Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa akiwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira katika jengo la Makumbusho na Numba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho Tanzania Bw Jackson Kihiyo akikaribisha na kuelezea Kazi, Mafanikio na Changamoto zinazoikabili Shirika la Makumbusho kwa Wabunge wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Mbunge wa Mafya Mh Shah akiushukuru Uongozi wa Makumbusho Tanzania na kuushauri, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw Hibrahumu Mussa na kulia ni Kaimu mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho Tanzania Bw Jackson Kihiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Aridhi, Maliasili na Mazingira na Mbunge wa Mafya Mh Shah akiangalia Sanamu sinazo elezea Biashara za watumwa na Maliasi zetu, zilizopo katika Ukumbi wa Historia wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Ardhi, Maliasi na Mazingira juu ya Fuvu la binadamu wa kale Zinj anae sadikika aliishi miaka milioni 1.75 iliyo pita.
Mbunge wa Viti maalumu CCM Mbeya Mh Dr Mary Mwanjelwa akiulizia jambo juu ya kionyweshwa katika Ukimbi wa Baiolojia wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, katikali ni Mbunge wa Matemwe Zanzimbar Mh Kheri Amer na kulia ni Afisa Tawala wa Shirika la Makumbusho Bw Fredrick Mwakalebela.

Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho Tanzania.

Makumbusho ya Taifa imeshauriwa kutunza kumbu kumbu muhimu za urithi unao shikika na usio shikika ambao hauja hifadhiwa hadi sasa na ukiwa hatarini kupotea ili ziweze kunufaisha vizazi vilivyopo na vya baadae.

Ushauri huo umetolewa na Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, aliasili na Mazingira ilipo tembelea makumbusho ya Taifa ili kujionea Shughuli mbali mbali za kimakumbusho ukiwemo mradi mkubwa wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam uliofunguliwa mwishoni mwa mwakajana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti maalumu CCM Dodoma Mh Mariam S. Mfaki, alipotaka kujua kama Mkumbusho imefanya jitihada zozote za kuhifadhi kazi na taarifa muhumu za wasanii walio liletea sifa Taifa hili akiwemo Hayati Mzee Moris Nyunyusa, Dr Paul Msemwa Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamauni alijibu kuwa Makumbusho imesha fanya jitihada hizo kwani kabla Mzee Moris Nyunyusa hajafariki alisha rekodiwa kwa njia ya sauti na Video, na hata Mzee Nyunyusa kuichangia Makumbusho Ngoma zake tatu kati ya zile kumi na mbili alizokuwa akizipiga, Aitha wasanii kama Marehemu Tinga Tinga kazizao na taarifa zinatakiwa zikusanywe.

Nae Mbuge wa Jimbo la Matemwe Zanzibar Mh Kheri Amer aliishauri makumbusho ifanye utafiti wakina kuhusu historia muhimu zinazo husu utawala wa kisulutani ulio husisha Tanzania Bara na Visiwani ili taarifa hizo ziweze kuwasaidia watanzania kuelewa vyema mahusiano hayo kwa minajili ya kuuimarisha Muungano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Pamoja na Kuupongeza Uongozi wa Makumbusho kwahatua mbali mbali za kimaendeleo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mbunge wa Mafya Mh Shah aluushauri Uongozi wa Makumbusho kuandaa Programu ya pamoja kati ya Makumbusho zilizopo Zanzibar na Tanzania Bara ili kuimarisha mahusiano ya kimuungano kama ilivyopo sasa katika sekta mbali mbali za Utalii.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho Tanzania, Bw Jackson Kihiyo, aliishukuru kamati hiyo kwa kutembelea Shirika la Makumbusho ya Taifa na kwa michango ya wanakamati na kuahidi kuwa Makumbusho itayatekeleza yaleyote yaliyo shauriwa na kamati hiyo.

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira walipata nafasi ya kutembelea kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na cha Kijijicha Makumbusho ambapo walipata nafasi ya kujionea shughuli mbali mbali za Makumbusho hizo zikiwemo za Uhifadhi, Uelimishaji, Uridhishaji kwa kupitia kumbi mbali ukiwemo ule wa Kisasa wa Maonesho ya Sanaa za Jukwaani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hawa jamaa wa kamati za bunge mi naonani wazururaji hamna lolote wanalofanya ........wanatumia kodi zetu kufanya utalii wa ndani,sidhani kama hizo ziara ziara zina tija kwa Taifa

    Adabrakadabra

    ReplyDelete
  2. Hizi kamati za bunge mbona zinatembelea mijini tu. Mara utasoma wapo MSD Mwanza, mara makumbusho n.k. Waende na vijijini wakaone wananchi wanavyoishi maisha yenye taabu. Wasingoje mpaka wakati wa kampeni wanapokwenda kuomba kula (kura).

    ReplyDelete
  3. vijijini hakuna hela. Wenzenu wanataka kukaa hoteli nzuri na kula posho za kutembelea makumbusho. Hakuna lolote wanalofanya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...