Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kuweka shada la Maua kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Regia Mtema aliyoongoza mjini Ifakara mkoani Morogoro leo.
 Rais Jakaya Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Regia Mtema ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Jimbo la Morogoro aliefariki kwa ajali ya gari maeneo ya Ruvu mkoani Pwani hivi karibuni .Rais Kikwete ameongoza mamia ya Waombolezaji wa mji wa Ifakara kwenye mazishi hayo leo ambapo pia viongozi mbali mbali walishiriki.
Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Regia Mtema aliezikwa leo Ifakara Mkoani Morogoro.
Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye mazishi ya Marehemu Regia Mtema yaliyofanyika Ifakara leo.Wengine pichani ni Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda (pili kulia),Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai (kulia),Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe, na kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kaka hapa sipati picha kamili kwanini hivi viti vimepanisiwa au wanahofia visije kuzama kwenye udongo?kama wanahofia hilo hawa ni viongozi na wanapaswa kuwekewa viti imara kwa hadhi walokua nayo na si kuwekewa viti vya beni mdau wa zenji.

    ReplyDelete
  2. JK akitoka huko inabidi aunganishe Arumeru kwenye mazishi ya MH: Sumari
    RIP

    ReplyDelete
  3. Kiti cheupe kilicho wazi kilikuwa cha Dr Silaha lakini nasikia amenuna bado na hivo alikataa kukaa karibu na Raisi wetu JK wala hakutaka kuonana nae uso bin uso.Ha ha haaaa!!!
    RIP Mtema!!

    ReplyDelete
  4. viti vya kichina bei rahisi ila inabidi ununue viwili kukalia mtu mmoja maana ni hatari kukalia kimoja kitakuangusha.
    kimahesabu unarudi palepale, ila unakuwa navyo vingiiiiii.
    huo ni mfano hai wa bidhaa vyenye viwango hafifu.
    Mchina oyeee,bongo ziiiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...