kila kitu wapeleke kwao wananchi wao wale.
    Serikali za nje zina wasaidia kuwapa mitaji waje africa na kuchukua maeneo kwa bei ya bure tuwe makini kwa hilo.

    ReplyDelete
  3. Kwa wale wanaofatilia vizuri hili swala,utaona kuwa sisi Watanzania tunaruhusu hili deal bila kuchukua muda na kufikiria. It is shame for our country.
    Naomba tujiulize tu faida zipi tunazipata? Na facts zipi?
    Agrisol energy some of their patners wameshaanza kujiondoa kwa kuwa wame danganya.Hawa jamaa hawana nia yoyote ya kuongeza au kuboresha chakula Tanzania ni biashara tu yenyefaida kwa kutumia mgongo wetu.

    Tanzania kilimo cha asili kitakufa,wakulima wata panda mazao yanayoleta faida tu/biashara na kuacha mazao mengine.Kutakuwa na unbalnce food production. Hatuna labs zinaweza kuchunguza Wadudu wanaotokana au kushambulia mazao yanayo tokana na Biogenitacally modified crops.

    Wakulima watanufaika vipi?hamna training na hayo mashamba sijui ni wakinanani wata ya tunza na kuendesha,wa southafrica?

    I think we are head of ourself.Chukua mfano wa similar situation in Mexico.Wakulima hawana
    Kazi na wanalima cocaine na bangi.Kwani kilimo cha asili kimekufa na hawawezi kushindana na hawajamaa.
    Wakulima hapa wanakuwa subsidize na huwezi kishindana nao.

    Msafiri kafiri.

    ReplyDelete
  4. hawa watu hawataki kuwarudisha wakimbbizi nchini mwao sasa wanakuja na hili. tanzania tusipo angalia hawa wakimbizi watakuja kutuletea shida baadae. hawa watusi wameshaanza njama za kuimega tanzania. wakisaidiana na wale wako kigoma, uganda, burundi na ruanda tutakiona. nina mararafiki toka rwanda na mara kwa mara huniambia tujiunge na shirikisho la east africa ili watu wao waweze kuamia tanzania kwasababu tanzania ina ardhi kubwa sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...