AL'MARHUM MZEE ESMAIL MANAMBI CHOKA ( SEPTEMBA 06, 1947 - JANUARI 23, 2011) |
Hatimaye siku , miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia mwaka mmoja (1) tangu ulipofariki bila ya sisi kutarajia Alfajiri ile ya siku ya Jumapili, Januari 23 , 2011.
Kwetu sisi kifo chako kimetuachia butwaa na hali ya kutoamini kilichotokea na majonzi endelevu kwa kipindi chote cha hiki cha mwaka mmoja.
Hakika tumezikosa bashasha zako , busara na hekima zako na kwa hivtyo basi unakumbukwa sana na Mama yako Mzazi ( Bi Hafsa Issa Kihenya), Wadogo zako ( Issa, Midladjy na Mwajelah) Watoto wako wapenzi Manambi, Masayanyika, Usamah, Natasha, Bahati, Himidi, Jamilu, Hawa na Buhari pamoja na Ndugu, Jamaa na Marafiki lukuki.
Ingawa kimwili hauko nasi , lakini sisi tunaamini kuwa kiroho uko nasi kutokana na misingi bora ya kimaisha uliyotuachia tuizingatie na kuifuata.
Tutaendelea kukukumbuka daima siku zote za uhai wetu, wakati huo huo tunakuombea Mwenyezi Mungu aendelee kuiweka roho yako mahali pema peponi.
INNALILLAH WAINA ILLAHIY RAJOOUN!
Allahumma Ghufir-Lahu...Allahumma thabituh.
ReplyDeleteAl-Marhum Sheikh Manambi kama nitakuwa sijakosea ni baba wa ndugu yangu Esmail.
Mwenyezi Mungu amraham yeye na wazee wetu pamoja na jamii Muslimina. ndungu zangu mlioondokewa na Mzee wetu huyu Mwenyezi Mungu akupeni subra kubwa na akulipeni thawabu kwa kusubiri kwenu.Kubwa msiwache kumkumbuka kwa duaa.Kwani ndio mapenzi kwa Maiti zetu kwani wao wapo karibu nasi kila wakati wakizihitajia duaa zetu.Kwa hiyo tusiwache kuwakumbuka Maiti zetu kwa duaa.

Pole sana Usama Choka kwa msiba mzito uliokupata wa kuondokewa na baba. Ulimpenda sana baba lakini Mola amempenda zaidi. Poleni wana familia.Baba apumzike mahala pema peponi.
ReplyDeleteApumzike kwa amani.
ReplyDeleteHujakosea kabisa Sheikh Khalfani,Dua ni kitu kikubwa na tunamuombea kwa mwenyezi mungu!
ReplyDeleteEsmail.