Chuo cha Maji kilipewa jina la aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Maji Fredrick Kilibata Lwegarulila kama kumbukumbu na kuthamini mchango wake katikakuanzisha chuo hicho.  Mchango wa Katibu Mkuu huyo katika wizara ya maji ulikuwa wa kupita kiasi.  Je Wizara ya Maji ilitumia utaratibu gani kufuta kumbukukumbu hiyo? Tutashukuru kupata ufafanuzi.
 Familia ya Lwegarulila

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. He heeeee..kwani kinaitwaje siku hizi?Kilishabadilishwa jina?Ngoja nisubiri maoni...hii nayo kali ya mwaka 2012

    David V

    ReplyDelete
  2. Tueleze ni mchango gani na ulipita kiasi kipi? Mkiwa kama wanafamilia, hamuoni kama kutakuwa na 'conflict of interest' katika shauri lenu?

    ReplyDelete
  3. Mie nilisoma pale 81 to 85 na nilikuwa sifahamu kuwa jina la Rwegarulila (please note R and not L)limeondolewa ktk Water Resources Institute. Ingawa nimebaki na memory negative na akina Mtayoba na Mnyanga & Co, na pia kulikuwa na uhaya saana ktk wizara ya maji, sioni umuhimu wa kubadilisha jina moreover kimya kimya tu. Hi 2 wana OKOA wote.....
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  4. Kwani hapa ndio kuna wizara ya maji?

    ReplyDelete
  5. Pengine tungepata kujuwa namna kumbukumbu hiyo ilivyowekwa kwa wakati huo ili tuweze kufahamu pia namna ilivyoondolewa, isije tu ikawa kuwa kila mtu akiwa na nafasi mahala fulani akisimamia kitu basi kiitwe jina lake. wangu mtazamo tu sina nia ya kubeza

    ReplyDelete
  6. elezeni ndugu yenu alifanya nini cha kumfanya awe tofauti na matibu wakuu wote baada ya uhuru, labda mnaweza mkapata wafuasi

    ReplyDelete
  7. Jamani hawa hawajauliza kwa nia mbaya.Vyuo,mitaa..viwanja vya ndege,hospitalishule,,nk kuitwa majina ya watu si suala la ukabila wala nini.Chuo kikuu cha Sokoine mfano.Hawa wanachouliza ni kwanini chuo kilibadilishwa jina?Hiyo ndiyo pointi muhimu mimi ninayoiona hapo.Kubadilisha jina siyo tatizo.,barabara ya Pugu ilibadilishwa jina na kuwa barabara ya Nyerere(Kulikuwa na sababu nahisi)..ndizo wanazotaka kufahamu hawa wanafamilia wala siyo kulazimishwa kiitwe jina la ndugu yao.Mimi ndivyo nilivyowaelewa..Walichosahau kutwambia hii familia ni kuwa kilibadilishwa kutoka hilo jina kwenda jina gani?Siyo wengi wanaoelewa.

    David V

    ReplyDelete
  8. Kufanya kupita kiasi si ndio wajibu

    ReplyDelete
  9. Nyie mnaowabeza wanafamilia, nadhani hamkusoma taarifa yao vizuri. Labda mmesoma kichwa cha habari tu. Kabla ya kuweka maoni yako fanya utafiti kwanza, siyo kukurupuka. Swali la kujiuliza na kutafiti ni je chuo hicho bado kipo? Kama kipo kimebadilishwa jina? Kadhalika hakukipa jina yeye, ni serikali iliyokipa jina hilo baada ya kutambua mchango wake. Mbona hamhoji kuhusu Sokoine University?

    ReplyDelete
  10. chuo kama kimebadilishwa jina-tunaomba tujuzwe,yaani ufisadi mpaka majina mnapora-itabidi nyerere afufuke

    ReplyDelete
  11. Haya. Wanfamilia wameuliza swali la ubdilifu wa jina. Mchezi momoja wapo kakimbilia ukabila. Hivi mpaka wakati huu watu bado wana ukabila Bongo?

    ReplyDelete
  12. Kujali Mchango ni muhimu sana, pia kama yeye Rwegarulira alifanya makubwa basi ni vema hayo makubwa yawekwe wazi ili umuhimu huo ounekane na yeye apewe hiyo Hadhi!

