Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika jengo jipya la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga jana.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Madiwani wa Kata za Wilayani Korogwe, alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika jengo jipya la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa Mpunga kuhusu kilimo hicho cha umwagiliaji wakati alipotembelea na kukagua mashamba ya Skim Mamlaka ya mji wa Mombo jana.
Makamu wa Rais wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akikagua mitaro ya maji yanayotumika kumwagilia mashamba ya mpunga ya Skim, mji wa Mombo, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga jana Januari, 26, 2012, akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma ujumbe ulioandikwa na vijana wa Harakati ya Mazingira, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Mamlaka ya Mji wa Mombo kwa ajili ya kuwahutubia wananchi, akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga, jana Januari26, 2012. Kulia kwake ni mkewe Mama Zakhia Bilal na (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kombe, Kiongozi wa timu ya Mombo Shooting, Mohamed Dassa, kwa ajili ya timu hiyo iliyopanda daraja kutoka Ligi ya Ngazi ya Wilaya na kuingia Ligi Ngazi ya Mkoa. Kombe hilo pamoja na vifaa vya michezo vimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Steven Ngonyani ‘Maji Marefu’. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mh bilal wazanzibar wanakupongeza kwa kuzurura ovyo ovyo hilo ndilo tulilokutuma ukalifanye tanganyiaka

    ReplyDelete
  2. hii sio kuzurura. hii ni kutembea nchini mwako kukagua maendeleo. kwqkweli nina wasifu sana viongozi wetu kwa hilo. viongozi sio lazima wakae ofisini peke yake.

    ReplyDelete
  3. Hii matembezi kwenda sehemu mbali mbali nchini NA KUIONA HALI HALISI ILIVYO ndio jukumu lenyewe badala ya kupata taarifa KWA NJIA YA SIMU!

    AMA KUTEKELEZA MAJUKUMU KUTOKEA OFISINI KWA NJIA YA SIMU!

    ReplyDelete
  4. Huyu Mhe. BILAL ndio DAKITARI wa kiukweli aliyesoma akaelimika!

    Kwa kuwa yupo kivitendo zaidi kuliko ki nadharia na maneno tu,

    ''seeing is believing'' yaani kuona ndio kuamini, na ndio maana anapita kukagua kagua sio kupokea taarifa za kuchakachuliwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...