![]() |
Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kuweka shada la Maua kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Regia Mtema aliyoongoza mjini Ifakara mkoani Morogoro leo. |
Rais Jakaya Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Regia Mtema ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Jimbo la Morogoro aliefariki kwa ajali ya gari maeneo ya Ruvu mkoani Pwani hivi karibuni .Rais Kikwete ameongoza mamia ya Waombolezaji wa mji wa Ifakara kwenye mazishi hayo leo ambapo pia viongozi mbali mbali walishiriki.
Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Regia Mtema aliezikwa leo Ifakara Mkoani Morogoro.
Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye mazishi ya Marehemu Regia Mtema yaliyofanyika Ifakara leo.Wengine pichani ni Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda (pili kulia),Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai (kulia),Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe, na kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
kaka hapa sipati picha kamili kwanini hivi viti vimepanisiwa au wanahofia visije kuzama kwenye udongo?kama wanahofia hilo hawa ni viongozi na wanapaswa kuwekewa viti imara kwa hadhi walokua nayo na si kuwekewa viti vya beni mdau wa zenji.
ReplyDeleteJK akitoka huko inabidi aunganishe Arumeru kwenye mazishi ya MH: Sumari
ReplyDeleteRIP
Kiti cheupe kilicho wazi kilikuwa cha Dr Silaha lakini nasikia amenuna bado na hivo alikataa kukaa karibu na Raisi wetu JK wala hakutaka kuonana nae uso bin uso.Ha ha haaaa!!!
ReplyDeleteRIP Mtema!!
viti vya kichina bei rahisi ila inabidi ununue viwili kukalia mtu mmoja maana ni hatari kukalia kimoja kitakuangusha.
ReplyDeletekimahesabu unarudi palepale, ila unakuwa navyo vingiiiiii.
huo ni mfano hai wa bidhaa vyenye viwango hafifu.
Mchina oyeee,bongo ziiiii