    ReplyDelete
  13. Du hawa jamaa wamenikumbusha hiki chuo; ni miongoni mwa list ndefu ya vyuo nilivyopita mpaka sasa; Wallah almost huwa nasahau kuwa kuna kitu kinaitwa RWRI (Rwegalulira Water Resources Institute); nilipita pale 1990-1994.
    Bila shaka ni hoja ya nguvu kuulizia vipi kibadilishwe jina; na nadhani si wakati wa kuuliza kwanini mwanzo kiliitwa RWRI kwa sababu huko tumeshapita; ama kama labda serikali imeona kuwa ilikuwa kosa kuitwa RWRI na wakabadilisha basi hasa ndio watwambie tatizo liko wapi.
    Hata hivyo naamini hawa wandugu si ving'ang'anizi au hawatakuwa ving'ang'anizi pindi labda wakifahamishwa kwamba labda kwasababu ya kwenda na wakati na kukitangaza zaidi hiki chuo ktk wakati huu wa ushindani mkubwa wa biashara hata kwenye elimu; ilifikia pahali ikaonekana hata jina linahitaji kufanyiwa polish kidogo ili lisaidia kukitangaza chuo.

    ReplyDelete
  14. Rahisi Sana Ndugu Kutetea ya Ndugu yao unauhakika gani kafanya mazuri na Mabaya hayapo kama kafanya zuri Kama Mwana Serikali ndio Kazi yake aliochaguliwa afanye kamaliza basi sio lazima kila kitu kisifiwe. Raisi Akifanya zuri ndio kafanya zuri sababu ndio kazi aliyewekwa afanye sio baya.

    ReplyDelete
  15. Hii ni mara ya kwanza Tanzania kusikia serikali imeondoa kumbukumbu ya kiongozi mzawa wa zamani mahali popote pale.
    Baada ya uhuru, serikali ilijitahidi kuondoa kumbukumbu tulizobandikiwa na wakoloni.
    Hapa kwetu Africa baadhi kumbukumbu uondelewa kama serikali imepinduliwa.
    Kumbukumbu pia inaweza kuondolewa kama chombo kimebinafsishwa.
    Mwaka 2008, bunge letu tukufu lilipitisha muswaada wa kuanzisha muelekeo mpya wa chuo cha maji. Kwa sababu moja au nyingine, nafikili hapa ndipo kumbukumbu iliponyofolewa.
    Msemaji mkuu wa Wizara ya Maji anweza kuchukua wasaa huu kuelezea kinaga ubaga kipi kilibidisha mabadiliko hayo na natumaini wanafamilia na yeyote mwenye haja ya kujua watakuwa mswano.

    ReplyDelete
  16. Nakubaliana na famili kwakutaka kujua,yaani leo wamenikumbusha mbali sana nilikuwa mtoto mdogo lakini nakumbuka huyu baba alivyokufa gafla na nakumbuka kulikuwa kunautatanishi kuhusu kifo chake,nilikuwa naishi jirani kurasi,mungu akuweke maali pema na nitafurahi kama familia watajibiwa swali lao ni familia nzuri sana,ingawa sasa tumepotezana.

    ReplyDelete
  17. The family has a point. When facts of such decision are not made public, one has every inclination to believe this was nothing but an act of ill will. It is a political equivalent of spitting on someone's grave; in this case a grave of a loved man, a family man who was also a dedicated civil servant. If you honored him in the first place, why dishonor him now? These are relevant and sensitive questions for the family. It is like removing the names "Mwaisela" or "Twalipo" from some of our revered public institutions. Why? for what? What point are you trying to prove? The man is dead! Since when has the government got into the business of dishonoring dead people? Even if some of the decision makers were preoccupied with their hatred towards the deceased man's ethnic group (as some of the comments here reflect), i am sure there are other "less malicious" ways to express your hatred towards this group and spare the family some pain. Wow, how low can we get?

    ReplyDelete
  18. Wanafamilia hii ni BONGO. Baadhi ya viongozi wetu wa dola ufanya maamuzi kama haya ambayo are simply unethical.
    It is more than likely hamtapewa jibu lolote. Serikali yetu ya BONGO haina muda wa masuala kama haya.
    Sisi tunaomkumbuka marehemu, na yote aliyofanyia serikali yetu hii, tunamwombea kwa Mungu. Thats the best we can do wanafamilia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...