Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill Gates wakati wa Kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos, Switzerland.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Bw. Kevin Rudd wakati wa Kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos, Switzerland.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra wakati wa Kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos, Switzerland.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Walmart Bw Doug Mc Millon wakati wa Kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos, Switzerland.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Madame Sadako Ogata, Rais wa Japan International Cooperative Agency mjini Davos.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri Mkuu wa Kenya Mh Raila Odinga baada ya kufanya naye mazungumzo mjini Davos.
Rais Jakay Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron mjini Davos, Uswisi.Picha na IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. muheshimiwa umemwambia david cameron kwamba hatutaki ushoga

    ReplyDelete
  2. huyu jamaa kila wakati anatabasamu, ni nini kinacho mfurahisha (maghembe)?

    ReplyDelete
  3. Mbinu ya Mapambano,

    Ndio kama hivyo JK ni kukaa nao meza moja na kuwabana ili tunufaike kutoka kwao na sio wao watubane sisi!

    ReplyDelete
  4. MHH!! Kikwete na Cameroun tena??! Nilikuwa napita tu.

    ReplyDelete
  5. Tungeambiwa alichoonge na David Cameron jamani...

    ReplyDelete
  6. jamaa naona anangalia saa poroo zimekuwa nyingi nini?

    ReplyDelete
  7. hizo hela mi sidhani kama zinakuja serikali hizo nahisi zinapigwa panga huko huko! #ni mtazamo tu wadau msijenge chuki maana sioni maendeleo yoyote bongo tunazidi kuwa maskini.hao wajamaa hapo wanachinga dili zao

    David-muni
    manchester

    ReplyDelete
  8. Bill Gates alishawahi kutoa mada na kusema duniani kuna watu wengi sana, "ndio maana tunatafiti dawa za kuwapunguza." Angalia hapa kwenye YouTube: http://www.youtube.com/watch?v=12DmpWbMSTI&feature=results_main&playnext=1&list=PL641B19BE2505B3CC

    ReplyDelete
  9. Anoy wa pili..
    Inaelekea unamchukia sana Rais Kikwete maana hata heshima ya kumwita hutaki kuitoa.

    "Huyu jamaa kila wakati anatabasamu,ni nini kinachomfurahisha"

    Yaani unataka Raisi wetu awe kama lidudu vile yaani kanuna tu hivo ndio utafurahi.No way we like him the way he is.Raisi anapendeza awe mcheshi na mwenye tabasamu kwa watu wote na ndivo alivo Raisi wetu hachagui tajiri wala masikini.

    Good luck Mr President

    ReplyDelete
  10. Mh JK hapa ndipo anaponifurahisha,yeye huwa hataki gharama za misafara ya kukutana na kila kiongozi duniani,Husubiri hadi kuwe na mikutano ya kimataifa hupatia hapo hapo viongozi wa dunia nzima,au kasoma uchumi huyu?

    ReplyDelete
  11. Nimefurahi sana kujua Rais wangu anavyojulikana nje ya nchi na contacts zake na watu maarufu duniani.

    ReplyDelete
  12. mbona sijaona akikutana/kuongea na raisi wa nchi fulani? au mkutano uliudhuriwa zaidi na mawaziri na marais wa makampuni? nauliza tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...