Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt Faustin Ndungulile (aliyevaa shati la kitenge karibu na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo, wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa mkoa huyo wakijitambulisha kuhusu kufanya ziara ya siku tatu mkoani humo kutembelea sekta ya afya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari Kuu ya Madawa nchini (MSD) Bi Eva Nzaro (wa kwanza kulia) akiwa na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Dkt Ndungulile (mwenye shati la kitenge) akimuongoza pamoja na wajumbe wengine wa kamati hiyo kwenda kutembelea bohari ya kuhifadhia dawa ya Kanda ya Ziwa iliyopo Jijini Mwanza.
Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii wakiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wao Dkt Ndugulile, wakimsikiliza Mkurugenzi wa kanda ya ziwa wa MSD akitoa maelezo namna wanavyoweza kuhifadhi dawa kisha kuzisambaza kwa wateja wao mbalimbali wa mikoa ya Mwanza, Musoma, Bukoba, Shinyanga na mkoa mpya wa Geita.
Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijiji mkoani Tanga (CCM) Stephen Ngonyani 'almaarufu Profesa Majimarefu' ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Huduma za jamii, akimsalimia mgonjwa Josephine Kalekwa aliyelazwa katika kituo cha afya cha Sangabuye kilichopo katika kata ya Sangabuye, wilayani Ilemela. Mwingine ni Mbunge wa Biharamulo Dkt Antony Mbasa (Chadema), wakati kamati hiyo ilipofika katika kituo hicho cha afya kuangalia matatizo mbalimbali.
Pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Ndikilo kulalamika kwamba kuna uhaba mkubwa wa dawa katika hospitali nyingi mkoani humo licha ya MSD kuwasilishiwa fedha lakini wajumbe wa kamati hiyo walishuhudia shehena na mabox ya dawa yakiwa yamehifadhiwa kwenye bohari hiyo ya madawa kanda ya ziwa.Picha na Mashaka Mhando wa Globu ya Jamii-Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Matatizoya matibabu kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na viongozi na matajiri ambao ni wachache,wakiugua huenda kutibiwa nje kwa hiyo kipaumbele cha huduma za afya nchini hakipo,ingekuwa serikali imepişga marufuku kuenda kutibiwa ncje kiholela basi wangelazimika kuboresha huduma za afya nchini

    ReplyDelete
  2. HAPO KAZI YA BOX NITAKOSA KWELI NA UJUZI WAKUPIGA BOX NCHI ZA NJE NIPATIENI NUMBER ZAO ZA SIMU NA ANUANI.

    ReplyDelete
  3. Waheshimiwa wetu wanafanya ziara ili kuongeza kipato kwa kuwa maisha kwao ni magumu na si kwa Watanzania wote. Haya twendeni jamani ingawaje tutafika choka ile mbaya.

    ReplyDelete
  4. ukisikia box wajomba ndo hilo tunalokufa nalo wadau majuu. keching kila wiki unakomba zako £400 keching unalala yombo.
    watu hawabebi box, ni conveyor belt au rollers nd'o zinafanya kazi hiyo. halafu zinapelekwa kwenye pallet huko kuna robot inayofanya kazi ya ku-stack to the required amount-kama box 50 kwa pallet au less inategemeana na ukubwa wa box.
    kila kitu wadau ni wewe na kompyuta. ndiyo ukisikia watu wanakula box! tanga kama ulaya vileeee

    ReplyDelete
  5. Dawa silizo-expire!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...