Facebook ikiwa ni nyumba ya online kwa mamilioni ya watu duniani, hivyo mabadiriko yanayotokea kwenye facebook ni dhahiri yanaathiri wengi wetu. Katika siku za karibuni Facebook wamekuja na kitu kipya ambacho wenyewe wanakiitaTimeline , hii Timeline ni mpangilio mpya wa kurasa ya facebook ambao unamuwezesha mtumiaji kupanga picha,matukio nk kulingana na muda husika.
Picha inayoonesha muonekano wa timeline ndani ya Facebook.

Katika Timeline, utaweza kupanga taarifa zako kwa mtindo wa kipekee zaidi huku ikimpa nafasi mtembeleaji kuzipitia kwa haraka zaidi. Kama utaangalia picha ya hapo juu, utaona kwenye timeline ya Mdau ambapo mtu akija mara ya kwanza ataona marafiki,picha na mengine meengi. Siyo hayo tu, kwa kutumia timeline mtu anaweza kuangalia matukio yako toka siku ya kwanza uliyojiunga na facebook.

Katika siku zilizopita Timeline ilikuwa ni kwa wanaohitaji, ila kuanzia tarehe moja mwezi wa pili timeline itakuwa ni lazima, utake usitake ni lazima utumie au kwa lugha ya kiufundi tunaweza iita default. Hivyo usishangae kuona mabadiriko kwenye kurasa yako.


Kitu ambacho kimenivuta kuandika hii makala ni kuwa,ingawa timeline ni nzuri na ya kuvutia, ila Facebook inaonekana wanazidi kufanya mambo kuwa magumu,nidhahiri kuwa kufanikiwa kwa facebook kumekuja kutokana na urahisi wa utumiaji. 


Hivyo kufanya mambo kuwa magumu kutawafanya watu wengi kuikimbia au kushindwa kuifungua hususan wale walio kwenye mgao wa bandwith (internet zilizo taratibu mno). Kuna siku niliwahi kuona mpachiko wa rafiki yangu ambaye ni mtumiaji mzuri mno wa facebook, yeye alikuwa akilalamika kwa kusema nani amesema tunataka hii timeline?

Kitu kingine kikubwa ambacho kinaniumiza kichwa ni privacy, facebook wenyewe mara kibao wamekiri kuwa privacy ni moja ya vitu vinavyowaumiza kichwa, kwenye facebook ya sasa mtu anaweza kuona matukio yako ndani ya wiki hadi mwezi,ila sasa kwenye hii timeline mtu anaona tukio tangu siku ya kwanza uliojiunga facebook, sasa huku si kuwaumbua watu? 

Chukulia mfano kwa wale wenzangu na mimi wazee wa kuongopa, huu si ndio mwanzo wa kukamatwa? Hivyo basi kwa kuweka timeline kuwa default kutawatatiza wengi. Habari njema ni kuwa kuanzia sasa unaweza kuanza kufuta matukio kadhaa usiyopenda kuwaonesha watu hadi hapo januari 31.

Je wewe unalionaje hili?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kweli nakubaliana kuwa umaarufu wa facebook umekuja kutokana na simplicity kwa matumizi yake. imekuwa user friend kwa sababu inafunguka haraka. picha zipo condensed to mpg ama zaidi. kwahiyo hazitumii bytes nyingi. haili salio. lakini sasa hii time line mh sijui itakuwaje hata mimi nina wasiwasi kuwa inaweza kufanya watu hasa watanzania wakaamia kwenye mitandao kama tuiter, badoo na hata jamii forums ili tu kujaamiika pamoja. pius senyagwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...